Klabu Yanga yafungiwa kusajili na Shirikisho la soka Duniani (FIFA)
Klabu ya Young Africans iliyoko Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Pamoja na masuala mengine, Young Africans haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

====
Pia soma

1.
Yanga yafungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana
Yanga ni lidude fulani hivi litishalo!
Hata wasiposajili kwa miaka 2 ijayo hakuna shida ingawa najua suala lao litakwisha mara moja!
 
Ni
We Jiandae tu kwa kipigo hapo tarehe 20 hizi propaganda zako hazitakusaidia
Linatengenezwa zengwe la Aprili 20 hilo. Kipigo kipo pale pale kwa Makolo. Halafu kesho Aprili 13 Uwanja wa Kilumba lazima kolo ale za kutosha kutoka kwa vijana wetu pendwa Yanga B the ...... Black Stars??
 
Barua ya TFF inaonyesha ni namna gani TFF inamlinda Yanga sana.

Huyo mchezaji ambaye hana kibali cha kucheza imekuaje akacheza ligi yetu kwa kibali kipi maana yake Yanga anatakiwa akatwe point kwenye mechi zote huyo mchezaji alizocheza.

TFF ina uyanga watu hamuoni????

Nimewaza tu kama hiyo kitu ina ukweli basi tuendelee kuchimba hadi ijulikane
 
Unayo nafasi ya kutaka rufaa
 
Barua inaonyesha wamefungiwa kufanya Usajili wa wachezaji wa ndani...tuendelee kula shushuu wakiwa wanasajili majembe ya nje...
Fifa wamezuia nje na ndani, tff wamezuia ndani tu
 
Ahmed Ally amewaambia makolo waanze kushangilia kwamba ligi wanaanzs kubeba baada ta Yanga kufungiwa!! Makolo bwana!!
 
Barua ya TFF inaonyesha ni namna gani TFF inamlinda Yanga sana.

Huyo mchezaji ambaye hana kibali cha kucheza imekuaje akacheza ligi yetu kwa kibali kipi maana yake Yanga anatakiwa akatwe point kwenye mechi zote huyo mchezaji alizocheza.

TFF ina uyanga watu hamuoni????

Nimewaza tu kama hiyo kitu ina ukweli basi tuendelee kuchimba hadi ijulikane
Nahisi huyo mchezaji atakuwa kibabage na mwigulu ndiye alimhamisha.
Hata Morison alisema alipokuja yanga mechi ya kwanza akicheza wakati usajili haujafanyika na alisajiliwa baada ya dirisha kufungwa.
 
Back
Top Bottom