Kituo Kikubwa Cha Mikutano "MOUNT KILIMANJARO CONVENTION CENTER." Kujengwa Jijini Arusha

Kituo Kikubwa Cha Mikutano "MOUNT KILIMANJARO CONVENTION CENTER." Kujengwa Jijini Arusha

Mnashindwa kutoa ardhi tu ya stendi ya mabasi ijengwe kubwa ya kusasa ndio mtoe ardhi kubwa kwa mradi.mkubwa kama huoo?

Kaeni na ardhi.yenu jazeni tu makaburi

Waachieni mikoa mingine isiyo na ubahili na Ardhi yao kwenye uwekezaji
ardhi ishatolewa kitambo au hukumbuki swala la stand ya moshi mpya na kuibuka kwa chemchemi
 
Nadhani ingekuwa sahihi zaidi kama ungejengwa Dodoma
Hamna international community itaacha ku-lodge meeting in Arusha a well established destination for MICE waje Dodoma au hata Mwanza! Tutahitaji miaka 50 kufikia Status na aura ya Arusha city! Arusha is more strategic to host the MKICC!
 
Dah si wangplan kujenga Dodoma!
Nadhani serikali imeamua Hivyo, kwa kuwa kanda ya Kaskazini na hususani Mkoa wa Arusha ni kitovu cha utalii Tanzania. Hivyo itakuwa wageni wakishamaliza mikutano yao, wanaunganisha na kwenda kufanya utalii. Sasa hapo Idodomya hakuna kivutio chochote cha utalii.
 
Ameandika msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika mtandao wa Instagram

"Tunakwenda kujenga kituo kikubwa cha mikutano Jijini Arusha kitakachoitwa MOUNT KILIMANJARO CONVENTION CENTER."

"Kitakuwa na sifa zifuatazo;
1. Ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 3,000
2. Eneo la maonesho lenye kuchukua watu 10,000
3. Hoteli 2 za Nyota Tano zenye uwezo wa kulaza wageni 1,000
4. Majengo ya nyumba za kuishi (apartments)
5. Kumbi ndogo za mikutano
6. Majengo ya maduka (shopping malls)
7. Nyumba za kulaza watu mashuhuli wakiwemo Marais
8. Maeneo ya kupumzika (recreation areas)
9. Maeneo ya burudani
10. Bustani"

Kila la kheri @aicc_jnicc kwa mpango huu mkubwa."

Aicc mtaifunga ?
 
Arusha ipo AICC, huo uwekezaji ufanyike Dodoma.
Tusifanye kosa kama la kuweka viwanja vya mpira katika eneo moja.
AICC iboreshwe alaf kituo kipya kijengwe mkoa mwingine, Mfano Dodoma
Dodoma sii mji wa utalii uliza Dodoma wanaingia watalii wangapi kwa mwaka hakuna kitu ni vumbi tu na umaskini na omba2 ndo sifa ya Dodoma Ar ni tofauti Ar pazuri sana yaaani naturally!
 
Nchi ina idadi kubwa sana ya Vilaza, Tafuta Serikali hata moja Duniani inayo jenga Mahoteli na Majengo ya mikutano, nitafutie hata moja tu
Kwani Kuna ulazima wa kuwa kama hao wengine? Kama tunaweza ku manage na kushindana na private sector kuna tatizo gani? Huu ni wivu..

Sasa Kwa taarifa Yako tuu ni kwamba Tanzania Sasa ni ya 5 Kwa Africa Kwa Conference Tourism Toka namba 15.
 
Jambo gani jema? Serilali kujenha Mahoteli? Huu ni ujinga na wanafanya kwa.sababu wanajua Watanzania ni wajinga sana, Hii ni kazi ya Private Sector na sio Serikali,
Ujinga Kiaje? Kwani ukijenga harafu ukaweka uendeshaji wake Kwa kushirikiana na private sector Kuna shida gani? Harafu kujenga Kwenyewe sio lazima Serikali itoe pesa Bali inaweza Jenga via PPP.

Shida yenu hamna akili nzuri ila mnadhani mna akili 😁😁
 
Ameandika msemaji mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa katika mtandao wa Instagram

"Tunakwenda kujenga kituo kikubwa cha mikutano Jijini Arusha kitakachoitwa MOUNT KILIMANJARO CONVENTION CENTER."

"Kitakuwa na sifa zifuatazo;
1. Ukumbi wenye uwezo wa kuchukua watu 3,000
2. Eneo la maonesho lenye kuchukua watu 10,000
3. Hoteli 2 za Nyota Tano zenye uwezo wa kulaza wageni 1,000
4. Majengo ya nyumba za kuishi (apartments)
5. Kumbi ndogo za mikutano
6. Majengo ya maduka (shopping malls)
7. Nyumba za kulaza watu mashuhuli wakiwemo Marais
8. Maeneo ya kupumzika (recreation areas)
9. Maeneo ya burudani
10. Bustani"

Kila la kheri @aicc_jnicc kwa mpango huu mkubwa."

Nani anajenga hii na kwa bajeti kutoka wapi? Mbona stendi tuu ya mkoa Wa Arusha imeendekea kutia aibu na hakuna anayetoa neno?
 
Back
Top Bottom