Kosa la Samia ni kuleta Siasa za Zanzibar huku Tanganyika

Siasa za Zanzibar (Unguja na Pemba) ni siasa za DAMU.

Weusi (ASP) na wenye damunza Kiarabu (Hizbu/CUF/ACT) haziwezi kuisha hivyo. Na huyo Mwinyi ni maendeleo gani kapeleka, labda kukodisha visiwa ili wajenge Hotel za kitalii.
 
Huyo jamaa anashindwa kuelewa kuwa Magufuli alidili na mapapa ila mama mpaka wapiga debe anateka
 
Nilivyofuatilia mabishano yenu, nilinusa kwamba shida kubwa ni kwamba anamkubali sana Magufuli ndiyo maana pamoja na kujifanya kutokubaliana na siasa zake ila alikwazika ulipomuhusisha na matatizo ya sasa. Nilivyombana ameshindwa hata kujificha.

Ila kwa bahati mbaya sana, watu wa aina hii wasio na uelewa huo mpana wapo wengi sana. Ndiyo maana naona siasa zetu zinaenda kuvurugika vibaya mno.

Tunaenda kuwa na siasa zitakazotawaliwa na pro-Magufuli factions, pro-Kikwete na pro-Lissu. Hizi pande zitakuwa zinajenga mahusiano ya muda yasiyo ya kudumu. Zitakuwa siasa kama za Kenya.

Wajanja wa Mtandao waliwahi kuuona mchezo wakamuweka Mpina kama msemaji wa watu wa Magufuli na wakamuwahi kumpa ubunge binti yake ila muda utasema kama kweli wanasimamia kile alichoamini au watatumika tu.
 
Wewe utakuwa ulikuwa una shida binafsi na Magufuli hapo ilitakiwa kama ni wizi useme ulianza tokea awamu ya kwanza lakini wewe unachokifanya eti ulianzia kwa Magufuli
Hujanifuatilia kwa kina tu. Na pengine siwezi kusema kila kitu katika kila post, nitakuwa naandika kitabu katika kila post.

Kimsingi hakuna kitu kipya alichofanya Magufuli Tanzania. Tofauti ni style aliyotumia kufanya mambo tu. Alifanya kibabe, kwa uwazi zaidi.

Hakuna kitu ambacho Magufuli alifanya ambacho hakikufanywa tangu utawala wa Nyerere.

Tofauti Nyerere alitumia hoja za kifalsafa na sheria kufanya mambo yake.

Magufuli alipiga marufuku mikutano ya kisiasa. Nyerere alipiga marufuku vyama vya kisiasa vya upinzani na vya wafanyakazi kabisa.

Nyerere aliweka watu kwenye indefinite detention na kiwafungia watu majumbani mwao na vijijini mwao kuna mzee alikuwa anaomba ruhusa kutoka kijijini kwake Kagera huko mpaka utawala wa Mkapa, anafikiri bado anatakiwa kuomba ruhusa kutoka kifungo cha enzi za Nyerere.

Kutoa mfano wa Magufuli ni kuwapeleka watu hatua moja nyuma ya Samia kuwaonesha matatizo ya kimfumo ambayo hata Samia akiondokewa yatakuwapo ti. Matatizo yaliyorudi nyuma si kwenye CCM tu, bali mpaka TANU huko.

Sasa katika nchi ambayo ina matatizo systemic hivyo unawezaje kuona Samia ndiye tatizo lako kubwa kabisa?

Nimeuliza Samia akisema anajiuzuku leo, akamuachia nchi Nchimbi, ndiyo tutakuwa tumemaliza matatizo yetu ya uongozi?

Mtafurahi Mzanzibari aliyetuletea matatizo ya siasa za Zanzibar kaondoka?

Kwani Magufuli alivyoteka na kuua watu naye alikuwa Mzanzibari?
 
Tatizo kubwa la siasa za watu wajinga wa Afrika ni kuwa siasa zinazozunguka around personalities.

Hizi ni siasa za watu shallow vichwapanzi ambazo haziwezi kuangalia policies, haziwezi kuangalia systemic issues.

Ndiyo maana mtu kama Polepole kajisikia huru kutoa siri za ndani kabisa za CCM, kuwa CCM huwa wanawachezea watu kwa mpango wao wa "kumwaga oil".

Awali tukisikia habari za "kujivua gamba".

Maana yake ni kwamba hakuna mabadiliko ya msingi yanayofanyika, CCM inabadilisha watu tu, inajinadi kuwa imefanya mabadiliko.

Nyerere kwenda Mwinyi ulifanyika ujinga huohuo, Mwinyi kwenda Mkapa ujinga huo huo, Mkapa kwenda Kikwete ujinga huohuo, Kikwete kwenda Magufuli, ujinga huohuo. Samia kaja katujaza ujinga huohuo.

Lakini rais akizoeleka tu, tunaona kuwa CCM ni walewale. Tunabadilishiwa style tu lakini we are still fvcked.

Kwa hiyo hapa tatizo ni CCM. Tatizo ni utamaduni wetu wa kukubali mazingaombwe yao.

Na bado watu wanajikita kwenye kutaka kumtoa Samia bila kuelewa kuwa hata Samia akiondolewa leo, matatizo yetu yapo palepale tu.

How do these people not see this?
 
Huyo jamaa anashindwa kuelewa kuwa Magufuli alidili na mapapa ila mama mpaka wapiga debe anateka
Hakuna mtu yeyote anayestahili kutekwa, pia, ukiruhusu mtu mmoja tu kutekwa umehatarisha usalama wa watu wote.

Mwanzo kabisa mngekataa mtu yeyote kutekwa, utekaji usingezoeleka na kuwa kitu cha kawaida mpaka ukashamiri nchi nzima.

Huelewi wapi?
 
Hee kumbe jembe nalo ni neno baya aiseee yale yale ya tume iliyoanzishwa na samia kuchunguza uharamia wake. Gen Z wana akili sana. Ningewaiga wala nisingekujibu. Anyway hongera kwa kujipendekeza kwa kiranga,naona hadi umemtag watu na role models waooo
 

Shairi Yako na wewe watakufuata wakuteke na kukuua
 
Kumuita jembe kumeniambia mengi ambayo haukuhitaji tena kuyatamka. Nimejua yote niliyohitaji kujua juu yako na mitazamo yako.

Huyo Kiranga mada nyingi tu tunatofautiana na hii mada nilisita kuingia maana inawezekana tungetofautiana tena. Ambacho sikuelewa ni angle ambayo mnatofautiana na nilinusa kwamba umekwazika sana kwa jambo ambalo kwa mtu kama wewe ambaye umeonyesha kupinga mauaji yaliyotokea, nilishangaa kukasirika kiasi cha kuanza kumrushia maneno kisa amemtaja Magufuli. Nikaona ni vyema "nilishe udadisi wangu" kwa kuchokonoa na kuuliza shida ni nini.
 
Ukweli ni kuwa wanaompinga Samia na kumkubali Magufuli wapo wengi sana.

Magufuli alijijengea taswira ya "demigod" kwa watu hawa. Waliona tu mazuri yake ila mapungufu na makosa yake hawakuyaona na hata walikuwa tayari kuyatetea kwamba yalifanyika kwa maslahi ya taifa. Hawa watu ndiyo aina kama ya huyo Numbisa. Hawa watu ukiwawekea Janet Magufuli au Jesca Magufuli kwa tiketi ya CCM na Tundu Lissu upande wa CHADEMA, watamchagua Janet au Jesca.
 
Ni vizuri umefunguka mapema ili nisipoteze muda wangu kujadiliana na wewe.
Hatu muungi mtu mkono kwa sababu yoyote bali kwa sababu za haki na uzalendo...lissu na chadema yote ilikengeuka na kushikamana na wahuni ndiyo maana chadema kilipoteza nguvu kabisa ...lissu alishikamana na mafisadi kina kikwete na Rostam na chadema yote ndiyo maana walipigiana simu na kupongezana baada ya JPM kuuliwa.
 
Mtu akishamuita Magufuli jembe unajua huyu mshamba bado ana akili zilizoishia kwenye ukulima wa jembe tu.

Yani hata mifano yake ya ukulima wa jembe tu.

Waafrika wengi hawawezi kufanya siasa za policy, siasa za systems.

Wanaishia siasa za ukabila, siasa za kumuangalia mtu.

Ndiyo maana hawa wametekwa na Magufuli lakini wanaamini Magufuli jembe.

Samia anawateka wanamuona shetani.

Wakati Samia michezo mingi ya utekaji kajifunza kwa Magufuli.
 
Hawa watu wanejaa ujinga na ushamba mtupu.
 
Stalker wa kiranga finally ushapata access ya kuchat nae hongera sana mkuu. Ila kuwa makini atakuchoka mapema
 
Bahati nzuri sikukuquote ni kiherehere chako tu kutaka ukaribu na kiranga ukaona udakie visivyokuhusu anyway kidume umepata chat nae mkuu maana mnakubaliana kwa kila kitu. All the best kiranga stalker
 
Stalker wa kiranga finally ushapata access ya kuchat nae hongera sana mkuu. Ila kuwa makini atakuchoka mapema

Bahati nzuri sikukuquote ni kiherehere chako tu kutaka ukaribu na kiranga ukaona udakie visivyokuhusu anyway kidume umepata chat nae mkuu maana mnakubaliana kwa kila kitu. All the best kiranga stalker
Ni suala la muda tu kuwajua watu na fikra zao za kweli. Wewe hauna uchungu wowote na mauaji yaliyotokea. Na inaonyesha upo jukwaani kwa kazi maalum. Nimekuweka kwenye "red alert".

Na leo nimemuona mwenzio kama wewe. Hapo utakuta mnaishi kwa kodi za wananchi kwa "kazi hii" halafu mnategemea nchi itafika popote.
 
Mkuu nimekuachia kidume wako uchat nae vizuri acha kulia lia kwa migazeti tele. Ila kiranga akisoma hapa anatakiwa awe makini sana na wewe kwa haya maandishi yako daima muuaji huacha alama eneo la tukio. All the best mtu wa kazi maalum
 
Mkuu nimekuachia kidume wako uchat nae vizuri acha kulia lia kwa migazeti tele. Ila kiranga akisoma hapa anatakiwa awe makini sana na wewe kwa haya maandishi yako daima muuaji huacha alama eneo la tukio. All the best mtu wa kazi maalum
Yaani haya yote kisa umeambiwa anachofanya Samia kilianza toka enzi za Magufuli? Ni hilo tu au kuna mengine maana unashangaza sana?
 
Afisa doria. Mbona kiherehere hivyo yaani umeumia kuliko niliyemquote. Pole jamani nimekuharibia dili la kumkamata kiranga
Yaani haya yote kisa umeambiwa anachofanya Samia kilianza toka enzi za Magufuli? Ni hilo tu au kuna mengine maana unashangaza sana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…