kwa hii miji yetu ambayo karibu 70% ya wakazi ni maskini sijui kama maamuzi hayo yana afya.
Umasikini sio sababu ya kukosa utaratibu. Maisha ni mjumuiko wa taratibu tofauti tofauti!! Kwani wamenyang’anywa pikipiki zao au kuzuiwa kufanya shughuli zao??
Tuseme unamiliki nyumba za kupangisha. Ufahamu kuwa mmoja wa wapangaji wako amegeuza chumba kuwa danguro, kiwanda cha kutengenezea pombe haramu, kafanya karakana au anapangisha mtu mwingine - utasema kwa kuwa alikulipa kodi basi anaweza kufanya chochote na chumba hicho??
Hujasikia magari makubwa hayaruhusiwi katikati ya mji? Kwa nchi za wenzetu kuna sehemu hata magari hayaruhusiwi bali wenda kwa miguu tu!!
Tubadilike na kufungua macho, sisi ni sehemu ya dunia!!