Kipigo cha Polisi, Halima Mdee apima na kukuta kavunjwa mkono wake wa kulia

Kipigo cha Polisi, Halima Mdee apima na kukuta kavunjwa mkono wake wa kulia

Kwa mwendo huu uhalifu hauwezi kuisha nchini,Kama polisi wanachukiwa na raia na hata kuwaogopa,lini watatoa ushirikiano chanya kwa jeshi letu..
Na Kama wangekuwa wanafanya kasi kwa akili bila kutumia nguvu,idadi ya polisi ingekuwa inatosheleza mahitaji kea 100% maana kazi nyingi za kiuhalifu wangekuwa wanashirikiana na raia Tena kwa kiwango Cha Hali ya juu.
Polisi wanachukiwa na cdm. Kwasababu cdm wamekuwa watetezi wa kila uovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo ana mapungufu ila JK alikuaga ana akili sana, yani anawaacha msemeee we ye anajua atawashika wapi.
Lakini si unakumbuka walivyokuwa wanamtukana JK, na mwisho wakamwita ni rais dhaifu/goigoi. Ina maana ule udhaifu haukuwa wa mtu binafisi kama JK bali ni taasisi ya urais, na taasisi ya urais ni pamoja na mifumo yote ya nchi.

Na ndiyo maana sasa taasisi hizo zikaonelea ni bora kuthibiti vimelea vya uvunjifu wa amani, ni muhimu kuviua hivi viashiria ili tuwe na taifa la wapenda nchi na washindani wa hoja. Huwezi mkuta mzungu anasaliti nchi yake kwa maslahi ya nchi nyingine, ndiyo maana wapinzani wetu wanazidi kupukutika kwenye umaarufu na bado!

Hata awamu ya 5 ikiisha mziki ule ule, lazima hivi vimelea vya wapinzani tumbo viangamizwe vyote ili waje wapinzani wa kuheshimu mamlaka.
 
Kwani walikuomba hiyo lift, walipungukiwa nin kukosa lift yako, utoto huo
Sipendi kbs siasa ila nawachukia sana polisi ambao hawana nidhamu ni watu wajinga sana. Sasa hapo utajikuta wanapongezana kwa ujuha wao waliofanya. Kuna siku mvua inanyesha kuna polisi wawili niliwanyima lifti kwa makusudi kbs. Kwanza toka lini askari anaogopa mvua. Ukweli siwapendi hawana msaada kbs na raia.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GODZILLA,
Je! Wewe umepigwa? Jibu ni hapana. Kwa sababu hukwenda magereza kuvunja amani! Halima alikwenda kule kusudi aoneshe uhodari wake na udemokrasi wake! Sasa tumuhurumie na tuwatukane walinda amani!
 
Hizi mambo za Polisi kupiga raia in the name of kulinda amani au kuzuia vurugu tushazisikia sana, zishalalamikiwa sana na hakuna kinachobadilika, walimuua Akwilina watu wakasema wee, bado vinaendelea iko siku wananchi watajachukua sharia mikononi mwao…….Polisi wenyewe tunaishi nao mitaani, ni majirani zetu, watoto wao wanasoma na wenetu, wake zao wanashiriki vikoba nasi...…...iko siku.
Una mtusha nani?
 
Niliwahi kusimamishwa na traffic, katika utetezi wng nikataja na Taasisi ninayofanya kazi, jamaa akanpotezea! Nikamuomba apokee ID aisome ili aamini! Alichonijibu yule askari..... ngoja ninyamaze ila nilielewa why wakianza kupiga wanapiga kama wameekewa Figo za Afghanistan!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila nikiangalia hii picha ya x-ray najisikia natetemeka. Tazameni jinsi mhe Halima Mdee walivyo mvunja mkono hapo kwenye picha chini.

Huu ni zaidi ya ukatili ulio putiliza jamani watanzania wenzetu. View attachment 1388478

In God we Trust
Tupe tafsiri ya hiyo x ray picha we ni Doctor. Au mnatafuta public sympath sababu uchaguzi mmeshindwa.Propaganda za kishamba
 
Back
Top Bottom