Klabu Yanga yafungiwa kusajili na Shirikisho la soka Duniani (FIFA)

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Klabu ya Young Africans iliyoko Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Pamoja na masuala mengine, Young Africans haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

IMG_0706.jpeg

====
Pia soma

1.
Yanga yafungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana
 
Mkomee Utopolo
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.

2. Mbumbumbu SC.

3. Mipang'ang'a SC.

4. Malalamiko SC.

5. Makelele SC.

6. Madunduka SC.

7. Mikia SC.

8. Mazumbukuku SC.

9. Manyaunyau (mapaka) SC.

10. Manyang'au SC.

11. Miso Misondo SC.

12. Mwakarobo SC.

13. Mazombi SC.

14. Kolokhamsa SC.

15. Kolowizards SC.

16. Kinyume nyume SC.

17. Zuwena SC.

18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.

19. Bahasha SC.

20. Ngada SC.

21. Kufa Kiume SC.
JamiiForums1683832807.jpg
JamiiForums-312072181.jpg
 
Barua inaonyesha wamefungiwa kufanya Usajili wa wachezaji wa ndani...tuendelee kula shushuu wakiwa wanasajili majembe ya nje...
 
Back
Top Bottom