Kocha wa Makipa Simba SC na wengine 8 wakamatwa na Dawa za Kulevya
Wanatusumbua sana wanajiona wameyapatia maisha wamenasa kwenye gundi
IMG_20221029_082727.jpg

By byeee go to hell
 
Kwa lile Bata la Wachezaji wa Cambiaso Soccer Academy, Hadhi yao na Mengineyo sishangai leo kusikia kuwa kumbe Mmiliki ni Drug Baron na anashirikiana na Watu wengine.

Shikamoo sana Kocha wa sasa wa Kagera Sugar FC Mecky Mexime ( ambaye ulikuwa Kocha wa Cambiaso Soccer Academy) kwa kuwa Mjanja, Kushtuka, kutoa Ushirikiano na kusepa Mapema kabka ya Msala Kukukuta.
Namaliza kazi iliyompeleka ..undercover
 
15 May 2022
Cambiasso Sports Management na namna inavyohakikisha vijana wengi wanafikia ndoto zao kisoka

 



Watuhumiwa tisa akiwemo Kocha wa Makipa wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam Muharami Said Sultan wanashikiliwa na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya kilo 34 aina ya heroin.

Akizungumza leo Jijini Dar Es Salaam Novemba 15, 2022 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya operesheni maeneo mbalimbali nchini kuanzia Oktoba hadi Novemba mwaka huu na kufanikiwa kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akifafanua zaidi Kamishina Jenerala Kusaya amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni Kocha wa Makipa wa Simba Muharam Said Sultani(40) mkazi wa Kigamboni na kufafanua kwamba Muharam amewahi pia kuichezea timu ya Simba.

Wengine ni Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kituo cha Soka cha Cambiasso Sports Academy kilichopo Tuangoma wilayani Kigamboni Alhaj Kambi Zeber Seif maarufu kwa jina la Kambiasso au Alhaj Kambi mbali ya kumiliki kituo hicho cha soka ana miliki kampuni ya Safia Group of Companies inayomiliki magari ya kusafirisha abiria (daladala) kutoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Pwani.

Pia Mamlaka hiyo inamshikilia Said Abeid Matwiko ambaye anaishi Magole A Kivule na kazi yake ni fundi selemala,mwingine ni Maulid Mohamed Mzungu maarufu kwa jina la Mbonde (54) mkazi wa Kisevule ambaye kazi yake ni mkulima.

Amewataja watuhumiwa wengine ni John Andrew John (40) mkazi wa Magore-Kitunda ambaye ni mfanyabiashara na amekuwa na jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kituo cha Soka Kambiasso, Pia wanamshikilia Seleman Matola Said(24) mkazi wa Temeke –Wailes Matola ni mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Alhaj Kambi.

Mwingine ni Hussein Mohamed Pazi(41) mkazi wa Kibugumo wilayani Kigamboni ambaye ni mfanyabiashara na mtuhumiwa wa tisa ni Ramadhan Rashid Chalamila(27)ambaye ni mfanyabiashara. “Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

You gonna be rich ask me
View attachment 2417734
How?
 
Huu ni ujasiri wa Hali ya juu kwa mamlaka zilizohusika na uchunguzi na ukamataji wa mapapa haya
. Tanzania wazalendo bado wapo wengi. Wajitahidi tuu ushahidi uwe watertight ili conviction ipatikane ijapokuwa ni ngumu Sana kwa kesi za aina hii.

Watanzania tunaoishi kinafiki Sana na dini zetu. Machoni mwa watu tunajionyesha ni wema Sana, watoa misaada kwenye jamii, wajenga nyumba za ibada ,hata mtu akiisema vibaya dini ambayo upo kwa jina tuu ila matendo upo tofautibkabisa unaweza kumtoa roho.

Najua ni jukumu la mahakama pekee kuthibitisha tuhuma hizi na haturuhusiwi kumhikumu hata kwa maneno lakini kitendo Cha mtu mwenye daraja la alhaji ambaye ameshasafiri kwenda kumpigia sheitwani na mawe kutuhumiwa tu au kutajwa linafikirisha. Tuwaombee vijana wetu wanaofanywa mazezete na watu hawa wasiojalinkesho yao
Hiyo sio mara ya Kwanza kukamatwa na akaachiwa hii ndio Africa



Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kuna yule mwandishi wa Habari wa Gazeti la Mwananchi some Kulangwa if am not mistaken jina lake nae alikamatwa Huko Italy mpaka Leo hajatoka.
Hii biashara inafanywa kwa siri siri na wajanja wanaopenda kudanganya kwa kufungua container za biashara wakijiita wafanyabiashara. Kumbe wauza unga. Kuna dada maarufu mpaka leo amekwama na mmewe. Alikuwa ndio mwalimu wetu wa kuweka elfu 10 kwa siku kwenye masanduku ya bati, ili tule Xmass
 

318EF2D4-B3D5-4617-9C33-40FD960B1F6F.jpeg


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imewakamata watuhumiwa 9 wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin kg 34.89 ambapo miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Muharami Sultan ambaye ni kocha wa magolikipa wa timu ya Simba na ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo pamoja


Muharami Sultan, Kocha wa magolikipa wa timu ya Simba, aliyekutwa na dawa za kulevya na Kambi Zuber Seif maarufu kama Cambiasso.
Mtuhumiwa mwinginie ni Suleiman Matola Said (24) ambaye ni mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Kambi Zuberi Seif.


Hayo yameelezwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Kamishna Gerald Kusaya, ambapo watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni iliyofanyika kuanzia mwezi Oktoba 2022, hadi mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.

NB:
Nilikuwa najiuliza Safari nyingi pre season na Post Seasons Kunani?

Time has spoken!
 
Kukamatwa ruksaa, kufungwa bongo kwa kosa la sembe sahau, utasikia kumbe ilikuwa ni unga wa lishe!!
Africa hii ukiwa tajiri ufungwi utalipa faini tu ..kufungwa ulaya uko au asia lakini siyo uku..DPP anaamka asubuhi anakuta kwenye account yake amewekewa bilion 5 ikisindikizwa na txt utakunywa supu mzee kwa hii asubuhi[emoji3][emoji3] kesi amna apo afungwi mtu
 
Back
Top Bottom