Wewe utakuwa ulikuwa una shida binafsi na Magufuli hapo ilitakiwa kama ni wizi useme ulianza tokea awamu ya kwanza lakini wewe unachokifanya eti ulianzia kwa Magufuli
Hujanifuatilia kwa kina tu. Na pengine siwezi kusema kila kitu katika kila post, nitakuwa naandika kitabu katika kila post.
Kimsingi hakuna kitu kipya alichofanya Magufuli Tanzania. Tofauti ni style aliyotumia kufanya mambo tu. Alifanya kibabe, kwa uwazi zaidi.
Hakuna kitu ambacho Magufuli alifanya ambacho hakikufanywa tangu utawala wa Nyerere.
Tofauti Nyerere alitumia hoja za kifalsafa na sheria kufanya mambo yake.
Magufuli alipiga marufuku mikutano ya kisiasa. Nyerere alipiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani na vya wafanyakazi kabisa.
Nyerere aliweka watu kwenye indefinite detention na kiwafungia watu majumbani mwao na vijijini mwao kuna mzee alikuwa anaomba ruhusa kutoka kijijini kwake Kagera huko mpaka utawala wa Mkapa, anafikiri bado anatakiwa kuomba ruhusa kutoka kifungo cha enzi za Nyerere.
Kutoa mfano wa Magufuli ni kuwapeleka watu hatua moja nyuma ya Samia kuwaonesha matatizo ya kimfumo ambayo hata Samia akiondokewa yatakuwapo ti. Matatizo yaliyorudi nyuma si kwenye CCM tu, bali mpaka TANU huko.
Sasa katika nchi ambayo ina matatizo systemic hivyo unawezaje kuona Samia ndiye tatizo lako kubwa kabisa?
Nimeuliza Samia akisema anajiuzuku leo, akamuachia nchi Nchimbi, ndiyo tutakuwa tumemaliza matatizo yetu ya uongozi?
Mtafurahi Mzanzibari aliyetuletea matatizo ya siasa za Zanzibar kaondoka?
Kwani Magufuli alivyoteka na kuua watu naye alikuwa Mzanzibari?