Kudai Israeli ni Taifa la Mungu huku Wayahudi wakimkaata Yesu, ni ushahidi hizi dini zimejaa uongo mwingi

Imani inafanya watu wasihoji, na ndio maana hata Wafuasi wa Kibwetere hawakuhoji matokeo yake wakaangamia.
Suala la msingi ni kwamba imani ipi?

Imani ya Ukristu inamhitaji muumini aelewe na kuhoji kile anachofundishwa, kabla hajaridhia kukifuata.

👉 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo. -Matendo ya Mitume 17:11

Dini yoyote inayosomesha imani dufu -- kufuata tu bila kujua sababu ya fundisho husika -- ni utapeli.

👉 Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu. -1 Petro 3:15
 
Nina mashaka na uislam kushikamana sana na waarabu, ukiwa na free mind lazima uone utata.
 
kasome kwanza bible usiwe kama andazi.

bible imeandika wazi,Yesu alikataliwa na hao wayahudi,ndio sababu hata ya kuuawa kwake.
"Yesu alikataliwa na hao wayahudi" sasa hili taifa teule limetokea wapi?
Enyi wagalatia jitafakarini!!!!
 
Unaposema “misingi ya mafanikio yako ni ukristo” unamaanisha kitu gani?

Fuatilia vyema utafahamu mifumo yote ina watu wenye mafanikio na walioleta mabadiliko makubwa duniani.

Iwe ni Christians, Muslims, Budhas, Hindus, Chinese etc etc.

Fuatilia, kama hujui uliza.
 

Na Bethlehemu na Nazareth na pia Galilaya nadhani ni miji ipo upande wa Palestina kwa ramani ya sasa hivi! Damascus ya kwenye biblia ipo Syria, Jangwa la Sinai lipo Misri, Babylon ipo Iraq.
 
Ukristo umetungwa baadae xn baada ya yesu mwili wake kuacha dunia.
Mafundisho yote muhimu yajengayo msingi wa imani ya Ukristu, Mwana wa Adamu aliyafundisha kikamilifu kwa muda wa miaka 3.5 akiwa na wanafunzi 12++

👉 [18]Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

[19] Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;

[20] na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, Mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. ~Mathayo 28:18-20
 
Point yangu ni kuwa matatizo ya Africa yanaletwa na sisi Waafrika wenyewe. Wazungu walitufanyizia na wameshaondoka ila watawala wengi wa kiafrika wamegeuka kuwa wakoloni weusi.
Kwani mimi kuna sehemu nimesema matatizo yetu waafrika yameletwa na wengine?

Ndo maana nimesema utumwa wa kinguvu uliisha, lakini upo wa ki hiyari na pia “mental slavery”

Utumwa wa kiakili umechangia kwa kiasi kikubwa zaidi kwenye hali iliyopo Africa hususan viongozi wale ambao nao ni zao la wananchi wenyewe.
 
Jewish people ! Jews ! = wayahudi !
They believe in Moses = Musa !
They have unique believe rather/more than what proclaimed of moses miracles!
Musa alipomkabidhi Haruni kuwaongoza wakimbizi, ilifikia hatua jamaa(Haruni) alishindwa kuwadhibiti kuumba/kuchonga masanamu ambayo hao wakimbizi(wanaIsrael-mayahudi) wanayatukuza na kuyaamini hadi leo ikiwemo Sanduku la Agano.
Halafu sisi wamatumbi tumeizika na kuikataa mizizi yetu ya mibuyu, mironge, mikwizingi, minyaranyanyara, miarovera, midimu, mikunungu, mikuzwingi, minangari na migagani
 
😆😆😆😆
 
Nimejaribu kukuelewa, ila nimeshindwa. Maana haionekani kama unauliza au unajibu.

Ni kama sentensi zako zinauliza, lakini mwishoni hakuna kiulizo. Sasa hapo ni ngumu sana kueleweka.

Kinachoshangaza zaidi, wadau wamekufurahia. Sijui wanafurahia vile ambavyo umeandika sentensi tata au la?
 

Ina maana mmeshindwa kumuelewa mleta mada ya kuwa ametambua chanzo cha huu uwongo umeanzia kwenye hiyo bibilia mnayomtaka akaisome tena....
Ukiwa na akili timamu ya utashi wa kujitambua kama binadamu lazima utatambua kuwa dini zote ni pilika za wajanja ambazo watu weusi mmeshupaza shingo kujifanya mnazijua kuliko waliozileta mpaka wanawaonea huruma kwa misaada ya kila kukicha.....
 

Sasa mambo ya akina Lissu yanaingiaje kwenye mada hii? Duh!
 

Wengine waseme risasi 16 ikiwa ni pamoja na Yeye Lissu mwenyewe alisema, leo tena zinakuja risasi 38, kesho tutaambiwa risasi 200 yote mradi ni kumkuza mtu! Mimi najua hata tembo tu angepigwa risasi tano angekufa hapo hapo, sembuse binadamu apigwe risasi 16 au 38 mnazotuambia abaki? Na wakati dereva aliyekuwa naye hapo hapo jirani kwenye gari isimpate hata risasi ya kumparua hata mguu au mgongo tu? Mimi ningekuwa nachunguza hili tukio ningekomaa kwanza na huyo dereva!
 
Dini hizi ni utapeli mtupu!

Zimelifanya bara la Africa kuwa bara la hovyo kuliko yote na watu wake hovyo zaidi.
Waliokuwa brainwashed watakupinga ila unasema ukweli mtupu, turudi imani zetu za kale..
 
ukielewa maana ya imani,utagundua kuhoji ni dalili ya ugonjwa wa akili.

imani inakuelewa uamini Mungu aliumba mtu kwa matope,akawaje na nyama??huhoji hili wewe mbioooo mpaka kwenye uteule wa israeli.

bangi bila msosi.
Hapo tatizo siyo kuhoji, bali majibu unayopewa.

Kwa mfano, sayansi ikikwambia umetokana na nyani, hapo utaelewa nini?

Ni lazima tukiri kwamba kuna mambo tusiyoweza kufafanua kibinadamu, na hapo ndipo tunakutana na imani katika miujiza ya Mungu.
 
Sema wewe sasa alipigwa ngapi? au alikatwa na mapanga?
 

Technocrat :

Hajaanzia kwenye Biblia Mkuu, kama angeanzia kwenye Biblia hilo swali lake angeli frame tofauti kabisa! Amekiri ni Mkristo, Mkristo gani hata hajui ABC ya imani yake? Hajakiri kabisa Biblia imemchanganya.......

Hiyo hoja yako haya dini zote ni pilika pilika za wajanja....hiyo ni mada tofauti mkuu......Mababu zetu walikua na dini zao za asili ....nani mjanja aliyewaanzishia hizo imani....hiyo ni mada tofauti mkuu....Maana itabidi tuanze Antropology 101...Uone imani ya dini kwa mwanadamu ilivyo sehemu ya mwanadamu.
 
Onyesha ushahidi

Kasome kwenye tourati ndiyo utagundua kuwa Wayahudi wanamkataa Yesu kwa kusisitiza kuwa Yesu siyo mwana wa Mungu kwa vile Mungu hakuzaa mtoto na pia hakuna kitu kinaitwa utatu mtakatifu. Hiyo ni tosha kabisa kujibu swali lako. Pia wanakuambia Yesu siyo Mungu.
 
Unangoja hadi wengine waamini ndipo wewe uamini?

👉 Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. ~Yohana 20:29
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…