Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu hawa jamaa sijui wanafanya nini humu jukwaani. Hawakustahili kuwa hukuHii ni JF..
Tanzania hii mtu ulipwe 6m na bado useme una maisha magumu..huu si ni uongo kabisa??
Ndie kamueka ndani Sanchoka na kumtuliza ..Kwa Cambiasso long time nilikuwa binafsi namshuku. Sema fresh, mwana alikuwa ana madharau mshamba huyo. Ayaoge sasa msala huo lazima abonye kizenji.
Namaliza kazi iliyompeleka ..undercoverKwa lile Bata la Wachezaji wa Cambiaso Soccer Academy, Hadhi yao na Mengineyo sishangai leo kusikia kuwa kumbe Mmiliki ni Drug Baron na anashirikiana na Watu wengine.
Shikamoo sana Kocha wa sasa wa Kagera Sugar FC Mecky Mexime ( ambaye ulikuwa Kocha wa Cambiaso Soccer Academy) kwa kuwa Mjanja, Kushtuka, kutoa Ushirikiano na kusepa Mapema kabka ya Msala Kukukuta.
Ana andaa neno Kwa ajili ya Wana wa kondooMasanja yupo wapi kwa sasa
Yuko Kwa upande wa msogani, majuzi nae alikuwa madina akifanya ibadaLile ripokaji kitenge nalo litaingia tu kwenye kumi na nane labda km yupo upande wa wakubwa
Mkuu Sancho hana uchafu kama huu. Heshima kwa huyo Nicole ila Sanchoka habari nyingine mkuu
Mkuu heshima yakoBdo Eddo Kumwembe, Siku zake zinahesabika Kale Kabinti Kaandishi ka Habari Kwa Mwananchi Some1 Kulangwa amekula mvua ya miaka 40 jera huko Italy
How?
Watuhumiwa tisa akiwemo Kocha wa Makipa wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam Muharami Said Sultan wanashikiliwa na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya kilo 34 aina ya heroin.
Akizungumza leo Jijini Dar Es Salaam Novemba 15, 2022 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya operesheni maeneo mbalimbali nchini kuanzia Oktoba hadi Novemba mwaka huu na kufanikiwa kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Akifafanua zaidi Kamishina Jenerala Kusaya amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni Kocha wa Makipa wa Simba Muharam Said Sultani(40) mkazi wa Kigamboni na kufafanua kwamba Muharam amewahi pia kuichezea timu ya Simba.
Wengine ni Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kituo cha Soka cha Cambiasso Sports Academy kilichopo Tuangoma wilayani Kigamboni Alhaj Kambi Zeber Seif maarufu kwa jina la Kambiasso au Alhaj Kambi mbali ya kumiliki kituo hicho cha soka ana miliki kampuni ya Safia Group of Companies inayomiliki magari ya kusafirisha abiria (daladala) kutoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Pwani.
Pia Mamlaka hiyo inamshikilia Said Abeid Matwiko ambaye anaishi Magole A Kivule na kazi yake ni fundi selemala,mwingine ni Maulid Mohamed Mzungu maarufu kwa jina la Mbonde (54) mkazi wa Kisevule ambaye kazi yake ni mkulima.
Amewataja watuhumiwa wengine ni John Andrew John (40) mkazi wa Magore-Kitunda ambaye ni mfanyabiashara na amekuwa na jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kituo cha Soka Kambiasso, Pia wanamshikilia Seleman Matola Said(24) mkazi wa Temeke –Wailes Matola ni mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Alhaj Kambi.
Mwingine ni Hussein Mohamed Pazi(41) mkazi wa Kibugumo wilayani Kigamboni ambaye ni mfanyabiashara na mtuhumiwa wa tisa ni Ramadhan Rashid Chalamila(27)ambaye ni mfanyabiashara. “Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
You gonna be rich ask me
View attachment 2417734
Hiyo sio mara ya Kwanza kukamatwa na akaachiwa hii ndio AfricaHuu ni ujasiri wa Hali ya juu kwa mamlaka zilizohusika na uchunguzi na ukamataji wa mapapa haya
. Tanzania wazalendo bado wapo wengi. Wajitahidi tuu ushahidi uwe watertight ili conviction ipatikane ijapokuwa ni ngumu Sana kwa kesi za aina hii.
Watanzania tunaoishi kinafiki Sana na dini zetu. Machoni mwa watu tunajionyesha ni wema Sana, watoa misaada kwenye jamii, wajenga nyumba za ibada ,hata mtu akiisema vibaya dini ambayo upo kwa jina tuu ila matendo upo tofautibkabisa unaweza kumtoa roho.
Najua ni jukumu la mahakama pekee kuthibitisha tuhuma hizi na haturuhusiwi kumhikumu hata kwa maneno lakini kitendo Cha mtu mwenye daraja la alhaji ambaye ameshasafiri kwenda kumpigia sheitwani na mawe kutuhumiwa tu au kutajwa linafikirisha. Tuwaombee vijana wetu wanaofanywa mazezete na watu hawa wasiojalinkesho yao
Hii biashara inafanywa kwa siri siri na wajanja wanaopenda kudanganya kwa kufungua container za biashara wakijiita wafanyabiashara. Kumbe wauza unga. Kuna dada maarufu mpaka leo amekwama na mmewe. Alikuwa ndio mwalimu wetu wa kuweka elfu 10 kwa siku kwenye masanduku ya bati, ili tule XmassKuna yule mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi some Kulangwa if am not mistaken jina lake nae alikamatwa Huko Italy mpaka Leo hajatoka.
Aliyeshukiwa na ngozi ndiye mwizi 🥱Unga alikua anauza Manji kipindi anailea Yanga mbona hamkuja juu
Nimechelewa, kumbe ilipostiwa tayar..Amekutwa kwa mara nyingine tena?
Africa hii ukiwa tajiri ufungwi utalipa faini tu ..kufungwa ulaya uko au asia lakini siyo uku..DPP anaamka asubuhi anakuta kwenye account yake amewekewa bilion 5 ikisindikizwa na txt utakunywa supu mzee kwa hii asubuhi[emoji3][emoji3] kesi amna apo afungwi mtuKukamatwa ruksaa, kufungwa bongo kwa kosa la sembe sahau, utasikia kumbe ilikuwa ni unga wa lishe!!
Kitambo tu wewe Kinye Fc tulia,Nimechelewa, kumbe ilipostiwa tayar..
Ucjali Kolongada