SYLLOGIST!
JF-Expert Member
- Dec 28, 2007
- 8,189
- 7,853
Na mwenye masikio asikie.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Taasisi haijengwi na majengo au vitabu ni watu. Pole kama hulijui hilo. Na lazima wawe na kiongozi na kwa mfumo wa katiba yetu hilo ni jukumu la Rais pekee mpaka hapo tutakapo amua vinginevyo.Tunahitaji taasisi imara zaidi kuliko wote
Mkuu,
Hapa kidiplomasia, Kitwanga amemwambia Rais anafanya mambo hovyo hovyo au anakosea kosea katika mambo yake.
Mara nyingi sana watu wanatumia lugha ya kuwasema vibaya washauri wa Rais ili kumwambia Rais haupo sawa, unakosea.
Wataalamu mnaweza kunisahihisha.
Si Kweli,Sukuma Gang wanapita kipindi kigumu sana dadeq zao
Voicer:Huyaoni matatizo ya mama yupi?
Au mama yako mzazi?
Nchi ya watu milioni sitini,unataka watembelee unavyojisikia wewe?
Na tutajuaje kama anaowasema kitwanga ndio kina wewe?
Shat ap [emoji67]
View attachment 2527543
Samia ni dhaifu mno,she's misfit to the position!Rais anaweza kuonekana dhaifu lakini anapoamua kushughulikia watu kwa mamlaka yake huwa tunakuja humu jukwaani na kuanza kulialia tukisema rais huyu ni dikteta,
Hayati JPM aliamua kutokuwa dhaifu na mpaka miaka miwili akiwa kaburini bado wapo watu wanaoulalamikia uongozi wake.
SSH sio dhaifu kama tunavyodai, ameruhusu uongozi wake uheshimu demokrasia na amewapa watu uhuru wa kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu.
Ndio rais mpaka 2025 na anafanya mengi akitekeleza miradi karibu yote aliyoiacha JPM. Hahitaji kutumia sana media katika propaganda ndio aonekane rais mkakamavu.Samia ni dhaifu mno,she's misfit to the position!
Mwisho ni 2025? Hamsemi hadi 2030 tena? Kulikoni?!Ndio rais mpaka 2025 na anafanya mengi akitekeleza miradi karibu yote aliyoiacha JPM. Hahitaji kutumia sana media katika propaganda ndio aonekane rais mkakamavu.
Miaka ya binadamu duniani anaipanga Mungu.Mwisho ni 2025? Hamsemi hadi 2030 tena? Kulikoni?!
Niliiangalia intavyuu, alikuwa amelewa chakariKitwanga anasema kuna kundi ambalo limejipenyeza kwa rais na kila mahala linamshauri vibaya Rais.
==========
WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema kuna kundi linalomzunguka Rais Samia Suluhu Hassan ambalo limekuwa likiweka vigingi kwa watu, wakiwamo wataalamu, wanaotaka kushauri kuhusu mambo mema ya kuipeleka nchini pazuri zaidi.
Kitwanga amesema mbali na kuweka vigingi kwa watu wenye nia njema, kundi hilo limekuwa likiwaona tishio, hivyo kuwachafua, ili kulinda masilahi binafsi. Amemwomba Rais kuwa makini na kundi hilo.
Kitwanga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na kwamba ameona kuna umuhimu wa kumshauri Rais Samia kupitia vyombo vya habari.
Alisema kundi hilo limejipenyeza katika kila sekta zikiwamo taasisi za umma na kwamba lengo lake ni kuharibu nchi kwa maslahi binafsi.
Chanzo: Nipashe
WatajeTunawafahamu.
Kitwanga kawataja?Wataje
Kitwanga anasema kuna kundi ambalo limejipenyeza kwa rais na kila mahala linamshauri vibaya Rais.
==========
WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema kuna kundi linalomzunguka Rais Samia Suluhu Hassan ambalo limekuwa likiweka vigingi kwa watu, wakiwamo wataalamu, wanaotaka kushauri kuhusu mambo mema ya kuipeleka nchini pazuri zaidi.
Kitwanga amesema mbali na kuweka vigingi kwa watu wenye nia njema, kundi hilo limekuwa likiwaona tishio, hivyo kuwachafua, ili kulinda masilahi binafsi. Amemwomba Rais kuwa makini na kundi hilo.
Kitwanga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini na kwamba ameona kuna umuhimu wa kumshauri Rais Samia kupitia vyombo vya habari.
Alisema kundi hilo limejipenyeza katika kila sekta zikiwamo taasisi za umma na kwamba lengo lake ni kuharibu nchi kwa maslahi binafsi.
Chanzo: Nipashe
Ukimuuliza watu gani, anaweza dai tubadilishe Katiba tuweke Wazungu, kana kwamba wao ndio Taasisi.Taasisi haijengwi na majengo au vitabu ni watu. Pole kama hulijui hilo. Na lazima wawe na kiongozi na kwa mfumo wa katiba yetu hilo ni jukumu la Rais pekee mpaka hapo tutakapo amua vinginevyo.
Una umri gani?Hapana, si kweli, labda kwenu tu.
Upanga tulikuwa na duka la baba Taybal, kulikuwa na duka la wahindi nimewasahau jina Four Flats jeshini watoto wa Muhimbili Primary tulikuwa tunakwenda kununua Peramaziwa.
Uswahilini kulikuwa na maduka ya watu binafsi. Hayakuwa mengi kama sasa lakini yalikuwapo.
Mkuu hii habari imeandikwa na Shivji katika kitabu chake "Development As Rebellion: A Biography of Julis Nyerere" si habari ya vijiweni.
Hao ndio wamechoka. Wanaongea ni wajumbe tu.Kwamba Hadi yule Mzee asiye na wizara maalum naye anatoa ushauri mbaya au anashauri bt hasikizwi?
Maombi juu ya nchi, viongozi na KANISA ndo yatalitoa Taifa letu ktk mkwamo tuliopo.
Amen
Ahaa kumbe Mwanamvua hana uwezo wa kuhakiki...Yani rais hata kama kweli anashauriwa vibaya, akiukubali ushauri, kosa ni lake.
Rais anatakiwa kuwa na njia za kuhakiki ushauri anaopewa.
Nyerere alishauriwa na washauri wake ataifishe maduka yote, yani maduka yote mpaka ya Uswahilini yawe ya ushirika au chama.
Akamfuata Mzee mmoja anaitwa Songambele, Mzee wa Dar tu wa chama, yani hakuwa hata katika washauri rasmi wa rais. Lakini Nyerere alimfuata kama Mzee wa kitaa anayeyajua mambo ya kitaa.
Nyerere akamwambia Mzee Songambele, nimeshauriwa hivi na washauri wangu, kwamba tuyafanye maduka yote yawe ya umma, unaonaje?
Mzee Songambele akamwambia chonde chonde usifanye hivyo baba, tutaadhirika mtaani, wenyewe tunajua tunavyojistiri kwenye viduka vyetu hivi, usifanye hivyo. Hao washauri wako hawajui maisha ya mtaani.
Nyerere akautupa ushauri aliopewa na washauri wake wasomi, akaenda na maneno ya Mzee Songambele, Mzee wa Dar ambaye yuko connected kitaa.
Hapo utaona rais kajiwekea namna ya kuhakiki ushauri anaopewa, hakubali kila kitu anachoshauriwa.
Rais akikubali ushauri mbaya, kosa ni la rais, kwa sababu rais anatakiwa kuhakiki ushauri kabla ya kuukubali.