Ni nani aliye na nafuu kati ya wana CCM au Wapinzani, au wote hali zao ziko sawa isipokuwa wale tu wanaojisalimisha kwa mtu mmoja?
Tumeona walionunuliwa tokea upinzani wakiula, kwa teuzi mbalimbali au kuahidiwa mambo kadhaa.
Sasa tunawaona walioko huko huko CCM, lakini wakawa na mawazo yasiyokuwa kwenye mstari wa mwenyekiti wao nao wakionjeshwa shubiri.
Kwa hiyo, ni sahihi kwamba haijalishi wewe upo upande gani, CCM au Upinzani; kama mawazo yako ni nje na yale ya Mwenyekiti huwezi 'survive'.
Tena nadiriki kusema kwamba heri ya wale waliopo upinzani na wamekataa kuuza utu wao, kwani bado wanayo nafasi ya kueleza mambo wasiyoafikiana nayo hata kama hayampendezi mwenyekiti.
Ukiwa ndani ya CCM hata hili dogo tu la kutetea mawazo yako ambayo pengine hayampendezi mwenyekiti hutakiwi kuyawasilisha.
Kwa hiyo ieleweke wazi kwamba wote walioko ndani ya CCM wapo huko kwa njia za 'ku'survive'. Ni lazima ukubali kila kitu anachotaka mwenyekiti. Wote wapo huko kumfurahisha mwenyekiti ili mambo yao yafane, na sio kwa sababu wanakipenda chama chao na sera zake.