Kwa huu upeo wako wa kufikiri, hukutakiwa kabisa kuchangia chochote kwenye huu mjadala. Ulitakiwa usome tu na kwenda zako kujitafutia huo mkate wako wa kila siku!Wanasiasa,mjuwe sisi wananchi,hatutaki madaraka yoyote kwenye siasa,kwetu sisi twahitaji mkono wende kinywani,tukishapata mahitaki muhimu,hatuna zaidi ya hapo.
Pamoja na hayo lkn mama bado anashaurika. Tatizo liko kwa wale waliomzunguka ni namna gani wanamshauri.Poleni sana maana mlikurupuka nyote michadema
Wanasiasa sio Wananchi?Je katiba mpya ni takwa la wanasiasa au la wananchi?
Babu ndiyo umeamka?Unahitaji nani akupe hiyo katiba mpya?
Nchi inaongozwa na Katiba ya Nchi..sio ya Chama BladiFakin weweBadilisheni kwanza katiba ya chama chenu
Watu mnakuwa wagumu kuelewa sijui mnawazaje, ipo hivii katiba iliyopo ni mbovu mkuuMumewauliza wananchi kama wanataka Katiba mpya au wanataka uchumi?.Wananchi wengi,tunataka uchumi,tupate mkate wetu wa leo na kesho,mambo ya Katiba ni yenu nyinyi wanasiasa,sisi wananchi bora mkono uwende kinywani.Hebu anzeni nyinyi wanasiasa muwaulize wananchi,hata kwa kupiga kura,kwenye maeneo yenu.
Sio chadema wanataka katiba mpya hata mm mwanccm nataka katiba mpya,Yaani nyie chadema mnajidanganya kuwa hicho mnachokitaka nyinyi ni hitaji la kila mtu mko wachache sana mnaolazimisha hiyo katiba yaani kama vile hamjui kama kuitengeneza inatumika hela acheni upiumbavu wenu mpeni muda atengeneze uchumi hayo ya tamaa zenu za madaraka yatafuata baadae hata mkipewa hiyo katiba mpya mnayoitaka hamuwezi kushinda hata siku moja hamna sera nzuri
Kwani shida kubwa ni katiba mpya au viongozi kufuata katiba? Kwa sababu hata hii katiba tunayoilalamikia ina mambo mengi mazuri tu lakini viongozi wetu mengine hawayafuati.Hapa Uko Sahihi 100%, Mfano ni Uongozi wa Awamu ya Tano, nchi iliendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja. Alilokuwa wanalisema ndio ilikuwa sheria na kila mtu alikubaliona nao apende asipende...Katiba mpya ndio jibu la mambo ya namna ile...
Nani alikwambia katiba mpya ndio inapandisha uchumi?Habari wakuu?? Ni mambo ya ajabu sana kusikia kila siku, kujenga nchi, kutengeneza ajira, mm najiuliza, Mpaka lini???? Hivyi kweli ni kwa sababu watanzania ni wapole ndo maana tunaambiwa mambo yaleyale, toka wakati wa jpm ni maneno hayohayo , jamani itafika wakati watanzania uvumilivu utawashinda, nchi hii uchumi umeyumba na hata ajira kwa sababu ya katiba hii, sasa kama hamna katiba mpya huo uchumi utapandaje???? Tunahitaji katiba mpya
Kwa hiyo Nchi hii aina demokrasia Mama anaongoza kidikteta?Utakuza vipi uchumi bila demokrasia?Wawekezaji na Demokrasia ni sawa na mtoto na mbeleko! Ikikatika mbeleko, mtoto huanguka...
Hiyo ya kupoza hapa na pale ni jambo zuri lakini ni short term. Kwa mfano akishamaliza kuondoa Mabaya ya Magufuli then yeye ana nini cha kuoffer?. Ni lazima asimame sasa ajipambanue kwa ujasiri kuonyesha anajua Taifa linahitaji nini. Asiangalie utswala wake wa miaka mitano au Tisa anayoweza kukaa nadarakani. Aangalie miaka 50 au 100 ijayo.Samia anacheza vizuri huu mziki, leo anapiga rungu inakua zogo, kesho anatupoza na lingine tunashangilia, kesho kutwa rungu tunaanza yalaaaaaa next anatupoza tena tunashangilia...
Unaelewa kuwa mikutano ya kisiasa siyo tu kwamba ni haki yetu ya kikatiba bali ni universal declaration of human rights?Kwa hiyo Nchi hii aina demokrasia Mama anaongoza kidikteta?
Ndio maana hapo juu nilisema tatizo kubwa ni viongozi kufuata yaliyomo kwenye katiba unaweza kuwa na katiba nzuuuri ila kama haifuatwi ni kazi bureUnaelewa kuwa mikutano ya kisiasa siyo tu kwamba ni haki yetu ya kikatiba bali ni universal declaration of human rights?View attachment 1834320
Kuwa na katiba bora hata kama haifuatwi kwa wakati huo ni one step ahead kwa sababu ukishakuwa na katiba bora kinachofuata ni mikakati ya kupigania katiba hiyo ifuatwe.Vita ya kupigania demokrasia siyo vita ya siku moja bali ni vita ya kudumu na kija jambo litakuwa archieved kwa muda wake.Ndio maana hapo juu nilisema tatizo kubwa ni viongozi kufuata yaliyomo kwenye katiba unaweza kuwa na katiba nzuuuri ila kama haifuatwi ni kazi bure
Kwani nani amekuwa na uhuru ambao upo kinyume na katiba?Hata kama kuna mtu amekuwa na uhuru ambao upo kinyume na katiba mahakama si zipo!Si apelekwe mahakamani?Rais au wewe mnapotaka kututafsiria maana ya uhuru na mipaka yake ni mmekuwa mahakama?Kama kuna mtu ana practise uhuru ambao hauna mipaka si apelekwe mahakamani?Ila pia tukumbuke hakuna uhuru usio kuwa na mipaka tumeshuhudi kipindi cha nyuma wanasiasa wetu walipokuwa huru kidogo matusi,kejeli,maandamano yasio na kichwa wala miguu kila uchwao ila kwa sasa Nchi imetulia kidogo
Mikutano ya kisiasa ifanyike ya ndani kwa mujibu wa sheria ipi?Katiba tuliyonayo inaruhusu mikutano ya nje,sasa wewe na Rais mnataka ifanyike mikutano ya ndani kwa mujibu wa katiba ipi?Yaani mnalazimisha tuvunje katiba?Mikutano haijakatazwa ila kila mtu afanye kwenye jimbo lake shida ni kwa wale wasio na majimbo inabidi wafanye mikutano ya ndani hiyo imeruhusiwa