Hebu wataje wafanyabiashara wakubwa watano wa kitanzania wenye fedha safi na halali. 😂😂. We taja tu. Uzuri humu jf wapo watu wazima wenye mafaili mengi ya watu 😂😂😂 hebu wataje watano tu 😂
Wa kutaja ni wewe unaesema wana makando kando na sio mimi mkuu.

Wote ambao serikali haijawatia mkononi basi biashara zao ni halali, huu unazi wa kuendekeza kua ili uwe tajiri lazima ufanye biashara haramu sijui mmeutoa wapi.

Hiyo ni mentality ya kivivu, kutaka shortcut. Na hii sio kwa hawa matajiri wakubwa tu hata wale wanaojiweza kitaa mnawananga kua ni wachawi, majambazi nk.
Acha uvivu mzee, tafuta utajiri.
 
Kwa kweli jamaa kafaidi ndio raha yenyewe hiyo mwanawane. Ate hela ule warembo maana warembo wenyewe hawan upendo wabachotaka ni hela tuu
 
Naomba unisamehe sana, tajiri. Nimekosa sana mkuu 🙏
 
Na El Chapo aliwahonga kweli hadi rais wa nchi [emoji28][emoji28][emoji28]
Sasa mwanawane shipment moja kama hiyo tayari ni billion 24 nashindwaje kuhonga rais.

Wee jamaa ana jeshi lake kabisa na vifaa vya kivita kabisa, military grade amunition unashindana nae vipi.
Mie bwana nasema tuu wacha vijana wapambane kama mtu anaona anaweza tokea huko wacha afanye tuu maana hawa tunaotegemea kufight hiyo vita wenyewe wanaendesha hiyo biashara
 
Meki alikuwa anakula million kumi kwa mwezi ajabu sana
 



Watuhumiwa tisa akiwemo Kocha wa Makipa wa Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam Muharami Said Sultan wanashikiliwa na Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya kilo 34 aina ya heroin.

Akizungumza leo Jijini Dar Es Salaam Novemba 15, 2022 Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Gerald Kusaya amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya operesheni maeneo mbalimbali nchini kuanzia Oktoba hadi Novemba mwaka huu na kufanikiwa kukamata watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Akifafanua zaidi Kamishina Jenerala Kusaya amewataja wanaoshikiliwa kwa tuhuma hizo ni Kocha wa Makipa wa Simba Muharam Said Sultani(40) mkazi wa Kigamboni na kufafanua kwamba Muharam amewahi pia kuichezea timu ya Simba.

Wengine ni Mfanyabiashara na Mmiliki wa Kituo cha Soka cha Cambiasso Sports Academy kilichopo Tuangoma wilayani Kigamboni Alhaj Kambi Zeber Seif maarufu kwa jina la Kambiasso au Alhaj Kambi mbali ya kumiliki kituo hicho cha soka ana miliki kampuni ya Safia Group of Companies inayomiliki magari ya kusafirisha abiria (daladala) kutoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Pwani.

Pia Mamlaka hiyo inamshikilia Said Abeid Matwiko ambaye anaishi Magole A Kivule na kazi yake ni fundi selemala,mwingine ni Maulid Mohamed Mzungu maarufu kwa jina la Mbonde (54) mkazi wa Kisevule ambaye kazi yake ni mkulima.

Amewataja watuhumiwa wengine ni John Andrew John (40) mkazi wa Magore-Kitunda ambaye ni mfanyabiashara na amekuwa na jukumu la kutafuta vijana wenye vipaji na kuwapeleka kituo cha Soka Kambiasso, Pia wanamshikilia Seleman Matola Said(24) mkazi wa Temeke –Wailes Matola ni mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Alhaj Kambi.

Mwingine ni Hussein Mohamed Pazi(41) mkazi wa Kibugumo wilayani Kigamboni ambaye ni mfanyabiashara na mtuhumiwa wa tisa ni Ramadhan Rashid Chalamila(27)ambaye ni mfanyabiashara. “Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.

You gonna be rich ask me
 

15 November 2022
TAARIFA YA SIMBA SC : MWARAMI MOHAMED SIYO MWAJIRIA WA SIMBA SC

 
Jidanganye Mo ni tapeli mzoefu toka enzi ya ubinafsishaji. Zile mali ni umafia wa Baba yake Gulamabbas na mjomba wake Azim. Tafuta wazee wa zamani wakupe mkanda mzima wa umafia wa familia ya akina dewji [emoji23][emoji23][emoji23]
Baba yako alikuwa wapi muda huo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…