Mwarami Said Mohamed Sultan mchezaji wa zamani wa Taifa Stars, Simba SC, Clube Ferroviário de Maputo ya Mozambique pia Ferroviario za Pemba na Nampula zote za Mozambique.
AT
THURSDAY, NOVEMBER 26, 2009

Huyu ndiye kipa mpya wa timu ya taifa ya bara a.k.a Kilimanjaro Stars Mohamed Mwalami anayechezea klabu ya Ferroviaro ya Maputo, Msumbiji. Anachukua nafasi ya kipa Shaaban Dihile ambaye ametemwa.
Kipa mwingine ni Shaaban Kado wa Mtibwa Sugar. Kwa habari kamili ya kikosi kinachoondoka asubuhi hii kuelekea Kenya kwenye michuano ya Chalenji inayoanza Jumamosi 28, 2009.
18 Jul 2014
KIPA SIMBA SC ABWAGA MANYANGA
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba, Mwarami Mohammed ‘Shilton’ amestaafu soka na sasa anataka kuwa kocha.
Mwarami mwenye umri wa miaka 35, amesema kwamba ameona bora kutungika glavu zake kwa heshima kwa sababu umri umeenda.
“Nimecheza kwa muda mrefu, tangu mwaka 1997 nacheza Ligi Kuu, ni miaka mingi na ninaona mwili umechoka. Ni wakati wa kupumzika kwa heshima sasa,”amesema.
 |
| Mwarami Mohamed amestaafu soka |
Mwarami amestaafu akiwa anachezea Ferroviario de Maputo ya Msumbiji ambayo alijiunga nayo baada ya kuchezea Ferroviario za Pemba na Nampula.
Kabla ya kwenda Msumbiji, nchini Tanzania, Mwarami alichezea timu za Coastal Union ya Tanga, Simba SC ya Dar es Slaam, Kariakoo United ya Lindi na Reli Morogoro.
“Nataka kuwa kocha, nimeanza kuafuatilia vyuo vya kwenda kusomea ukocha, lakini kwanza nitapata kozi za awali hapa hapa nchini kwa kuanzia,”alisema