Ni ujinga na umasikini tu unawasumbua watu!
shida kubwa ni ubongo wenu, umejaa matope ya udini na utumwa wa fikra. mwarabu kwenu ndio malaika. sisi tuliowengi, hasa watanganyika, hakuna hata mmoja anayepinga mwarabu kuwekeza. tunapinga vipengele vya mkataba, haviko sawa. wakiweka vipengele vikawa sawa nakuambia hakuna mwekezaji bora kama Dubai, nani asingependa awe connected na bandari ya dubai ambayo ipo busy sana, wao wana connections za meli nyingi toka ulaya, japan na china n.k, hivyo ukiungana nao meli zinazopitia kwao na hasa kama wao hapa ndio wanaoiendesha bandari meli hizo watazielekeza hapa na bandari yetu itakuwa busy sana na mapato yatapatikana. kwa kifupi, connection ya Dubai ni hot cake kwetu na hakuna mwingine anayeweza kuwa bora kuliko dubai kama hatutakuwa tumejenga bandari ya bagamoyo.
shida ipo hapo. na ukumbuke, Oman ambao ni waarabu na wajomba zako walishasainiana na China kujenga bandari ya bagamnoyo, kwani hao sio waarabu? waoman ni waarabu tena hapa Tanzania waarabu waliopo wengi ni asili ya Oman na Yemen. hao walitaka kujenga bandari ya bagamoyo ili nao wawe kama Dubai, yaani meli zikitoka China kuja Afrika, zisipitie dubai, zipite moja kwa moja hadi Oman, na toka Oman zije Bagamoyo (and you know Oman wanaijua sana bagamoyo na route yake kwasababu wameendesha sana biashara ya utumwa na bagamoyo ilishakuwaga mji wao wa kibiashara hapo kale),...hivyo Oman nao wangekuwa busy kama ilivyo dubai kwasababu meli toka china ni nyingi sana.
sasa Dubai kuona kitumbua kinataka kwenda Oman na china kwenye bandari ya bagamoyo, ndio kaja na mkataba kwamba yeye akikamata bandari ya Dar es salaam basi tusijenge bandari zingine bila yeye kuambiwa, yaani tumwombe ruhusa kwenye nchi yetu. maana yake ni kwamba, hataki bandari yeyote ijengwe hapa bongo itakayoshindana naye, au kwa lugha nyingine, hataki Oman (mwarabu mwenzake) ajenge bandari kwa kushirikiana na china, bandari ya bagamoyo waliyokuwa wanataka kujenga ambayo ingepunguza biashara yake ya usafirishaji pale dubai.
kwa hayo machache, hebu jifikirieni muone hakili zenu zilivyojaa funza, na mnachowaza siku zote ni udini na mwarabu tu, ndio maana tulisema hata mwarabu akitoa harufu huwa mnasema hiyo ni pafyumu tu. Kama tunamtaka Oman, utasema tunachukua waarabu? kwani Oman ambao wana ndugu wengi sana Zanzibar na bara sio waarabu? hamtaki Oman naye awe Dubai? au kwa akili zenu fupi mnafikiri yale maendeleo yaliyopo pale Dubai atayahamishia kama yalivyo hapa bongo kwa kuyakopy na kuyapaste? mbuzi zingine hazinaga akili kabisa kabisa.
fikiria haya hapa chini;
1. Dubai wapewe DSM port, waendesha kwa ufanisi sana.
2. Oman na china pia wapewe ridhaa ya kujenga bandari ya Bagamoyo ili washindane na DP world, huu ni ulimwengu wa ushindani, sio wa monopoly kama ilvyokuwa enzi zileee? watu washindanishwe na huduma zitakuwa bora zaidi.
3. mtu mwingine yeyote apewe bandari yeyote, iwe ya Tanga au mtwara, aendeshe zishindanishwe na bandari zingine, hiyo ndio capitalism, uwepo uwekezaji wa kiushindani, wawekezaji wawepo wengi washindanishwe kwa huduma, sio mmoja ili awe ndio final say, akishindwa yeye uchumi wote unaporomoka hadi asimame tena.
lakini hiyo haiwezekani kwasababu dp world hataki bandari ya bagamoyo au ingine ijengwe isije kushindana naye. na kama hakutakuwa na bandari shindani basi yeye atakuwa mungu mdogo atakayefanya lolote atakalo kwasababu tukimzingua atatuadhibu kwa kupitia bandari. hivi akiamua tu kuhujumu miundombinu akasema bandarini kunahitaji ukarabati hata mwezi na hakuna bandari ingine inayooperate, mwezi mzima tunamtegemea yeye tu, hali itakuwaje? unampa mtu monopoly ya kitu kwenye nchi yako? badala ya kuweka ushindani ili mmoja akizingua mwingine anafanya? unakabidhi uhuru wako wooote kwa dp world, ulishasomaga history zile enzi za monopolism? ndio hizo sana, ambazo mtu mmoja au watu wachache wanweza kuponopolize uchumi wakakufanya chochote ukawa mtumwa kwenye nchi yako, tutakuwa watumwa wa dp world hata akifanya chochote hauwezi kumfanya lolote kwasababu bandari zoooote ziko mkononi mwake. hivyo ndivyo samia na mbalawa wanavyotaka iwe? usalama wa taifa upo wapi kufikiria kwa mawazo kama haya?