Kosa la Samia ni kuleta Siasa za Zanzibar huku Tanganyika

Si lazima watii amri kutoka juu, wameamua tu kutii.

Unajua kuna Polisi walikataa kuua watu October 29 na mpaka sasa wameacha kazi ya u Polisi?
 
Muongo mkubwa, ZNZ watu wanaisema CCM na Serikali yake vijiweni na hakuna aliewahi kuchukuliwa. Munapenda kuzua vitu eti ZNZ acheni uzushi.
 
Kwani wapi nimesema muache liendelee?

Kusema hili tatizo halijaanza na Samia ndiyo kusema muache liendelee?

Unajua kusoma kwa ufahamu?

Unajua logical non sequitur fallacy ni nini?
Kwahiyo mantiki ya maswali yako ilikua ni ipi?
 
Kwahiyo mantiki ya maswali yako ilikua ni ipi?
Mantiki ya swali langu ilikuwa ni kuonesha mambo haya yalikuwapo kabla ya Samia kuwa rais na kuyapa sura ya Uzanzibari kunaweza kufurahisha watu fulani, lakini ni kasumba ya ubaguzi tu.

Kwamba Magufuli aliteka na kuua pia.

Nikisema Samia si wa kwanza kuteka na kuua hata Magufuli aliua sijasema Samia hajaua, nakanusha tu kwamba haya ni mambo ya Wazanzibari yaliyowekwa na Samia, nasema haya yalikuwapo hata wakati wa Magufuli.

Na kusema haya yalikuwapo hata wakati wa Magufuli haimaanishi muache yaendelee. Pengine inaweza kuwa ni kuwaasa muyamalize kwa sababu yamekuwa tatizo la muda mrefu.

Ushaelewa?
 
Mkuu, binafsi unaona ni nini chanzo cha haya matukio yote ya utekaji yanayofanyika kote Tanganyika na Zanzibar?
 
Watu sijui wameanza kufatilia siasa juzi
 
Tabia ya kimafia hapa nchini imeanza kitambo sana. Kadri muda unavyokwenda na watawala kubadilika, ndivyo tabia hiyo inavyoshamiri (kwa scale na scope).

In the 1990s, kulikuwa na high profile eliminations za Stan Katabalo, Lt General Imran Kombe na Horace Kolimba. Kipindi hicho pia mashambulizi kwa kutumia tindikali yalishamiri sana. Watawatala walikuwa hawajihangaishi na politically harmless critics!

Utawala wa Kikwete ulipambwa na muendelezo wa tabia ya kimafia. Hata hivyo, tabia hiyo ilianza kubailika sura. Kumbuka, Dr Steven Ulimboka alitekwa kipindi hicho. Other high-profile cases zilikuwa kushambuliwa na kuuawa kwa Professor Jwani Mwaikusa na kushambuliwa kwa waandishi wa habari Saed Kubenea na Absalom Kibanda.

Utawala wa Magufuli nao ulipambwa na muendelezo wa tabia ya kimafia. Kipindi hicho, umafia ulionekana kujikita zaidi kwenye kidnappings and enforced disappearances. High-profile disappearances za kwanza kwanza zilikuwa za Ben Saanane na mwandishi wa habari Azory Gwanda. Mo Dewji naye alitekwa kipindi hicho, lakini baadaye watekaji walimuachia bila kumdhuru kimwili. Ni katika kipindi hiki pia Tundu Lissu alishambuliwa na kunusurika kuuawa kwa risasi.

Utawala wa Suluhu unapambwa na tabia ya kimafia ambayo inaonekana kupanua zaidi mawanda ya kidnappings and enforced disappearances. Sasa hivi hata politically harmless critics wanatekwa na kupotezwa. Kusema kweli, it’s totally out of control. High-profile cases, kwa uchache, zinajumuisha abductions za Mzee Ally Kibao, Balozi Humphrey Polepole, mwanaharakati Nyagali Mdude, etc.

Truth be told, Samia The Killer has outperformed everyone. She’s the de facto queen of evils!
 
Mkuu, binafsi unaona ni nini chanzo cha haya matukio yote ya utekaji yanayofanyika kote Tanganyika na Zanzibar?
Tatizo ni viongozi kutaka kutawala kwa nguvu sana na ushawishi kidogo.

Tatizo ni wananchi kuachia matatizo haya yalipoanza, kutoyakemea, kutoyapinga, kufikiri yatatokea kwa wengine tu.

Tuna tatizo la jamii nzima. Of course kwa kanuni ya "Noblesse Oblige", viongozi wana wajibu zaidi na lawama zaidi (To whom much is given, much shall be required).

Lakini, kiukweli hata viongozi nao ni matokeo ya jamii yetu. Ni watoto waliolelewa katika familia zetu, wamesoma shule zetu, wamehudumia serikalini, wamekaa bungeni kwetu, wakishindwa maana yake hizi taasisi zote zimeshindwa kuwaandaa na tuna tatizo la kiutamaduni pia.

Matatizo yetu mara nyingi tunayaongea ki sheria (katiba mpya) na kisiasa (kuiondoa CCM), lakini hatuzungumzii sana matatizo yetu ya kiutamaduni. Matatizo ya watu karibu wote kutokuwa wawazi na wakweli, matatizo ya watu kuwa na woga sana, matatizo ya watu kutojielimisha kuhusu nchi inavyokwenda na hivyo kutoweza kufuatilia mambo kwa kina.

Haya mengine ni matatizo ya jamii nzima, si uongozi tu.

Matatizo ya uongozi yanaonekana sana kwa sababu viongozi wako juu pale, ni "tip of the iceberg".

The tip of the iceberg is usually about 10%, the rest of the iceberg is underwater.
 
Lakini haya mambo mbona yalianza hata kabla ya Samia kuwa rais?

Magufuli alipoteza watu sana pia, naye ni Mzanzibari?
KUna watu walipotezwa wakati wa Magufuli na hata wakati wa Kikwete, lakini ilikuwa kwa nadra sana, idadi yao ilikuwa ndogo sana, haifiki hata 10% ya wale waliotekwa na kuuawa na Samia. Samia ameweka record ya pekee, siyo Tanzania tu, bali kwa Afrika nzima.
 
This is a moral equivalence fallacy.

Kuua ni kuua tu. Kuua watu wachache si bora zaidi ya kuua wengi kwa sababu ya namba tu.

Na pengine kuachia viongozi kuua watu wachache ndiyo kumewafanya watawala waweze kuua watu wengi, na kwa hiyo, kuua watu wachache kulikotangulia ndiyo jambo baya zaidi, kwa sababu kumeweka precedent mbaya ikiyofuatwa na kisababisha watu wengi kuawa.
 
Kila kitu magufuli kwa hio mkuu unahahalisha yanayoendelea nchini kisa magufuli alitenda? Kwani wakati anateka na kuua akina mange hawakumsema na kumsakama kama samia wako?
Lakini haya mambo mbona yalianza hata kabla ya Samia kuwa rais?

Magufuli alipoteza watu sana pia, naye ni Mzanzibari?
 
Muongo mkubwa, ZNZ watu wanaisema CCM na Serikali yake vijiweni na hakuna aliewahi kuchukuliwa. Munapenda kuzua vitu eti ZNZ acheni uzushi.
Mimi nimeishi kule Zanzibar miaka 10 tena nimeishi kwenye jamii yao kabisa nilipanga kwenye Nyumba psmoja na familia zao kwahiyo nawajua vizuri sana tabia zao mazuri yao na Mapungufu yao , Wale Maisha yao tofauti na sisi Watanganyika kuanzia kwenye maswala ya kitamaduni na kijamii, wale kule wao tamaduni zao siyo za kijadi ni zaki Kiarabu wao wakesi zao nyingi wanaegemea kutatua kifamilia kuliko kisheria za nchi, mfano Kwenye kesi za Uzalilishaji na ubakaji kesi nyingi zinamalizwa kienyeji kisili sili. Na hata mifumu yao ya kuchakula Wanawake wa kule Usiku hawapiki chakula wanaenda kununua chips tu na Mwanaume anaenda kula kwenye vibanda vya soup, na Wanawake akimua hakupi haki ya ndoa na anaweza kwenda kwao Alaa ata mwezi bila sababu ya Msingi, na kingine wanapenda kuzaa zaidi ya Mwanaume mmoja yani wanaolewa ata mara 10, usishangae Mama ana watoto 8 na Baba zao wapo 6
 
Kila kitu magufuli kwa hio mkuu unahahalisha yanayoendelea nchini kisa magufuli alitenda? Kwani wakati anateka na kuua akina mange hawakumsema na kumsakama kama samia wako?
Wala hata hajahalalisha. Kaweka record sawa kwamba hata Magu alipoteza watu.
 
Uongozi wa namna hiyo hauwezi kuleta maendeleo hivyo ni lazima aondoke!! Hana akili, leo anasema NEPOTISM katika nchi itafifisha maendeleo kwa kuua taasisi; kesho yake anatangaza Baraza lililojaa ndugu zake kama Mawaziri wa taasisi nyeti!! Kweli pana Uongozi hapo au ni pumba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…