Wanasiasa,mjuwe sisi wananchi,hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa,kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani,tukishapata mahitaki muhimu,hatuna zaidi ya hapo.
Basi nyie wachumia tumbo msiojua mbele wala kesho kaeni kimya.
 
Hicho kibovu ndio maana yeye Ni rais na kwa vile ashaonja utamu sidhani Ni rahisi kihivyo ajitose kwenye fungu la kukosa.
 
Mkuu kuna dikteta mwingine Ikulu anayedhani ana haki ya kutuamulia Watanzania vile atakavyo yeye kinyume na Katiba ya Nchi.
Hivi kasema uchumi utatengemaa lini?

Na kipimo cha uchumi kuwa mzuri ndipo katiba ifanyike kipimo cha uchumi huo ni kipi; hadi hapo kila mwananchi atakapokuwa na Noah Yake?

Naona mama hajui namna ya kudanganya ili watu waweze kuamini ayasemayo.
 
Rais kutuzuia wananchi kutaka namna ya kuongozwaje hiyo ni dharau kubwa ya rais na chama cha mapinduzi kwa wananchi.
Hilo ni jambo ambalo hatuwezi kulikubali!
Atawaambia vumilieni; mbona miaka yote mlivumilia na hiyo katiba mbovu hadi alipokuja kuivuruga hata hiyo mbovu mtangulizi wake?

Atawatuliza kwamba yeye atafuata hiyo mbovu bila kuivunja hadi hapo uchumi utakapokuwa katika hali nzuri..., hana haja ya kueleza uchumi wa namna hiyo ni wa aina gani!
 
KWA kweli kitendo Cha mama alichokiongea kuhusu vyama vya siasa sijapenda,kwamba anaendelea na katazo lile ambalo ni kinyume Cha katiba, kwamba mtu afanye mikutano katika eneo lake, mh SSH umenikwaza Sana KWA kauli yako, sio sawa
 
Mama anawafurahisha wapinzani kweli kweli ngoja ifike 2024 ndo ataona rangi zao
 
Ajabu ni kwamba kila rais anayeingia hutaka tuamini kwamba nchi ilikuwa inaliwa na hivyo inahitaji kujengwa upya.Ukiwasikiliza utafikiri hawakuwa sehemu ya serikali zilizotangulia.Anadai ajenge uchumi Kwanza,je,huo uchumi ataukamilisha baada ya muda gani? Kwa mujibu wa katiba iliyopo amebakiza miaka minne tu ikiwa tungelikuwa na uchaguzi huru na wa haki.Ataanza kutwambia ,huu uchumi ninaoujenga nitamwachia nani?
 
Nilikuwa na bado nipo makini kusema lolote juu ya huyu mama, maana huwezi mtabiria mtoto akianza kuona!.

Wale wanazi wa kusifia na kusema tuliumizwa sana huko nyuma nawafuatilia kwa kuzoom nione wanachokoment.
 
Hata wewe huwezi kuongoza nchi eti kila mwananchi atasema lake na mapendekezo yake na wewe ufuate tu,nchi haitatawalika maana mnadhani hilo ndilo linalowezekana,msidhani katiba ni kitu rahisi sana,kina madhara yake pia
 
Samia anacheza vizuri huu mziki, leo anapiga rungu inakua zogo, kesho anatupoza na lingine tunashangilia, kesho kutwa rungu tunaanza yalaaaaaa next anatupoza tena tunashangilia.

Hivo hivo Mama tutafika.
 
Hapa Uko Sahihi 100%, Mfano ni Uongozi wa Awamu ya Tano, nchi iliendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja. Alilokuwa wanalisema ndio ilikuwa sheria na kila mtu alikubaliona nao apende asipende...Katiba mpya ndio jibu la mambo ya namna ile...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…