Kuanza leo usiku mpaka Nov ndio tutajua kama nchi hii nayo ina Deep State au namna gani?

Yaani huu ni Uchaguzi Mkuu wa 13 Tanzania, lakini watu wana porojo kibao. Nchi hii ni imara na itaendelea kuwa imara. Tunakunywa Konyagi tunaendelea kunywa raha mustarehe hadi Serikali Mpya ya CCM itakapoingia madarakani!
Wewe unachokijua ni CCM ya Samia na Genge lake, basi. Nje ya hapo hutaonekana tena humu JF.
Hili ulisha litabiri mwenyewe, kama hukumbuki!
 
Unazidi kupotoka kwa sababu umeshindwa kumtetea huyu kilaza-mjinga wako. Ni mjinga mmoja asiyejua lolote kuhusu siasa sembuse ukomunisti. Narudia kusema kwamba ukinifanya mimi mshauri wa CCM kuhusu --mbinu za kushinda kwa haramu, njia za ku deal na wapinzani wa ndani na nje ya CCM, nitafanya kitu kinacho make sense kuliko wanavyofanya sasa. BTW. Hivi Tanzania ya sasa unaweza kusema inaendeshwa kikomunisti?
 
Wengine wamekariri hata hawajui maana ya ukomunisti ni nini? Hivi Tanzania ya sasa ina hata chembe za ukomunisti? Mnadhani ukomunisti unakuwa defined na kukataa upinzani au kuua wapinzani? Nendeni shule mkasome.
 
Inawezekana huo "Mswada" anao uzungumzia yeye ni kitu kingine! Wala hakugusia mswada ulihusu mambo gani?
Kuna Act ame assent Rais mwaka 2023 na kupitia hio act kuna reform nyingi zimefanyika mojawapo ni Kuwa kutakuwa kuna Deputy DGIS wawili mmoja anatoka Bara mwingine anatoka Zanzibar, Pia Tiss imepewa jukumu la kuwalinda Viongozi wakuu Wa Nchi na Immediate family zao,

Ila pia Tiss imerudishwa Ofisi ya Rais na Wizara itabaki responsible kwa mambo ya Kibudget tu itafute uisome
 
Wengine wamekariri hata hawajui maana ya ukomunisti ni nini? Hivi Tanzania ya sasa ina hata chembe za ukomunisti? Mnadhani ukomunisti unakuwa defined na kukataa upinzani au kuua wapinzani? Nendeni shule mkasome.
Kwa kweli inashangaza sana. Hivi Russia bado ni nchi ya Kikomunisti? Uganda ni nchi ya Kikomunisti?
 
Itikadi zinasemaje? Huko katika hizo nchi umeona zinashabaha tofauti? Kabla ya kusoma twende kwanza kuangalia muundo na picha

Muundo wa CCM ni sawa na China, Russia nk hawana tofauti. Vyama pinzani ni ombwe kuonesha Kuna demokrasia ikizingatiwa ni nchi isiyofungamana na upande wowote

Tumia vitabu vyako kusoma huku ukiangalia uhalisia ulivyo, kitabu cha Karl max cha mwaka 1907 (kwa mfano) hakina nguvu au mashiko sana kwa maisha ya sasa 2025 au miaka 100 ijayo

Ndio maana utakuja kuona watu walikuja ku criticize theories mbali mbali kwa kuwa neno lako wewe au yule sio mwisho au kuzuia wengine kufikiri
 
Mom ni nani na ana uwezo mkubwa namna ile!
 
Kwa kweli inashangaza sana. Hivi Russia bado ni nchi ya Kikomunisti? Uganda ni nchi ya Kikomunisti?
Inashangaza kama tunavyosema sisi ni wajamaaa

Je kweli ni wajamaaa?
 
Uzalendo kwanza

Zidumu fikra za mwenyekiti

Mapambio kwa Rais na viongozi wake kwa kila kitu

Kikundi cha watu wachache wanaamua baadae wengine (wengi) wanapitisha

Mambo ni mengi ya ufanano na siasa za kikomunist
 
Mwesigwa ni mtu wa hovyo sana yule kiumbe
Kwa anachokifanya Kwa Sasa,
Ndicho wenye mamlaka walimtuma kwenda kukisomea ughaibiun,

jamaa keshahitimu na kesharudi home na anaderiver jinsi waliomsomesha wanavyotaka.

Sasa Nyie WA tabaka jingine,
Labda nanyi tafuteni mtu wenu mkamsomeshe uko ughaibuni.

Nae aje pale TISS kumcounter-deriver mwesigwa.

Kitu ambacho ni nearly impossible Kwa mwendo wa siasa za nchi unapoelekea
 
Inashangaza kama tunavyosema sisi ni wajamaaa

Je kweli ni wajamaaa?
Ni CCM iliyobaki na muundo wa Kikomunisti, amoja na kwamba utendaji na utekelezaji wa mambo siyo wa kikomunisti, kama ilivyo kwa CCP (China Communist Party).
Kilichobaki sasa ni chama kinacholindwa na hao TISS na mitutu ya Bunduki dhidi ya vyama vya upinzani na waTanzania kwa ujumla.
CCP, hata siku moja hawaendi mitaani kuwahonga wananchi baiskeli na mifuko ya matakataka yenye picha ya Xi.
 
Na hao ndo marafiki wakuu WA chama Cha mapinduzi, na mkutano mkuu wa chama juzi kati, wacommunist wote (friends of CCM) walikua na uwakilishi wao pale chamwino.
 
Uzalendo kwanza

Zidumu fikra za mwenyekiti

Mapambio kwa Rais na viongozi wake kwa kila kitu

Kikundi cha watu wachache wanaamua baadae wengine (wengi) wanapitisha

Mambo ni mengi ya ufanano na siasa za kikomunist
Mbali ya muundo wa CCM; hakuna hata moja wanalofanya CCM lenye mfanano na chama cha Kikomunisti cha China.
 
Hujui maana ya ukomunisti na CCM ya sasa siyo wakomunisti. Sina muda na kiazi kama wewe unayebisha bila kujua unazungumzia nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…