Kisiju mkoani Pwani watu wanaswali kuliko kazi

Kisiju mkoani Pwani watu wanaswali kuliko kazi

Ilikua ni kabla ya mwaka 1993. Inasemekana kuna ngalawa au mtumbwi ulipunduka huko Commoro, sasa kama ilivyo kawaida, watu wa Pwani wana msemo unasema bahari haikai na uchafu.

KIle chombo kilichozama kilikua na mzigo mkubwa tu, mzigo ule ulisukwasukwa na mawimbi hadi mizigo mingine ikatokea Pwani ya Kisiju. Katika mzigo ule kulikuwepo na vinywaji vilivyokuwa kwenye kopo.

Pakawa na udadisi sana kuhusiana na kilichokuwemo mule ndani. Hapo mzigo upo mikononi mwa wazee wanao heshimika na kule wazee wanaoheshimika na Shehe, Imam, Ostaadhi na wengineo ambao ni viongozi kwenye dini na wazee ndani ya jamii[emoji3].

Wakati wanajiuliza kuhusu kilichomo mwenye vikopo vile, ikabidi akatafutwe kijana mmoja ambaye ndiye allikua ni mjanja mjanja pale Kisiju maana alikua ni mtu wa kuvuka sana, yaani kwenda sana mjini[emoji3] (Mbagala na Mkuranga 1991 - 1993)[emoji2].

Kijana alipoitwa, akawekwa kati na wazee ambapo wakamuuliza kuhusu vile vikopo. Kijana wa mjini alipoviangalia, akawaambia "aaah hizi ni fanta, ni soda tamu sana hizi" kijana akafungua, akaonja mbele yao akaomba na vikopo kadhaa aondoke navyo wakampatia vikopo vinne akasepa.

Wale wazee kwa kuwa palikua na cartons za kutosha wakaugawa ule mzigo haki bin haki na hata wasiokuwepo wakapelekewa. Basi wazee ma Mwinyi wakaanza kunywa fanta kikopo kimoja baada ya kingine.

Ikafika muda wa azana kimya, muda wa azana nyingine kimya...wanaanza kutafutwa viongozi msikitini wote hawapo, kuanzia Muazini hadi Mnadi swala, waumini ni mmoja mmoja. Walipowafuata majumbani wanakuta watu hawajitambua, kuja kustuka na kurudiwa na akili ni kesho yake.

Ikabidi kiitishwe kikao waulizane ni kipi kilitokea na yule kijana mtaalamu wa mjini naye akaitwa. Wakamleta wamembeba. Maana yeye baada ya kikopo kimoja alitulia , siku hiyo asubuhi ndiyo akanywa.

Yule kijana akaulizwa ina maana wakinywa fanta ndiyo inakuwa vile? Katika vitu viliwakwaza na kuwakasirisha wale wazee ni siku kupita bila azana na kwa ukubwa wa mzigo karibu waumini na wananchi wengi walikua bwii. Wakiulizwa nini kimetokea wanajibu kwa sauti ya kilevi "Fantaa", wakiulizwa ndiyo nini na imefanya nini wanajibu tena "Fantaa".

Katika kujadiliana Ilibidi wazee wafikie muafaka wa kuipiga marufuku Fanta pale Kisiju, na hatua kali kuchukuliwa kwa yeyote atakayekutwa anakunywa au hata kuileta Fanta pale Kisiwani.

Kumbe walichokuwa wamekunywa siyo Fanta bali ni beer aina ya Stella Artois ya vikopo ambayo ilikua maarufu sana miaka ile[emoji2]View attachment 2782313
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kule hakufai kabisa. Pamesahaurika sana. Watu hawaendi shule, badala yake ni Madrasa, akipiga zake Madrasa miaka minne tayari ni msomi wa heshima.
Kinywaji adui kuliko vyote kule ni 'Fanta'😃. Fanta ina historia yake kule😀
Mkuu tusimulie tusioifahamu hii historia, usije jikuta unaenda Lindi siku moja unabaki unatoa macho tu
 
Kodi inayolipwa Kilimanjaro na Kariakoo inatumika kujengea watu wavivu shule na vituo vya afya huko Kisiju
Kwenye mikoa yenye kipato kikubwa Kilimanjaro ipo?

Kariakoo ni sehemu ya mkoa wa Dar es salaam ambayo ni Pwani.

Hivyo ni sahihi pesa ya watu wa Pwani kuendeleza wa Pwani wenzao Kuna tatizo gani?
 
Mkuu umeongelea umasikini wa mkoa wa kagera sijui nawe ulikua una lenga kipi kati ya hivyo ulivyo taja ila mimi nilikujibu interms of gdp per capital.
Bado Kagera ipo chini
Sababu ya umasikini Kagera ni pamoja na ugonjwa wa Mnyauko wa migomba na ndilo lilikuwa zao la kiuchumi na chakula.

Kuvurugika kwa Soko la kahawa
Na serikari kutotoa ajira kwa kipindi Cha miaka 6 iliyopita.
 
Hoja ni kujifanya kuswali swala zote ilihali mtu ni Mchawi na mshirikina.

Huko kwingine wachawi wapo lakini hawaswali kiivyo swala zote,

Mtu anae swali/Sali inatarajiwa awe mtenda mema ,
Mtu asojaa husuda na chuki zidi ya mtu mwingine,
Lakini mtu anajifanya kuswali/kusali ilihali moyoni ni muovu muuaji inafaida gani?!

Ndiyo maana maendeleo yanachelewa na nchi kuwa gizani pamoja na kupata Uhuru kwa zaidi ya miaka 60
Hukuwahi kusikia wazee wa kanisani ndio magwiji wa uchawi?

Katembelee Sumbawanga [emoji15][emoji15][emoji15][emoji15]
 
Kwenye mikoa yenye kipato kikubwa Kilimanjaro ipo?

Kariakoo ni sehemu ya mkoa wa Dar es salaam ambayo ni Pwani.

Hivyo ni sahihi pesa ya watu wa Pwani kuendeleza wa Pwani wenzao Kuna tatizo gani?
Kilimanjaro TRA 2022 walikusnya bilioni 240 ni walipa kodi wakubwa nyuma ya Dar na Arusha!

Kungekuwa na serikali za majimbo hii mikoa watu wanaocheza tu bao hawazalishi chochote wajiongeze!
 
Hapo ndipo waislam wanapokosea.

Wanaamini sana imani yao kuliko uhalisia wa mambo.

Allah hawezi kukuletea maendeleo ama kukusaidia kama wewe hujitumi.

Mfano israel anambonda mpalestina. Waislam wa nchi jirani na palestina na duniani wamebakia kusema Allah Akbar tu. Badala ya kushika mitutu kwenda kumsaidia mpalestina kupigana.

Hizi dini tulizoletewa ni myth tu


Mataifa ambayo hawaziabudu wala kusali ndio wenye maendeleo.

Maendeleo yamekuja sababu wanafanya kazi kwa bidii

Japan, korea na China hawamjui Yesu , wala mtume Muhammad ila wanaendelea kwa spidi.

Sasa kisiju watu wanashinda kwenye swala halafu wanataka maendeleo. Yanakujaje ?
Mbona unahukumu vitu kirahisi hivyo? Hivi yule msandawe anaeiishi porini hana habari ya facebook, Instagram wana social media zenu. Hawazi kodi ya nyumba, umeme, maji wala gharama za usafiri kwenda kazini na anaishi poa kwa furaha amani na utulivu.

Wewe uliyezoea maisha yako ya kimjini mjini ukienda kumkuta huko porini utamuona amechelewa, anapata tabu, Hana malengo Hana future na mengine mengi.. Hivi ni kweli anateseka kama unavyomhisi wewe au ni mtazamo wako tu.!?

Hivyo ndio inavyokuwa hata hao waislam huko kimbiji hayo maisha wanayoishi ndio maisha yao na they are happy. Ila wewe mwenye mitazamo tofauti ndio utawaona tofauti na kujaribu kuwahukumu kulingana na mitazamo yako. Kipindi nao wao wakiona maisha yako wanakushangaa na kukuona unapotea.. So ni kuwaacha tu na maisha yao as long as hawavunji sheria za nchi.
 
we kafanue mambo yako hakuna unayemlisha. Huko Unakokutaja Kilimnjaro kuna wazembe, wavivu na walevi wengi tu acheni kudanganya watu. Kwanza Kilimanjaro hasa wachaga hawafanagi kazi nguma za uzalishaji wao kazi yao kubwa ni uchuuzi. Hakuna watu wavivu km wachaga, wazalishaji kule kaskazini hasa ni wairaqw na wamasai ndio wenye mashamba makubwa ya kilimo na ufugaji ingawa huwezi kusikia wakipiga kelele za kujisifu. Wachaga lilikuwa kabila dogo tu lilokuwa ndani ya wilaya ya Arusha wakati Northern province ikiwa na wilaya 2 za Mbulu na Arusha. Hata sahivi bado kabila la kawaida ila lenye kupenda kujisifu kwa mambo madogo mno, ni kwamba hamjiamini. Post zenu za hovyo zinakera humu JF badilikeni acheni upuuzi wa kujisifu na kudharau makabila mengine ambayo hata yamewazidi mali sema hawataki maonesho
Ufahamu wako kidogo sana kuhusu Wachaga!
Unafahamu mashisika haya ni mali ya nani? Precision Air, Mabasi ABC, BM, Kilimanjaro, Dar Express, Viwanda Cococola, Bank ACB nk.nk. nk. Duka la Mangi ni kila sehemu Hapa Tanzania?
Hawa watu ni maskini?
Jifunze kuwafahamu watu kwanza ndo uje hapa!
 
Kusali sana hakuondoi umasikini.
Kufanya kazi sana bila Mungu nako ni ubatili.

Kila kitu kinapaswa kuwa na kiasi...
Kusali kiasi, kazi sana lakini ibada muhimu
 

Attachments

  • IMG-20231031-WA0014.jpg
    IMG-20231031-WA0014.jpg
    86 KB · Views: 20
Kilimanjaro TRA 2022 walikusnya bilioni 240 ni walipa kodi wakubwa nyuma ya Dar na Arusha!

Kungekuwa na serikali za majimbo hii mikoa watu wanaocheza tu bao hawazalishi chochote wajiongeze!
Baada ya Dar es salaam ni Mwanza, mbeya, hiyo Arusha haipo tatu bora.
 
Back
Top Bottom