KKKT ni kanisa kubwa kuliko mtu, Kiburi kimemponza Mchungaji Kimaro

KKKT ni kanisa kubwa kuliko mtu, Kiburi kimemponza Mchungaji Kimaro

Inawezekana sasa haya makanisa yameanza kutumiwa na wachungaji kama vijiwe vya kutafuta umaarufu ili wajipatie wafuasi, siku wakitoka nje ya hapo wahame na wafuasi wao waende kwenye makanisa watakayoanzisha..

Waumini wanatumika bila kujua dhamira za ndani za hao wachungaji, kwasababu kama nia ya mchungaji ni kuihubiri injili, ujuaji hauwezi kupata nafasi mahala hapo, lakini kama mtu ana sababu zake zilizojificha, lazima awe mjuaji ili mwisho wa siku atimize malengo yake.
Na hilo ndilo lilivyo kwa huyu na yule wa Kimara na Mch. Richard H.
 
Waliogopa tu kuwa siku akisimama kugombeya U Askofu atawabwaga wote.
Hilo waliogopaje wakati wao ndio wasimamizi wa uchaguzi?? Wanaomchagua Askofu si huwa ni wachungaji wenyewe, tena kwa uwakilishi tu? Kwamba Kimaro ana ushawishi mkubwa kwa wachungaji wenzake, mbona sasa hatusikii wachungaji hao wakimtetea na kupinga uonevu?
 
Alionywa kwa kosa lipi?

Waliogopa tu kuwa siku akisimama kugombeya U Askofu atawabwaga wote.

Yupo huyo mkuu wa jimbo naamini ana lenga kuwa Askofu, anadhoofisha wengine nguvu.

Je mmesahau huyu mkuu wa jimbo kufikia hapo alifanya kitu gani?

Na hapa wanajiandaa kumdhoofisha pia Matsai
maaskofu hawachaguliwi na waumini
 
Mtumishi akiwa na Karama au upako lazima aongozwe na hekima na siyo jeuri na kiburi cha kufanya na kusema atakavyo kwa kujiona yuko juu ya taratibu zilizowekwa. [emoji818][emoji817]
Kaka nauliza tu

Hivi inawezekana kuwa Mganga wa Kienyeji(Mchawi) halaf bado ukawa Mkristo?
 
Lengo langu ni uelewe kwamba KKKT ni taasisi. Na kila taasisi inaendeshwa na taratibu zake ambazo imejiwekea. Ni simple tu kama Kimaro anaona taratibu za KKKT zinambana anauwezo wa kujitoa ili awe huru zaidi.
Concept ni kwamba amekiuka taratibu.
nimewai kuudhuria ibada pale kijitonyama Lutheran, mchungaji Kimaro alikuwa hafuati Liturgia ambay ndio inaongoza ibada, pamoja na mazuri mengi aliyofanya haimaanishi kuwa anapokosea asikosolewe na yey ni binadamu kuna mahali anakosea.
Hekima imewaangusha wengi, ana mazuri mengi aliyofanya na pia anapokosea anaambiwa vile vile

Ukikazania kusema AMEKIUKA TARATIBU bila kuzitaja na wewe huna tofauti na LOKOLE
 
Ukikazania kusema AMEKIUKA TARATIBU bila kuzitaja na wewe huna tofauti na LOKOLE
Nadhani hujui kusoma nimetolea mfano hapo. Huwa hafuati Liturgia, KKKT ibada huwa inaongozwa kwa kufuata Liturgia na sio upeo au ufaham wa mtu.
 
... ingawa mara nyingi viongozi wasio na maono wala karama yoyote wanakuwa na wivu sana ingawa sikatai ukweli kwamba baadhi ya wenye karama nao sometimes wanakuwa na viburi.
huyu jamaa clip.zake zimesambaa akitoa maneno ya kejeli
 
This is too low for Mamndenyi. Unaombea utengano? Serious? Kisa tu Kimaro kuondolewa Kijitonyama? Inamaana KKKT nzima ni Kimaro tu anayefaa kuwa mchungaji wa Kijitonyama? Mbona wataka kudhalilisha kanisa la KKKT kiasi hiki. Kwani huko atakapopelekwa hakuna watu wanohitaji huduma yake kama ninyi? Tusemeje basi? Ninyi ni wabinafsi sio? Ningekuwa Askofu wa KKKT ningepiga marufuku mahubiri kupitia accounts binafsi za youtube na digital platforms. Wachungaji wengi huzitumia kujitengenezea umaarufu binafsi kuliko taasisi wanayoisimamia, na hivyo kusababisha migogoro isiyo na tija.

Kumbe ni WIVU tu
 
Usimfananishe Bwana Yesu kwenye zamani zile na zamani hizi..

Yesu hakuwa na mke,
Hakuwa na watoto,
Hakulipa bili ya Umeme,
Hakulipa nauli ya Basi,
Hakutumia bundle la Internet.
Hakuwa na Bima ya Afya
Hakulipa Ada ya watoto wa shule

Sasa utumishi wa Leo hii ni tofauti sana na wa kipindi cha Yesu kwa maana Yoote hayo na zaidi unayahitaji kwa hiyo ukisema uishi kama Yesu alivyoishi enzi zake haiwezekani....

Tumia akili.
Na wachungaji wengine wako vipi, maana nayealamikiwa na kuchukuliwa hatua ni huyu Kimaro tu.
Msijaribu kuficha uchu wa pesa na utumiaji vibaya wa madaraka kikanisa, shutuma ambazo ndiyo analaumiwa huyu Kimaro.
 
Usitumie kichaka cha wivu kuvuruga taratibu za kanisa. Na hii ndio dhana ambayo wafuasi wake mnataka kuijenga. Sijui mlitaka mkae naye milele hapo Kijitonyama? Haikubaliki na haitakubalika kamwe.

Kama huweki utaratibu uliovunjwa maana yake huna hoja ACHA WIVU WA KIJINGA
 
Makanisa na Dini zote ni utapeli...

Mungu Hana dini..

Hao walioweka Sheria makanisani waliweka kwa maslahi yao binafsi wala si maagizo ya Mungu...

Religion is a crowd control...

Mwenye povu ruksa...[emoji1][emoji1]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Kama huweki utaratibu uliovunjwa maana yake huna hoja ACHA WIVU WA KIJINGA
Wewe ni nani mpaka uletewe taarifa hiyo? Hujui hata taasisi zinavyofanya kazi hivyo kaa kimya. Umeumia sana mshauri mtu wako aanzishe kanisa lake maana maamuzi yameshafanyika.
 
Back
Top Bottom