Kufanya biashara na Watanzania mtandaoni ni taabu sana

Duh utakua ulienda kununua mkorogo aisee
 
Vipi husomi feedback za wateja huko kikuu?
 
Kuna mmoja muuza saa nilikutana nae insta kuna saa niliiona town posta muhindi anakomaa 480K yeye akawa anaiuza 225K nikaona hapa hapa kitonga wala sikupatana nikauliza namna ya kuipata akaniambia njoo dukani makumbusho au ije nilipo (Kariakoo) niongeze 5K.

Nikamwambia ok mpe mtu ailete,ilipofika kuitizama ni fake siyo kama ile aliyoi-post maana kuna namna posta waliniambia jinsi fake inavyokuwa nikaikataa yule aliyeileta nikampa 5K yake nikamwambia ukifika mwambie jamaa nimeikataa kwa sababu hii hii na hii,nimekaa nishasahau hiyo ishu nashangaa text za matusi zinaingia kwenye simu yangu nikamuuliza bro inakuwaje mzee kwani umepata hasara gani na mletaji nimemlipa na sikuridhika na kitu ulichompa maana kipo tofauti na ulicho-post mtandaoni akazidi kunitukana nikaachana nae.

Jamaa hawana akili wanadanganya kwenye picha wanakuletea kitu fake ukiwaambia ukweli wanakutukana.
 
Sas wew s ungemripotia police kuwa natukanwa bila sababu unamjambisha
 
Wauzaji wa magari hasa madalali wa magari ndio misukule.
Ukifika Bei na kumwambia akuunganishe na mwenye Mali ndio utajua Kuna umuhimu wa kuagiza gari au kununua toka show room au kununua kwa mwenye gari unayemjua.
Hao wakoje mkuu eleza sifa zao nichukue taadhari
 
Wauzaji wa magari hasa madalali wa magari ndio misukule.
Ukifika Bei na kumwambia akuunganishe na mwenye Mali ndio utajua Kuna umuhimu wa kuagiza gari au kununua toka show room au kununua kwa mwenye gari unayemjua.

Tunakuunganishaje na mwenye Mali sasa wakati kuna chain ni mwenyewe sijui gari ya nani[emoji1787][emoji1787]
 
Mimi biashara ya mtandaoni siiamini hata kidogo,hata Alibaba nahisi napigwa sembuse kibongobongo ndo huwezi kula mia yangu,
Ukiwa hivi vitu vizuri hutatumia mkuu,au utakuwa unaingia gharama sana ili kuvitumia.

Mimi nikiona kitu kinauzwa nikakipenda wala sijiulizi mara mbili mbili,namshukuru Mungu sijawahi kung’atwa japo nakiri udhaifu sina subira ya kuanza kuchunguzana na seller kama nachunguza mchumba,hivi kuna mwamba nimemtumia 35K aniunge bundle la Voda inaenda week ya tatu kimya uzuri bado yupo responded nikimuuliza anajibu smoothly na pia ni biashara tuliwahi kuifanya ndo maana sina wasi sana.
 
Kuna wale wanauza spare parts za gari kwa bei ya jumla. Unakuta mtu kapost picha bei haweki unauliza kwenye comment halijibu. Ukienda inbox hajibu
Wanazingua sana tena mfano wawakilishi wa Befoward Tz wanajikuta sana mkuu! Kuna mmoja nilikuwa nachati nae kuhusu parts fulani aisee hakunipa ushirikiano wabongo customer care bado sana.

Mjapani mwenyewe hadi simu anakupigia wenzetu wanathamini sana customer
 
Elimu ya customer care mkuu unamaanisha nini kuweza kuvumilia ujinga wa wengine..

Ili kupunguza maswali unaweka maelezo yote yaliyoshiba tena kwa msisitizo ili mtu akija inbox basi aje kama mnunuzi. kama sio mnunuzi ni alipite tu tangazo.
Hapa inabidi ujichunguze wewe... Huna ujuzi wa huduma kwa wateja japo maarifa unayo. Ukiwa na ujuzi huo hutawachoka badala yake utawatafutia namna ya kuwapunguzia maswali
 
Aaah!! Niko na mambo mengi ukipata muda soma au Google customer behaviour mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…