KKKT ni kanisa kubwa kuliko mtu, Kiburi kimemponza Mchungaji Kimaro

Yesu hakuwa na kipato binafsi pembeni.

Yohana Mbatizaji vilevile, alikula asali na nzige jangwani, lakini bado alipata wafuasi wengi.
Usimfananishe Bwana Yesu kwenye zamani zile na zamani hizi..

Yesu hakuwa na mke,
Hakuwa na watoto,
Hakulipa bili ya Umeme,
Hakulipa nauli ya Basi,
Hakutumia bundle la Internet.
Hakuwa na Bima ya Afya
Hakulipa Ada ya watoto wa shule

Sasa utumishi wa Leo hii ni tofauti sana na wa kipindi cha Yesu kwa maana Yoote hayo na zaidi unayahitaji kwa hiyo ukisema uishi kama Yesu alivyoishi enzi zake haiwezekani....

Tumia akili.
 
Naomba kujuzwa,kwa mujibu wa structure ya utawala ya KKKT,Mchungaji anawajibika kwa Askofu au kwa Katibu Mkuu wa Kanisa?
 
Katibu Mkuu ndiyo Muajiri mkuu.
Kwa maana hiyo yeye ndiyo mwenye mamlaka ya kumpangia sehemu ya kazi pia? Kama ni huvyo why sasa lawama za kuondolewa Mchungaji anapewa Malasusa? Au Katibu Mkuu anapokea maelekezo kutoka kwa Askofu?
 
IIa lazima tukubaliane kuwa Doyasisi ya mashariki na Pwani chini ya Mwalasusa ina matatizo mengi sana miaka yote!

'Saa ya ukombozi ni sasa': By Mch. Hananje



Utaratibu ukoje wa muda wa kuwa askofu?

Au ndio mpaka Yesu arudi ?

Afadhali mngeweka miaka 2-3 lakini miaka 5 mmmh!
 
Mtumishi akiwa na Karama au upako lazima aongozwe na hekima na siyo jeuri na kiburi cha kufanya na kusema atakavyo kwa kujiona yuko juu ya taratibu zilizowekwa. [emoji818][emoji817]
Taarifa za chini chini ni kwamba Kimaro alikuwa anajipanga kuchukua nafasi ya Malasusa ambae kapwaya kweli kweli.

Ili kumpunguza nguvu wakaamua kumkata pembe mapema akose sifa na nafasi ya kuendelea kukita mizizi.
 
Ubinafsi, jeuri na kipato binafsi ndivyo vinavyomsumbua Kimaro.
Anaitumia karama yake vibaya.
Akiona anazongwa, akawe Yohana mbatizaji nyikani, tutamsikia tu.
ila sikushangai maana hata huko kwenu ccm mkiambiwa ukweli mnaona kuwa ni matusi
 
Utamtiije Mungu kama hutii viongozi wako na utaratibu uliowekwa na kanisa? Hio kichwa acha kubebea kamasi tu!
 
Unaweza kutafuta kichaka Cha kujificha, lakini haihalalishi kiburi kama kweli kipo! Lazima amtii MUNGU na waajiri wake pia.
 
Kuna kiburi na kibri.
Kiburi ni wajinga wanafanya hivyo. Kibri kinafanywa na watu waelevu.
Kimaro amefanya Kibri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…