Kosa la Rais Samia ambalo watanzania wengi hawalitaki ni hili

Watanzania tupo sahihi, waliowengi anaowaita wameendelea wengi wao ni hela za rushwa na kukwepa kodi.

Hilo lipo wazi, unamkuta afisa manunuzi local gvt huko ana ukwasi hatari, DT, DED, injinia kutaja wachache. Nenda kwenye kwenye taasisi sasa TRA, tanroads, ewura.

Njoo kwa wanasiasa sasa huko ndo unazimia kabisa, kuna watu walituambia vijisenti hela ya mboga. Ni lugha za dharau kutokana na upigaji ukiokithiri.

Kwa nini wanaiba?
Wananchi wamekubaliana na wizi huo? Kama hapana je ni Hapana midomoni au moyoni?
Kwa nini hawachukua hatua kukabiliana na viongozi wa Aina hiyo?
 
sijawahi kukupinga..ila leo nitakupinga..kuhusu ishu ya usawa, kihulisia hatuwezi kuwa sawa hasahasa kwenye ishu ya uchumi mpaka yesu anarudi mfano juzi tu hapa kwenye nyumba ya ibada nilikutana na jamaa mmoja amenililia sana shida zake nikamuonea huruma nikamuambia twende kwangu ukawe hata houseboy, ajabu jamaa akiishafanya kazi ndogo ndogo akapata zake ugali mkubwa anapumzika mpaka kesho😃😃😃😃 hivi unategemea mtu kama huyu awe sawa na mimi??

Mkuu sijasema kuwa Watu ni Sawa.
Naungana na maelezo yako
 
Tatizo upigaji kwa wachache umeongezeka, huku maisha ya wengi yakiendelea kudidimia. Katika hili, ajiandae tu kusikia kelele kutoka kila kona ya nchi.
Mkafanye kazi kwa bidii jamani magufuli mlisema vyuma vimekaza huyu tena mnalialia yani watanzania wanapenda vya bure.
 
sijawahi kukupinga..ila leo nitakupinga..kuhusu ishu ya usawa, kihulisia hatuwezi kuwa sawa hasahasa kwenye ishu ya uchumi mpaka yesu anarudi mfano juzi tu hapa kwenye nyumba ya ibada nilikutana na jamaa mmoja amenililia sana shida zake nikamuonea huruma nikamuambia twende kwangu ukawe hata houseboy, ajabu jamaa akiishafanya kazi ndogo ndogo akapata zake ugali mkubwa anapumzika mpaka kesho😃😃😃😃 hivi unategemea mtu kama huyu awe sawa na mimi??

Mkuu sijasema kuwa Watu ni Sawa.
Naungana na maelezo yako
Kwanini wewe ulazimishe fasihi yako ndio maana ya kauli Rais Samia alikusudia?, hopeless kabisa

Unajua maana ya kulazimisha Mkuu?

Mimi nimeandika Maoni yangu, wewe umeandika yako. Sijaona mahali popote nilipokulazimisha au ulipo kulazimisha. Mbona unanipa jukumu ambalo sijafanya?
 
Hopeless thread,unatetea upumbavu wa kauli ya kiongozi mkuu?,rohoni kwa mtu ni mbali yeye ambaye madhara ya hii kauli kaisikia toka kwa jamii atoke hadharani kuitolea maelezo,sio wewe kapuku waheed

😀😀
Sasa unakasirika nini sheikhe?

Mimi nimeelezea vile ninavyomuelewa Samia, Kwa hiyo nikiwa kapuku ndio nisimuelezee?

Haya Tajiri WA mafenesi, nimekuachia wewe umuelezee.
 
Shetani anachukiwa yeye au Matendo yake?

Matendo ya MTU ndio MTU Mwenyewe na hata adhabu hupewa MTU na sio Yale aliyoyatenda.

Kuhusu Katiba mpya, sina uhakika. Ila kama wangefanya amendment hasa kipengele cha mamlaka ya Rais ningepongeza Sana.
Yule ni binadamu kama sisi wala si shetani. Matendo yake ndio hukumu yake kwa raia.

🤣 Kubadilisha kipengele cha mamlaka yake ni sawa na yeye kujipeleka kwenye deathrow. Hilo ni gumu sidhani kama ataweza.
 
Kama unadhani kumiliki mali nyingi ni kazi rahisi basi inaonekana na wewe utakuwa maskini tu.

There is always behind bussness nyuma ya utajiri Mkubwa.

Sio utajiri wa kuuza duka na kuuza Nyanya kariakoo

Tatizo la watanzania na Wanawake wengi hasa Afrika ni kufanya imagination ya vile wanavyofikiri na kuwawekea Watu wengine hizo imagination zao kwenye fikra za wengine.

Ati kama ninadhani, ninafikiri. Hayo mawazo yangu umeyajuaje? Au ndio hizo imagination zako juu ya fikra zangu?
 
Yule ni binadamu kama sisi wala si shetani. Matendo yake ndio hukumu yake kwa raia.

🤣 Kubadilisha kipengele cha mamlaka yake ni sawa na yeye kujipeleka kwenye deathrow. Hilo ni gumu sidhani kama ataweza.

Binadamu akifanya mambo ya kishetani huitwa shetani tuu. Shetani ni Cheo, Sifa, MTU yeyote anaweza kuitwa.

Mimi nataka hapo kwenye mamlaka ya Rais ndio pafanyiwe kazi. Huko kwengine wapaaache kama palivyo. Uone Hii nchi kama haiendi.

Katiba ikiruhusu Rais kushtakiwa kama Watu wengine automatically nguvu ya Mahakama na Bunge itakuwepo.
 
🤣 Hahahah ngoja tuone fupa lililomshinda fisi kama litatafunika awamu hii
 
Habari Wakuu!

Kwanza ijue nchi yako, waelewe Watu wako. Ifahamu jamii yako.

Sisi ni jamii ambayo mtu ukifanikiwa utaitwa ni Freemasonry,
Tupo kwenye jamii ambayo ukiwa na utajiri unaitwa Fisadi, Jizi au muuza madawa ya kulevya.
Tupo kwenye jamii ambayo ukimiliki vimiradi kadhaa au biashara za hapa na pale unaitwa unatumia Uchawi wa ngende. Ielewe jamii yako na watu wake.

Fanya vyovyote utakavyofanya, TOA jasho lako utakalotoa lakini elewa kuwa siku utakayofanikiwa watanzania wengi watakuweka kwenye mojawapo ya makundi hayo hapo juu.

Kwa kweli Taikon Master tangu nimezaliwa mpaka umri nilionao sijawahi kumuona Tajiri au mtu aliyefanikiwa hapa nchini ambaye Watu wanasema amepata Pesa kihalali. Hiyo sijawahi kusikia. Itakuwa mara yangu ya Kwanza na ambayo nitaiandika kwenye kumbukumbu zangu na pengine kuandika kitabu cha huyo mtu ambaye Watu watamsema amepata Mafanikio yake Kwa halali.

Leo sitaki kuwasumbua Sana,
Mama Samia kosa alilofanya ni Kutumia Ile Kanuni ya kila MTU ale urefu wa kamba yake. Kauli ambayo watanzania hawatakuja kuitaka Kwa sababu watanzania ni jamii ya kijamaa. Watu ambao wanataka kula kamba Kwa kushirikiana.

Watanzania wanavutiwa zaidi na viongozi ambao wanataka kuwafanya Watu wote kuwa Sawa ndani ya jamii. Yaani matajiri na Maskini wote wawe Sawa. Wavivu na wachapakazi wawe Sawa. Wenye bahati na wasio na bahati wawe sawasawa. Hilo Kwa Samia halipo, hiyo sio falsafa yake. Hapo ndipo anapopishana na upendo wa watanzania.

Samia anatumia Ile falsafa ya Yesu isemayo kila MTU abebe msalaba wake. Kila mtu ajikune pale mkono wake unapofikia.

Samia hawezi kumshusha wa juu ili afanane nawa Chini. Hiyo sio falsafa yake. WA Chini akitaka kwenda juu apambane kivyake vyake. Wakati vivyohivyo.

Wenye bahati wabaki wenye bahati Yao mpaka bahati Yao itakapokwisha. Wasio na bahati waendelee kuhenyeka mpaka bahati Yao utakapokuja yenyewe au Kwa wao kuitafuta.

Watanzania kama jamii hainaga Tabia ya ku- appreciate uwezo wa waliofanikiwa. Hata hapo kwenu wewe ukifanikiwa bado watakuona kama aidha umebahatisha, huna uwezo, au umetumia ndumba, au umebebwa bebwa.

Samia hiyo falsafa yake hawezi kutoboa kwenye mioyo ya Watanzania. Na sidhani kama yeye ni wale Watu wanaotafuta kupendwa au kulazimisha kukubalika.

Eeeh! Acha nipumzike tuu.

Ijumaa Kareem
Mitanzania Mingi ni mijinga sana na iliharibiwa akili na Babu Yao wa Taifa chini ya ujamaa mbuzi.

Ndio maana utasikia fisadi sijui analamba asali ila hayana hata ushahidi Bali uropokaji tuu.

Akitokea Kiongozi wa ambae ana muelekeo wa kukandamiza wengi Kwa sababu za wivu na chuki basi maskini hao hufurahi sana.

Mwisho tabia ya ujamaa ni kulisha Imani ambazo hazipo yaani kama dini wanapigiwa propaganda harafu Kwa kuwa ni majinga yanaamini na hii ndio sababu utasikia Bora Magufuli lakini Uliza sasa wewe Kwa Mwendazake maisha Yako yalifanikiwaje hakuna kitu ila ataanza kutaja mifano ya wafanyabiashara walioporwa pesa basi hapo yalivyo makolo yanafurahii..

Samia kaza hivyo hivyo na Huwa napenda sana nikiona unawajazia hakuna kulemba Kila mtu afanye kazi ale jasho lake hakuna Cha Bure.

Yamekaa huko Mjini yanategemea mkulima ahenyeke harafu Rais aje aseme hakuna kuuza mazao Nje Ili yenyewe yanumue bei chee Kwa jasho la wasio na sauti,Samia amekataa huu upuuzi.
20230922_130530.jpg
 
Habari Wakuu!

Kwanza ijue nchi yako, waelewe Watu wako. Ifahamu jamii yako.

Sisi ni jamii ambayo mtu ukifanikiwa utaitwa ni Freemasonry,
Tupo kwenye jamii ambayo ukiwa na utajiri unaitwa Fisadi, Jizi au muuza madawa ya kulevya.
Tupo kwenye jamii ambayo ukimiliki vimiradi kadhaa au biashara za hapa na pale unaitwa unatumia Uchawi wa ngende. Ielewe jamii yako na watu wake.

Fanya vyovyote utakavyofanya, TOA jasho lako utakalotoa lakini elewa kuwa siku utakayofanikiwa watanzania wengi watakuweka kwenye mojawapo ya makundi hayo hapo juu.

Kwa kweli Taikon Master tangu nimezaliwa mpaka umri nilionao sijawahi kumuona Tajiri au mtu aliyefanikiwa hapa nchini ambaye Watu wanasema amepata Pesa kihalali. Hiyo sijawahi kusikia. Itakuwa mara yangu ya Kwanza na ambayo nitaiandika kwenye kumbukumbu zangu na pengine kuandika kitabu cha huyo mtu ambaye Watu watamsema amepata Mafanikio yake Kwa halali.

Leo sitaki kuwasumbua Sana,
Mama Samia kosa alilofanya ni Kutumia Ile Kanuni ya kila MTU ale urefu wa kamba yake. Kauli ambayo watanzania hawatakuja kuitaka Kwa sababu watanzania ni jamii ya kijamaa. Watu ambao wanataka kula kamba Kwa kushirikiana.

Watanzania wanavutiwa zaidi na viongozi ambao wanataka kuwafanya Watu wote kuwa Sawa ndani ya jamii. Yaani matajiri na Maskini wote wawe Sawa. Wavivu na wachapakazi wawe Sawa. Wenye bahati na wasio na bahati wawe sawasawa. Hilo Kwa Samia halipo, hiyo sio falsafa yake. Hapo ndipo anapopishana na upendo wa watanzania.

Samia anatumia Ile falsafa ya Yesu isemayo kila MTU abebe msalaba wake. Kila mtu ajikune pale mkono wake unapofikia.

Samia hawezi kumshusha wa juu ili afanane nawa Chini. Hiyo sio falsafa yake. WA Chini akitaka kwenda juu apambane kivyake vyake. Wakati vivyohivyo.

Wenye bahati wabaki wenye bahati Yao mpaka bahati Yao itakapokwisha. Wasio na bahati waendelee kuhenyeka mpaka bahati Yao utakapokuja yenyewe au Kwa wao kuitafuta.

Watanzania kama jamii hainaga Tabia ya ku- appreciate uwezo wa waliofanikiwa. Hata hapo kwenu wewe ukifanikiwa bado watakuona kama aidha umebahatisha, huna uwezo, au umetumia ndumba, au umebebwa bebwa.

Samia hiyo falsafa yake hawezi kutoboa kwenye mioyo ya Watanzania. Na sidhani kama yeye ni wale Watu wanaotafuta kupendwa au kulazimisha kukubalika.

Eeeh! Acha nipumzike tuu.

Ijumaa Kareem
Niambie yule waziri wa mapesa anayemiliki timu ya mpira na kusajili kwa pesa ya kutisha huku akiajiri wazungu kuifundisha kapata vipi huo utajiri? Mstaafu wa Msoga anayemiliki biashara kubwa akiwa madarakani kapenya vipi? Wapo wengi tukianza kuorodhesha
 
Huyo ni WA kwanza hapa Tanzania? Mnyeti alikzipata ? PM alikzipata wapi?

Nachojua mfano Mimi ni Meneja wa TanRoads mathalani Ili mkandarasi apate kazi anakuja kunihonga Sasa naachaje kuchukua pesa ya Bure? Maana hii haihusiani na execution ya kazi ni kama dalali kukutafutia mteja tuu.

Hongo za hivi ndio wakubwa wengi wanapata Sasa hapo unakuathiri vipi wewe maskini? Tafuta pesa Mzee hakuna namna 🤪🤪
 
Tafsiri yako ni Wizi si ndio Mkuu.
Kwa hiyo msemo wa kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake unauelewaje?
Sio wizi hiyo ni kanuni ya kibilia na kanuni ya kibepari,utakula Kwa jasho lako kadiri ya Juhudi zako.

Hapo kwenye Juhudi Kuna mambo mengi bahati,connection,Juhudi,kupata pande nk nk
 
Mkafanye kazi kwa bidii jamani magufuli mlisema vyuma vimekaza huyu tena mnalialia yani watanzania wanapenda vya bure.
Una uhakika sifanyi kazi, na badala yake nimekaa tu na kulialia! Na kupenda vya bure? Ni vipi hivyo vya bure mnaweza kunipa nyinyi maccm?

Ungekuwa jirani, ningekuzabua vibao vya kutosha sana.
 
Niambie yule waziri wa mapesa anayemiliki timu ya mpira na kusajili kwa pesa ya kutisha huku akiajiri wazungu kuifundisha kapata vipi huo utajiri? Mstaafu wa Msoga anayemiliki biashara kubwa akiwa madarakani kapenya vipi? Wapo wengi tukianza kuorodhesha

Sijakataa.
 
Back
Top Bottom