Kosa la Rais Samia ambalo watanzania wengi hawalitaki ni hili

Je, wakati huo ambao upigaji haukuwepo ulifikiwa na fursa au mafanikio gani?
Muwe mnasoma kwanza ninachokiandika kabla ya kuni quote! Huwa siwapendi watu viherehere.
Mimi nimeandika upigaji umeongezeka, halafu wewe unasema upigaji haukuwepo!!!
 
Huyo ni WA kwanza hapa Tanzania? Mnyeti alikzipata ? PM alikzipata wapi?

Nachojua mfano Mimi ni Meneja wa TanRoads mathalani Ili mkandarasi apate kazi anakuja kunihonga Sasa naachaje kuchukua pesa ya Bure? Maana hii haihusiani na execution ya kazi ni kama dalali kukutafutia mteja tuu.

Hongo za hivi ndio wakubwa wengi wanapata Sasa hapo unakuathiri vipi wewe maskini? Tafuta pesa Mzee hakuna namna 🤪🤪
Hongo ni hela iliyoongezwa kwenye gharama za miradi, hakuna anayetoa hongo kutoka kwenye hela yake binafsi. Pesa natafuta ndio maana siombi kwa mtu na naridhika na kidogo ninachopata kwani hata ningemiliki dunia yote mwisho mitaondoka mtupu kama nilivyokuja
 
Hakuna kitu kama hiyo na kwanza hujui unachoongea.

Unajua maana ya ushindani au unadhani anaetafuta ni uko peke yako? Madereva wanaotoa hongo Kwa traffic Huwa wanaongeza nini?

Wewe Kwa akili Yako mbovu unadhani Boeng wangepata tender ya Kutengeneza ndege bila hongo? Kwenye mazingira ya ushindani bila hongo hutoboi Iko hivyo Dunia nzima
 
Tatizo la watanzania na Wanawake wengi hasa Afrika ni kufanya imagination ya vile wanavyofikiri na kuwawekea Watu wengine hizo imagination zao kwenye fikra za wengine.

Ati kama ninadhani, ninafikiri. Hayo mawazo yangu umeyajuaje? Au ndio hizo imagination zako juu ya fikra zangu?
Sawa na wewe kuwa bilionea basi kama no rahisi
 
Kuna nyakati fulani huko nyuma nilianza kuvutiwa na hoja zako ila kadri siku zikipita naanza kuyaona mapengo mengi kwenye maandiko yako. Maana ya kula kwa urefu wa kamba hasa ndo yenyewe inayosimama na utu ama ukienda uite "ujamaa", na si kwa namna unavyojaribu kuipotosha maana hii.

Maana ya ujamaa harisi ni kwamba watu wote wafanye kazi ama washiriki kazi za uzalishaji. Mfano wa hili ni ile ikiitwa age set system, watu wote ukiachia watoto na wazee walitakiwa kuelekea kazini kuzalisha. Na hata katika maandishi fulani ya Baba wa Taifa aliwahi kuandika juu ya uhuru na kazi(freedom&work). Hii ni dhana ya kijamaa maana yake asiwepo wa kukaa akalala alafu akadai kula huyo ataitwa mnyonyaji a.ka. bourgeoisie.

Kwahiyo ukimsema mama kwa hilo basi tutasema mama ni "mjamaa" ijapo kwa mienendo yake huko wala hayuko. Katika serikali yake kaunda mfumo wa inequality, wengi wanaumia kwa ajiri ya wachache.

Majority wa nchi hii wanapambana sana lakini mfumo wa utawala ni exploitative mno, kila mahala sasa hivi ni rushwa na nepotism. Huruma za jamii zinapatikana kwa misingi ya kibaguzi, unyanyasaji na upendeleo.

Wafia nchi wanasota huku utajiri wao unagawiwa kama peremende ..where is justice, where is social justice?

Niishie hapo yasije kunikuta maana sahivi hatuna hata uhakika wa maisha yetu huku uraiani, watu wanachukuliwa na kunyakuliwa kama vifaranga kwa mwewe. Wewe pengine unayo haki ya kutamba hivyo kulingana na tawi gani umelikalia na ni tawi gani limeelekezewa upanga ila punguza utoto
 
Hakuna kitu kama hiyo na kwanza hujui unachoongea.

Unajua maana ya ushindani au unadhani anaetafuta ni uko peke yako? Madereva wanaotoa hongo Kwa traffic Huwa wanaongeza nini?

Wewe Kwa akili Yako mbovu unadhani Boeng wangepata tender ya Kutengeneza ndege bila hongo? Kwenye mazingira ya ushindani bila hongo hutoboi Iko hivyo Dunia nzima
Una akili mbovu kama mmeo
 
Una akili mbovu kama mmeo
20230922_130530.jpg
 
Wewe ndio ujipe moyo kuwa utazipata hizo Pesa unazotafuta. Pia ujipe pole Kuwa na Akili ndogo ya kudhani Watu wote Duniani wanatafuta Pesa.
Mwanamume lazima atafute pesa hilo ni jukumu tulilopewa hata kwenye vitabu vitakatifu.

Utatunzaje familia yako ikiwa hutaki kufanya kazi uingize kipato?
 
Bro rejea nchi zilizoendelea kama China, Korea, Japan, USA, Britain n.k
wako makini na rushwa wanajua jinsi inaharibu maendeleo
in Africa njia rahisi kuwa billionaire ni kuwa mwana siasa kwa sababu huku kuna rushwa na hili mama 100 kaliweka wazi tena hadharani
Lkn nchi nyingne na wenye akili kuliko wewe brother mjinga wanakemea viongozi weny rushwa wanataka uadilifu.
Binafsi kuona unatetea rushwa naumia, bora ukae kimya.
Next time uweke namba yako wakujue kbsa
 
Habari Wakuu!

Kwanza ijue nchi yako, waelewe Watu wako. Ifahamu jamii yako.

Sisi ni jamii ambayo mtu ukifanikiwa utaitwa ni Freemasonry,
Tupo kwenye jamii ambayo ukiwa na utajiri unaitwa Fisadi, Jizi au muuza madawa ya kulevya.
Tupo kwenye jamii ambayo ukimiliki vimiradi kadhaa au biashara za hapa na pale unaitwa unatumia Uchawi wa ngende. Ielewe jamii yako na watu wake.

Fanya vyovyote utakavyofanya, TOA jasho lako utakalotoa lakini elewa kuwa siku utakayofanikiwa watanzania wengi watakuweka kwenye mojawapo ya makundi hayo hapo juu.

Kwa kweli Taikon Master tangu nimezaliwa mpaka umri nilionao sijawahi kumuona Tajiri au mtu aliyefanikiwa hapa nchini ambaye Watu wanasema amepata Pesa kihalali. Hiyo sijawahi kusikia. Itakuwa mara yangu ya Kwanza na ambayo nitaiandika kwenye kumbukumbu zangu na pengine kuandika kitabu cha huyo mtu ambaye Watu watamsema amepata Mafanikio yake Kwa halali.

Leo sitaki kuwasumbua Sana,
Mama Samia kosa alilofanya ni Kutumia Ile Kanuni ya kila MTU ale urefu wa kamba yake. Kauli ambayo watanzania hawatakuja kuitaka Kwa sababu watanzania ni jamii ya kijamaa. Watu ambao wanataka kula kamba Kwa kushirikiana.

Watanzania wanavutiwa zaidi na viongozi ambao wanataka kuwafanya Watu wote kuwa Sawa ndani ya jamii. Yaani matajiri na Maskini wote wawe Sawa. Wavivu na wachapakazi wawe Sawa. Wenye bahati na wasio na bahati wawe sawasawa. Hilo Kwa Samia halipo, hiyo sio falsafa yake. Hapo ndipo anapopishana na upendo wa watanzania.

Samia anatumia Ile falsafa ya Yesu isemayo kila MTU abebe msalaba wake. Kila mtu ajikune pale mkono wake unapofikia.

Samia hawezi kumshusha wa juu ili afanane nawa Chini. Hiyo sio falsafa yake. WA Chini akitaka kwenda juu apambane kivyake vyake. Wakati vivyohivyo.

Wenye bahati wabaki wenye bahati Yao mpaka bahati Yao itakapokwisha. Wasio na bahati waendelee kuhenyeka mpaka bahati Yao utakapokuja yenyewe au Kwa wao kuitafuta.

Watanzania kama jamii hainaga Tabia ya ku- appreciate uwezo wa waliofanikiwa. Hata hapo kwenu wewe ukifanikiwa bado watakuona kama aidha umebahatisha, huna uwezo, au umetumia ndumba, au umebebwa bebwa.

Samia hiyo falsafa yake hawezi kutoboa kwenye mioyo ya Watanzania. Na sidhani kama yeye ni wale Watu wanaotafuta kupendwa au kulazimisha kukubalika.

Eeeh! Acha nipumzike tuu.

Ijumaa Kareem
Hatuwezi kutoboa kwa kupata Mali za duniani halafu tutazamie maisha mazuri.Lazima tutafute uso wa Mungu mwenye haki halafu hayo mengine yatatutafuta yenyewe
 
Mambo uliyoongea ni ya kibinafsi zaidi kuliko ya kitaifa,unaongelea watu watu watu muda wote watu watu,SAMIA ni Rais na Rais amebeba matarajio ya watu,kuna mambo ambayo ni common kwa Taifa ukiyachezea unakuwa umetengeneza ugumu kwa kila mtanzania,hawa watanzania ndio walipa kodi wa kila siku,tusiwadharau kiasi hicho hasa kwa kumtumia Rais dhaifu na UTENDAJI wake dhaifu na serikali yake dhaifu.Ukibeba matarajio ya watu KAZI yako kama kiongozi ni kurahisisha maisha yao ndicho watu wanachotarajia na si kufanya maisha yao kuwa magumu.Tuombe sote tupate KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI ili nchi ipate serikali na viongozi wanaotoka kwa wananchi na sio wanaojichagua.
 
Mnaomba hiyo Katiba mpya Kwa Nani Mkuu?
 
Bro rejea nchi zilizoendelea kama China, Korea, Japan, USA, Britain n.k
wako makini na rushwa wanajua jinsi inaharibu maendeleo
in Africa njia rahisi kuwa billionaire ni kuwa mwana siasa kwa sababu huku kuna rushwa na hili mama 100 kaliweka wazi tena hadharani
Lkn nchi nyingne na wenye akili kuliko wewe brother mjinga wanakemea viongozi weny rushwa wanataka uadilifu.
Binafsi kuona unatetea rushwa naumia, bora ukae kimya.
Next time uweke namba yako wakujue kbsa

Kukemea hakutoshi
 
Mwanamume lazima atafute pesa hilo ni jukumu tulilopewa hata kwenye vitabu vitakatifu.

Utatunzaje familia yako ikiwa hutaki kufanya kazi uingize kipato?

Wanaume wanatafuta mamlaka ili Pesa Ike yenyewe Mkuu.
Nimekupa Siri usije ukajihangaisha miaka nenda Rudi hakuna unachokifanya wala kukipata.
 
Tatizo upigaji kwa wachache umeongezeka, huku maisha ya wengi yakiendelea kudidimia. Katika hili, ajiandae tu kusikia kelele kutoka kila kona ya nchi.
Hata wakàti wa Nyerere upigaji ulikuwapo tofauti ni dimension. Hata wakati wa "shujaa feki" mwendazake watu walipiga wakiongozwa na mwenyewe.

Dunia yote kuna upigaji hata USA
 
Back
Top Bottom