Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini

Kuanzia Novemba Mosi Bajaji na Bodaboda marufuku kuingia Mjini

kwa hii miji yetu ambayo karibu 70% ya wakazi ni maskini sijui kama maamuzi hayo yana afya.

Umasikini sio sababu ya kukosa utaratibu. Maisha ni mjumuiko wa taratibu tofauti tofauti!! Kwani wamenyang’anywa pikipiki zao au kuzuiwa kufanya shughuli zao??

Tuseme unamiliki nyumba za kupangisha. Ufahamu kuwa mmoja wa wapangaji wako amegeuza chumba kuwa danguro, kiwanda cha kutengenezea pombe haramu, kafanya karakana au anapangisha mtu mwingine - utasema kwa kuwa alikulipa kodi basi anaweza kufanya chochote na chumba hicho??

Hujasikia magari makubwa hayaruhusiwi katikati ya mji? Kwa nchi za wenzetu kuna sehemu hata magari hayaruhusiwi bali wenda kwa miguu tu!!

Tubadilike na kufungua macho, sisi ni sehemu ya dunia!!
 
Kwani Leseni za biashara zao zinasemaje?
Katazo halijasema kwa wasio na leseni ya kuingia mjini, limesema wenye bodaboda na bajaj wote. Sasa kuwa na leseni halali itakuwa ni moja ya hoja mahakamani kwamba nina leseni na bado nimefukuzwa isivyo halali.
 
Zamani walidai zinatahisisha wizi ila siku hizi wizi hamna...na wala haziko nyingi kiasi kwamba zinachafua mji
Hii nchi ina vituko mkuu, niliwahi kwenda Bank na bodaboda aina ya Boxer nikamwambia nisubiri hapa parking sichelewi... Aisee huwezi amini, natoka bank bodaboda simkuti bahati nilikuwa na namba yake nikampigia akaniambia wale maaskari wa bank wamemfukuza na kumwambia kwamba pikipiki aina ya Boxer ni marufuku kupaki bank!! Daaah nikabaki nacheka tuu...
 
Munawaonea tu
Kero kubwa kariakoo ni malori, malori, malori
Na musipoyatoa kariakoo malori basi hatuwapi kura ng'o
 
Ni kwa dasilamu tu au Mimi yote tz hii?
Ama kweli..ngoja nikimbie hii nchi
 
Watanzania tunatakiwa tuachane na mazoea. Kujaza bajaj na pikipiki mjini ni umasikini MKUBWA
Tuambie hiyo ni kwa mujibu wa sheria ipi?? Kuna siku mtasema ni marufuku kuvaa yebo yebo au kutumia simu ya Tecno mjini... Swala la msingi ni kuweka utaratibu usio na ubaguzi.
 
Hii ndilo tatizo kubwa sana na utawala wa Tanzania. Na hasa lilizidi wakati wa Magufuli. Nchi inaongozwa bila organisation yoyote. Ni matamko na usanii wa kujiweka mbele mbele kwenye social media ili ionekane viongozi ni wachapakazi kumbe ni maigizo tu.
Katiba, katiba, katiba.....
 
Huwa wanatoa hayo matamko karibu kila baada ya miaka kadhaa...wanakuwa serious kidogo baadaye maisha yanendelea kama kawaida
 
Nasikia ukitokea Morogoro road mwisho ni fire, ukiwa unatokea airport mwisho Banda la Ngozi Na barabara ya Mwenge mwisho Ni wapi?
 
maamuzi yaleyale kuamua bila matumizi ya numbers kwa maana ya data..

Hesabu zipi mlipiga kujua zinahitajika au hazihitajiki, yaana kwa kutumia data zipi mkagundua hazihitajiki?..

Miundombinu na Usafiri hapo Dar es salaam bado si rafiki vs population ya mji hivi sasa..
Hali hiyo inafanya matumizi ya boda na bajaj kuwa makubwa ili watu waspeed up operations na movements zao..baadala yake nini kimefanyika kuziba hilo gap?...

Mwendo kasi unaoanzia kibaha to kivukoni via city centre and Manzese mpaka sasa bado capacity yake ni ndogo na inasuasua kiasi cha binadamu kusimama kuanzia kivukoni to Mbezi...huyi binadamu ameamu kupanda bodaboda sasa.... la msingi ni kuboresha usafiri wa mwendo kasi na uwe na option nyingi pamoja na watu kutokaa sana vituoni...
Option nyingi ni pamoja na kuwa na mwendokasi express, excutive kwa maana ya nauli yake from mbezi to posta ni 2000 labda na haisimami to post au to Mbezi..
Serikali mboreshe ile delux train na huduma ya usafiri kutoka Gongo lamboto to Posta ikiwa pamoja na kutatua matatizo ya foleni..

TUSIPENDE KUCHUKUA MAAMUZI BILA DATA WALA KUTOA SULUHU YA MATATIZO, UKITOA MAAGIZO BILA DATA WALA SULUHU KWA MAANA YA MBADALA WATU WATAKUJA TENA NA SOLUTION ZAO AMBAZO HAZITAKUFURAHISHA PIA..
 
Sio kila wakati kutaka kuonyesha ubabe wa bila kutumia akili

Huwezi kufukuza tu wakati wanajua fika hao wanahitajika sana kwa mishe mishe za haraka
Wapo mpaka wanaobeba parcels au documents za muhimu

Bora kuwa na mpaka wa marufuku kuingia na anaeingia nakazia yaani chombo chochote cha moto kilipe hela kama congestion charge na Camera zifungwe na kurekodi kila anaeingia na analipa kwa muda maalumu

Anakuwa analipia kwa masaa 24 kiasi fulani hapo wengi wataondoka wenyewe au hata watalipia serikali itakusanya fedha za kuendeleza miradi ya jiji

Duniani nchi zilizoendelea wanapambana na uchafuzi wa hewa kwa hiyo wamejiongeza na nyie mjiongeze sio kuwafukuza

Kwa sasa mataifa makubwa wanajuandaa kuyaondoa magari ya mafuta yote na wameweka malengo na ili watu wanunue magari ya kisasa zaidi

Watu hawafukuzwi bali gharama zimekuwa nyingi na bei ya mafuta imepanda zaidi, kuingia mjini gharama mara mbili
Ila ndio hivyo

Ubunifu unatakiwa sio kufukuza tu
Akili za Wakuu wa wilaya na mikoa 200 ni sawa na wewe jamaa pekeyako.
 
Kwa hiyo hapo zilizo wekewa katazo la kuingia mjini ni Bajaj na bodaboda ila pikipiki nyengin za matairi 2&3 zenyew ruksa tu?! Huo ni uonevu
 
Utakuwa unamiliki bodaboda wewe..vumilia kama machinga walivovumilia kutolewa town
Machinga gani katolewa town? Unazani ni rahisi hivyo?
Nenda kkoo alafu uje utuletee mlejesho km machinga wameondoka.
Ni mbwembwe ambazo haziwezekani kirahisi
 
Vijana wangu Kama 4 pale kivukoni wanaondolewa barabarani duh hii serikali hii

Wakati ninalipia Kodi za kutosha kwa kupitia boda zangu.

Hii Nchi hi basi tu!!! Kuja kutengeneza route mpya na kupata wateja wapya na kuzoea kituo sio chini ya miezi 6 Sasa Hawa vijana watakuwa wanakula wapi?

Mimi nitalipaje vibali vikiisha? Hatuna serikali kiukweli hapa.
Mkuu na kuna watu wanashangilia tu hawatazami kua tuna takiwa tuwe na mipango mizuri sio matamko tu watu wanajiajiri leo mtu anakuja anakuambia usije mjini na boda lako.
 
maamuzi yaleyale kuamua bila matumizi ya numbers kwa maana ya data..

Hesabu zipi mlipiga kujua zinahitajika au hazihitajiki, yaana kwa kutumia data zipi mkagundua hazihitajiki?..

Miundombinu na Usafiri hapo Dar es salaam bado si rafiki vs population ya mji hivi sasa..
Hali hiyo inafanya matumizi ya boda na bajaj kuwa makubwa ili watu waspeed up operations na movements zao..baadala yake nini kimefanyika kuziba hilo gap?...

Mwendo kasi unaoanzia kibaha to kivukoni via city centre and Manzese mpaka sasa bado capacity yake ni ndogo na inasuasua kiasi cha binadamu kusimama kuanzia kivukoni to Mbezi...huyi binadamu ameamu kupanda bodaboda sasa.... la msingi ni kuboresha usafiri wa mwendo kasi na uwe na option nyingi pamoja na watu kutokaa sana vituoni...
Option nyingi ni pamoja na kuwa na mwendokasi express, excutive kwa maana ya nauli yake from mbezi to posta ni 2000 labda na haisimami to post au to Mbezi..
Serikali mboreshe ile delux train na huduma ya usafiri kutoka Gongo lamboto to Posta ikiwa pamoja na kutatua matatizo ya foleni..

TUSIPENDE KUCHUKUA MAAMUZI BILA DATA WALA KUTOA SULUHU YA MATATIZO, UKITOA MAAGIZO BILA DATA WALA SULUHU KWA MAANA YA MBADALA WATU WATAKUJA TENA NA SOLUTION ZAO AMBAZO HAZITAKUFURAHISHA PIA..
Ushauri wako umezingatia data zipi zenye namba zinazooshesha kuwa ni sahihi kwasasa kufuata hatua ulizoshauri?
 
Back
Top Bottom