Nimekuambia Mungu ni dhana ya kufikirika isiyo na uhalisi nje ya ulimwengu wa dhana tu.
Kama unabisha, taja Mungu yeyote ambaye yupo nje ya ulimwengu wa kufikirika tu.
Ukiniuliza dhana gani ya kufikirika, itabidi unitajie Mungu gani, kwa sababu kila Mungu ni dhana tofauti ya kufikirika, na hivyo swali la dhana gani ya kufikirika bila kumtaja Mungu halina mantiki.
Sasa jibu swali.
Taja Mungu ambaye yupo nje ya dhana ya kufikirika tu.
Ukishindwa, umeshindwa kukanusha kwamba Mungu ni dhana ya kufikirika tu.