Kisutu: Tundu Lissu ashindwa kutokea Mahakamani, kesi zake zaahirishwa hadi 26/08/2020

Kisutu: Tundu Lissu ashindwa kutokea Mahakamani, kesi zake zaahirishwa hadi 26/08/2020

Huyu huyu aliyekuwa anasema kazuiwa kwenda msibani leo excuse ni isolation! I ama a kwenda kuaga mwili angewakilishwa na ghost wake? tukiwaambia jamaa ni empty headed mtabisha. I hate people who cares the most about cheap publicity.
Hayo mengine atajijua mwenyewe sisi tunachojua kuanzia tarehe 26/08/2020 tunaanza kumsikiliza akijinadi na tarehe 25/10/2020 tunachukua kalamu tunaweka vema kubwa kwake full stop!
 
Ana maneno ya kichonganishi sana huyu wakala wa mabeberu
 
Lissu aliyokuwa hayupo walipumzika sana Sasa hivi watakuwa wanalala hoi wengine ni kwa mawazo tu kuwa wanavhokitaka kwa Lissu ni sawa na kutaka maji baridi jangwani.
 
Hizi kauli ndio anataka apewe nchi? Kauli za kuudhi, kibaguzi na sio za kiuongozi. Huwa nasema jamaa hafai hata kidogo kuwa raisi wa nchi. Ndio wale class tulikuwa tunawaita "much know".

Note: Kunusurika kuuwawa isiwe sababu ya mimi kumuonea huruma na kumpa kura yangu. Huruma isihusishwe na kura yangu.

Rais alikuwa huko Lindi anatoa kauli zisizo za kibaguzi kuwa watu wa huko wachague mtoa rushwa mwenzake wa ccm, maana kuchagua muadilifu wa upinzani hataweza kufanya naye kazi!
 
Lissu Bana akili kubwa naye kaamua awapotezee siku eti kashauriwa akae karatini kujua sharia Raha na mtu kukunea ajipange
 
Salaam Wakuu,

0911HRS: Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu hajatokea Mahakamani kama ilivyotarajiwa kwenye kesi inayomkabili namba 123 ya 2017 mbele ya Hakimu Mheshimiwa Enock Matembele.

Wakili wa Utetezi Peter Kibatala, ameiambia Mahakama kwamba Tundu Lissu alikuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu, amerudi majuzi (Jumatatu). Kutokana na hali yake, ilishauriwa apate mapumziko (isolation/karantini) aweze kuangalia afya yake, hivyo tunaomba tarehe nyingine, tunaamini siku hiyo atakuwepo.

Mawakili Upande wa Jamhuri, Wakili Mkuu Renatus Mkude na mwenzake Wakili Wankyo Simon (Wakili Mwandamizi) hawakuwa na pingamizi, hivyo kesi imeahirishwa hadi tarehe 26 August 2020.

Hii kesi ina Makosa matano

KOSA LA KWANZA

Kwenye kesi namba 123 ya Mwaka 2017, inadaiwa tarehe 11January 2017 Tundu Lissu akiwa huko Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar katika Kampeni za Uchaguzi huku akiwa ni raia wa Tanzania Bara, aliongea maneno ya kuwaudhi Waislam, alisema;

... "Kwahiyo hicho kunachoitwa Uchaguzi wa marudio uharamia mtupu, haramu, haramu, haramu.. Kinachoitwa Uchaguzi wa marudio ni haramu tupu... Nyie ni Waislam sana naomba niseme uharamu wa Uchaguzi wa Marudio wa Mwaka jana hautofautiani na kula nguruwe, kwa wala nguruwe hawa, wala nguruwe hawa, nlikuwa nazungumzia yaliyokuja baada ya wala nguruwe hawa kufanya uharamia wao.. Laana tullah'

KOSA LA PILI

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Tangu 1964 Tanganyika ndiyo inaamua nani atawale Zanzibar".

KOSA LA TATU

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Tangu mwaka 1964 Zanzibar inakaliwa kijeshi na Tanganyika, nani anayebisha... Tangu mwaka 1995 ikifika Uchaguzi askari wa Tanganyika wanahamia Zanzibar ili kuja kihakikisha Vibaraka wao wa Zanzibar hawaondolewi Madarakani na Wananchi wa Zanzibar mnapigwa, mnateswa, mnauawa kwa sababu ya Ukoloni wa Tanganyika kwa Zanzibar...., Marehemu Karume alipoanza kushitukia mwaka 71, 72 akauawa...., itakapofika tarehe 15 mwezi wa kwanza muadhimishe mika 53 ya kukaliwa Kijeshi na Tanganyika"

KOSA LA NNE

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Jumbe aliondolewa Dodoma, Ally Hassan Mwinyi alipewa Urais Dodoma, na aliyempa ni Nyerere sio Wazanzibar.., Marais wa Zanzibar wote ni made in Tanganyika..
.., wametengenezwa Tanganyika, wanakaa madarakani kwa sababu ya Tanganyika...,

KOSA LA TANO

Tarehe 11 January 2017 Kombeni Mjini Magharibi Zanzibar wakati wa Kampeni za Uchaguzi alisema;

"Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika kwa kivuli cha Tanzania, Tanzania ni Tanganyika..., Tanzania ni kivuli cha kuikalia Zanzibar, cha kuigeuza Zanzibar Koloni na Makoloni huwa yananyonywa, Makoloni yanatawaliwa, Kisiasa yananyonywa Kiuchumi na yanakandamizwa Kijeshi..., metawaliwa kisiasa na Tanganyika miaka yote hii.. Ali Mohammad Shein hatufai tena ataondolewa kama Aboid Jumbe alivyoondolewa.... ".

NOTE: Leo hapa Kisutu watu hawaruhusiwi kuingia isipokuwa wenye kesi na Mashahidi tu. Ulinzi ni Mkali wa Polisi kila sehemu hapa Kisutu. Hawataki mtu asogee.

=====

0925HRS: Sasa tunaingia Kesi ya Pili ya Lissu Open Court #2.

Hii Kesi ya Pili tupo kwa Hakimu Mbando.

Kesi inayo mkabili Tundu Lissu namba 236 ya mwaka 2017 ya Uchochezi imeahirishwa hadi 26 August 2020. Sababu za kutokufika zinafanana na kesi ya Kwanza.

Kwa leo kesi zake zote zimeahirishwa.

Katika kesi namba 236, inadaiwa Tarehe 17 July 2017 Maeneo ya Mtaa Ufipa Kinondoni, Tundu Lissu aliongea Maneno ya kuudhi kwamba "Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ni ya Kibaguzi wa Kifamilia, Kikabila, Kikanda na Kidini. Vibali vya kazi Work permit vinatolewa kwa wamishenari wa Kikatoliki tu huku Madhehebu mengine yakielezwa kupanga foleni Uhamiaji. Viongozi Wakuu wa Serikali wanachaguliwa kutoka kwenye Familia, Kabila na Ukanda... Acheni woga pazeni sauti.. Kila mmoja wetu.. Tukawaambie kama tulivyo waambia Serikali ya Makaburu, hii Serikali Isusiwe na Jumuiya ya Kimataifa, isusiwe Kisiasa, Kiuchumi na Kidiplomasia kwa sababu ya Utawala huu wa Kibaguzi.. yeye ni Dikteta Uchwara".

Mwisho.
Mimi si mwanasheria na sijui vifungu vya sheria lakini hilo kosa la kwanza silioni kama ni kosa... kwa mujibu wa imani ya kiislamu NI HARAMU KULA NGURUWE!!! Sasa kama kuna aliyekula nguruwe ajitakase tu... au labda alikuwa na njaa ya kufa akala kidogo kwa dharula? Naomba wajuvi mnipe ufafanuzi hapo sijaelewa labda kinazungumzwa kitu kingine
 
Lissu The Greatest

Lissu ana achwa ili page five ifanye kazi, anatumiwa kuigawa Chadema . Wanachama na Viongozi wamegawanyika. Kuna wanao taka Lissu ateuliwe kupeperusha bendera ya Chadema Uchaguzi Mkuu 2020 na kuna wengi hawataki.

Anaachiwa ili afanye kampeni ndani ya chama kwa ajili ya uteuzi wakati Uongozi wa Chadema ulitaka Mahakama iwasaidie kufanya kazi ambayo wao wanasita kuifanya na kuimalizia kwenye Mkutano Mkuu.

Utarudi hapa kuniambia. Usikimbie sababu wewe unaonekama Mahaba niuwe.
 
Nichukue fursa hii kumpongeza Tundu Antipas Lisu kwa hatua aliyochukua ya kujiweka katika karantini ya siku 14 baada ya kurejea nchini akitokea Ubelgiji.

Nawatakia Eid Mubarak.

Maendeleo hayana vyama!
 
  • Thanks
Reactions: bmk
mimi ni mshabiki wake ila kwa hili hapana
 
Sasa wale waliompokea na kutembea barabara za Dar kwa mwendo mrefu itakuwaje nao waende karantini na je chadema hawakujua kuwa mtu anayetoka nje ya nchi inampasa kwenda karantini au ilikuwa ni kuitega serikali. Dah hawa jamaa sometime siwaelewi kabisa
 
Back
Top Bottom