Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini

Hayo yamezungumzwa na Abdi Issango ambaye ni mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar Es Salaam alipokuwa akihojiwa na Philip Mwihava katika kipindi cha Power Breakfast on Saturday pale Clouds Fm.

Baada ya Machinga, sasa ni bodaboda na bajaj zamu japo bajaj za walemavu zimeruhusiwa kuingia mjini.

Una maoni gani juu ya hili? Tunaelekea wapi?

View attachment 1991793
ipo siku tutaimba wimbo mmoja, hao nao wanasema matatizo ya nchi hii ni ya wana CDM. Funda nyondo, ccm hoyeeeee
 
Hayo yamezungumzwa na Abdi Issango ambaye ni mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar Es Salaam alipokuwa akihojiwa na Philip Mwihava katika kipindi cha Power Breakfast on Saturday pale Clouds Fm.

Baada ya Machinga, sasa ni bodaboda na bajaj zamu japo bajaj za walemavu zimeruhusiwa kuingia mjini.

Una maoni gani juu ya hili? Tunaelekea wapi?

View attachment 1991793
Ni jambo. Utaratibu huu upo hata kwa nchi za wenzetu. Pale Perth, Australia, kuna sehemu moja yenye biashara nyingi, na watu wengi, ni marufuku magari, pikipiki au baiskeli kuingia. Kule electric bikes, kama huna uwezo wa kutembea unazichukua, unazitumia, ukimaliza unaacha sehemu hiyo hiyo. Magari yanaruhusiwa kuingia kuanzia saa 6 - 11 usiku kwaajili ya kuingiza bidhaa.

Huu utaratibu ungeweza kufanyika hata eneo la soko la Kariakoo.
 
Kuna watu wameshiba humu ila kwa kua hawaja wahi kupambana hawataelewa umeandika nn.
Vijana wengi ni machinga na bodaboda. Tena kuna hadi watu wa makamo tuko nao hapa posta ni bodaboda. Sasa mtu kama huyo unafikiri anapenda kuwa bodaboda!? Ni kwa kuwa ndiyo option aliyobaki nayo.
 
Ukiona mtu anafikiria alipoanzia kufikiria na siyo alipoishia utajua kuna tatizo mahali, subiri.

Ukiona mtu anafikiria alipoishia kufikiri bila kutakafari alipoanzia kufikiri basi fikra zake zitaendelea kuwa zile zile hata kama kuna tatizo.
 
Nilisema! CCM imeshaishiwa pumzi subiri matokeo! Ombi wapinzania legend mtu mwenye uwezo kwa wananchi! Msituletee watu wa ovyo kama Lisu!CCM hawa wapesi sana!
Mshebzi mwili mzima, mlete mamako tumchague
 
Wangeondoa na Maguta yanatia aibu sana na kuchafua uhalisia wa jiji.
 
Tatizo ni hao wanaondesha hivyo vyombo wengi wamekuwa watu wa hovyo sana wanashindwa kuthamini kazi zao ila kuwazuia hapana wangeweka course ili watu waende shule na watoe vibali kwa watakao fanikiwa ila bajaji zibaki za walemavu tu bodaboda ziwe monitoring
Wengi wa hao walemavu hawana leseni. Hao wangewasaidia wakasome.
 
Maeneo tulimo hamishwa sie machinga wenzetu wa bajaji ndio wamegeuza kuwa vituo.
Ni kweli walitucheka. Tukawajibu huyo mwendawazimu anayejiita makala kwenye huu utawala wa wapiga dili atawashukia muda si mrefu.
 
Vijana wengi ni machinga na bodaboda. Tena kuna hadi watu wa makamo tuko nao hapa posta ni bodaboda. Sasa mtu kama huyo unafikiri anapenda kuwa bodaboda!? Ni kwa kuwa ndiyo option aliyobaki nayo.

Kwa nini vijana wengi na hata watu wa makamo ni wamachinga na bodaboda? Wamachinga na bodaboda ni mtaji wa wanasiasa.
Wanasiasa wanatengeneza tatizo halafu wanalitatua huku wamachinga na bodaboda wakidemka.
Siku hizi vijana wengi hawafikirii zaidi ya umachinga na bodaboda huku wanasiasa wakiendelea kutesa.
 
Ndizo ajira zenye mitaji nafuu zaidi. Bodaboda na bajaji zina wamiliki na hawa wanapeleka hesabu tu. Hapo mtaji ni ujuzi wa kuendesha chombo.
 
Mimi ofc mathalani ipo Sokoine Drive, mchana natakata niende Kinondoni makaburini fasta kwenda nakurudi, kwa hiyo sina haki ya kupanda boda?

Hivi sisi abiria wa katikati ya miji wanatuchukuliaje?
Matajiri
 
Ni jambo. Utaratibu huu upo hata kwa nchi za wenzetu. Pale Perth, Australia, kuna sehemu moja yenye biashara nyingi, na watu wengi, ni marufuku magari, pikipiki au baiskeli kuingia. Kule electric bikes, kama huna uwezo wa kutembea unazichukua, unazitumia, ukimaliza unaacha sehemu hiyo hiyo. Magari yanaruhusiwa kuingia kuanzia saa 6 - 11 usiku kwaajili ya kuingiza bidhaa.

Huu utaratibu ungeweza kufanyika hata eneo la soko la Kariakoo.
Usafiri wa bodaboda unatakiwa upigwe marufuku jijini Dar. Huwezi kutengeneza usafiri wa mwendo kasi huku ukitegemea usafiri wa pikipiki kwenye sehemu za jiji.

Najua bodaboda ni delicate issue, sijui ni usafiri wa maskini n.k lakini linahitaji mtu mwenye balls kutokomeza kabisa usafiri wa pikipiki Dar.

Usafiri wa mabasi ya mwendokasi na hata wa trams ambao ni cheaper na salama uimarishwe jijini.
 
Hayo yamezungumzwa na Abdi Issango ambaye ni mkuu wa Usalama barabarani Kanda Maalum ya Dar Es Salaam alipokuwa akihojiwa na Philip Mwihava katika kipindi cha Power Breakfast on Saturday pale Clouds Fm.

Baada ya Machinga, sasa ni bodaboda na bajaj zamu japo bajaj za walemavu zimeruhusiwa kuingia mjini.

Una maoni gani juu ya hili? Tunaelekea wapi?

View attachment 1991793

Machinga alipofurushwa mijini haba bandugu bengine bakachekelea.

Yale yale ya jogoo aliyekuwa akishadadia mwenziwe mbuzi kuchinjwa kwa ajili ya sherehe.

Asijue kuwa waalikwa wanaweza kuja kidogo kuliko walivyotarajiwa na hivyo kumchinja yeye ikawa ndiyo sahihi zaidi.

😂😂

Hiiiiii bagosha!
 
Nilisema! CCM imeshaishiwa pumzi subiri matokeo! Ombi wapinzania legend mtu mwenye uwezo kwa wananchi! Msituletee watu wa ovyo kama Lisu!CCM hawa wapesi sana!
Kiongozi/chama ambacho kuwepo madarakani hakutegemei kura za wananchi kamwe hawezi kuwanyenyekea hao wapiga kura.
 
Vijana wengi ni machinga na bodaboda. Tena kuna hadi watu wa makamo tuko nao hapa posta ni bodaboda. Sasa mtu kama huyo unafikiri anapenda kuwa bodaboda!? Ni kwa kuwa ndiyo option aliyobaki nayo.
Sababu ya kuwazuia boda kuingia mjini ni nini?

Ova
 
Back
Top Bottom