Huenda anaisujudia hii iliyopo kwakua ndio umemfanyia "nipige tafu"
 
Siku 100 mama aanze mchakato wa katiba kweli?!! Mimi sio CCM lakini nakataa.

Mama amekuta nchi imeoza,imefungwa kila kona,inanuka uozo,ni lazma aifungue kwanza,aanze kuitibu ndipo mambo mengine yafuate.

Katiba mpya sio wapinzani au watanzania tu wanaitaka ila hata mama mwenyewe SSH ni muhimu kwake kwa manufaa ya nchi yake Zbar. Zbar haina tofauti na jimbo ndani ya nchi, haina maamuzi yake yenyewe,imecheleweshwa kimaendeleo na viongozi uchwara.

Sasa mtawala kapatikana wa wa Zanzibar na hana uhakika wa kuchaguliwa tena na chama chake,akishindwa tena unategemea ni lini huu mtego wa muungano fake utaondoka? Labda aje afe Rais mwingine madarakani.

SSH anawavutia kasi tu.
 
Chini ya Ibara ya 3 ya Katiba ya nchi yetu, Tanzania inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa tangu mwaka 1992. Utekelezaji wa majukumu ya vyama vya siasa ikiwemo mikutano ya hadhara hautegemei hali ya uchumi tulionao. Mikutano ya hadhara ya kisiasa ni haki ya kikatiba.
 
Mkuu; haya ni mawazo na tabia ya kizembe.
 
Kwani wanasiasa sio wananchi? Au wewe unapoongelea wananchi unamaanisha kiumbe gani. Hata hivyo yote unayojinasibu nayo bila muongozo kamwe usifikiri yatafanikiwa.vinginevyo msome mtoa mada umuelewe.
 
Mama umeanza vizuri lakini jana umechafua hali ya hewa.

Fikiria tena mama etu kabla hujachelewa.

Kikwete aliweza na alitoa uhuru 100% kwa wanasiasa kujiachia na uchumi wa mtu mmoja mmoja ulikuwa fresh.

Kumbuka miongoni mwa sababu za kuchukiwa Magu ni pamoja na mambo hayo mawili, fanya leo kesho aijuae ni Mungu pekee.

Kila la heri namuomba Mwenyezimungu akufunue macho uone na uwe kiongozi na siyo MTAWALA.

Tchaoooo!
 
Hakuna asiyejua kua ikipatikana katiba mpya hasa ile ya mzee Warioba itaondoa nafasi zote za Wakuu wa Wilaya na mikoa, Wakurugenzi hawatasimamia tena uchaguzi. CCM wanajua kabisa wamechokwa na wananchi wanategemea zaidi kubebwa bebwa zaidi na vyombo vya dola.

Hawa vijana wa ccm wao ni bendera upepo wanaona katiba ikipatikana watakosa ulaji. Licha ya katiba kutajwa katika ilani yao lakini wamegeuza hili suala
 
kuandika katiba mpya ni mchakato unao hitaji fedha nyingi.
kwa sasa nchi yetu imeshuka kiuchumi kutokana na janga la korona, hivyo ni busara kwa sasa kama taifa kiongozi wetu na sisi wanachi tukajikita kujenga uchumi wetu.
katiba ni mchakato unao hitaji muda.
hivyo naungana na Rais kwa sasa kulingana na hali ya kiuchumi tuliyo nayo tufanye jambo moja kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Kilichoshuka ni kasi ya ukuaji wa uchumi, lakini uchumi wetu bado unakua.

Usisahu kuwa tuko uchumi wa kati!
 
kuandika katiba mpya ni mchakato unao hitaji fedha nyingi.
kwa sasa nchi yetu imeshuka kiuchumi kutokana na janga la korona, hivyo ni busara kwa sasa kama taifa kiongozi wetu na sisi wanachi tukajikita kujenga uchumi wetu.
katiba ni mchakato unao hitaji muda.
hivyo naungana na Rais kwa sasa kulingana na hali ya kiuchumi tuliyo nayo tufanye jambo moja kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…