Kuhusu Mungu na chanzo cha Ulimwengu, kuna mahali hatuna taarifa kamili/sahihi?

Kwanini watu huanguka mapepo?, na kwanini wengine hupandisha mapepo, makanisani wanapoombewa.

Kama mapepo yapo na malaika wapo.

Kama mapepo yapo na shetani yupo

Kama malaika wapo na Mungu yupo

Kama shetani yupo na Mungu yupo

Na Mungu ndiye mfalme na mkuu wa wote na vyote, Mungu mmoja muumba wa mbingu na nchi

Na dini zipo kuelimisha watu kuhusu Mungu na matakwa yake.(Yani Mungu anataka tuishije, tufanyaje na tuweje ili mwisho tuweze kufika kwake mbinguni)
 
Haya Mkuu nimekubali kabisa ... Daaah my hands are up on you!!!
 
Nadhani wewe ni mgeni humu JF,

Ni sawa unataka kumfundisha Albert Einstein au Isaac Newton physics.

Halafu Ukianza kuwekewa calculations ngumu ngumu za kifizikia na kihisabati utakimbia mwenyewe.

Kiranga ni next level kwenye maswala ya kujenga hoja.
 
Hatuwezi fanana katika kutazama jambo. Wapo wanaomsifia Makonda wapo wanaomponda. Maisha yapo hivyo.

Relax!!!!!
 
Si kwamba akili ipo, bali ni kwamba ufanyaji kazi wa ubongo wako upo.

Kitu ambacho hata kwa wengine kipo.

Wewe mfano ukifa huwezi tena kusema una Akili kwa sababu ufanyaji kazi wako wa ubongo umekufa.
Ubongo na akili ni vitu tofauti vyenye kazi tofauti. Chizi ana ubongo lakini hana akili.
 
Hatuwezi fanana katika kutazama jambo. Wapo wanaomsifia Makonda wapo wanaomponda. Maisha yapo hivyo.

Relax!!!!!
Wewe ndio inabidi u relax!!!

Na uchambue maoni yako kwa kina.

Kabla ya kufanya "ad hominem attack" kwa mtu, Hakikisha kwanza huyo mtu hoja zake umezielewa sio umekurupuka tu kumshambulia pasipo kuchunguza ukweli wa hoja zake.
 
Ubongo na akili ni vitu tofauti vyenye kazi tofauti. Chizi ana ubongo lakini hana akili.
Chizi sio kwamba hana akili, ila ufanyaji kazi wa ubongo wake una dosari kidogo.

Kwani wewe hujawahi kuona watu waliokuwa machizi wamepona na kurudi hali zao za kawaida?

Je madaktari walirekebisha akili ya huyo chizi kwa kuishika na kuitibu?

Au walitibu ubongo wa chizi ukafanikiwa kurudi katika hali yake ya kawaida ya ufanyaji kazi?
 
Ubongo sio akili, haiwezekani kutazamana katika ramani ya shuhuli za ubongo na kutabiri au kujua emotions au ufahamu na uelewa wa mtu. Hiyo yote ni kazi ya Mind.
 
Ubongo na akili ni vitu tofauti vyenye kazi tofauti. Chizi ana ubongo lakini hana akili.
Mkuu mimi ninaona hiyo situation kuwa chizi amepata hitilafu ya kiafya katika ubongo wake hivyo ufanyaji kazi wake umepata shida na hivyo utendaji kazi wa ubongo huo kwasababu unaenda ukiwa una hitilafu, basi hata akili inayotokana na utendaji kazi wa ubongo huo nayo inatoka ikiwa na hitilafu.
 
Maswali ya kijinga haya. Kwahiyo unataka ufananishe ushahid wa uwepo wa akili na uwepo wa mungu?
Nami nikuulize unaamini una DNA? Umewah kuziona?
Lengo lilikuwa kumfahamisha mto mada kwamba haijalishi kwasababu kitu hakionekani basi hakipo.

Kuhusu DNA, Naamini ninayo na sijawahi kuziona.
 
Kumbuka Brain ni physical, ili ipate hitilafu basi sababu inakuwa physical pia.
Sasa nadhani unafahamu kuna watu wamepata uchizi bila hata kuguswa physically.

Kupata uchizi ni matokeo ya kuvugika kwa mfumo wa akili, yani bado brain inakuwa inafanya kazi vizuri tu na ina sence na kutafsiri vitu kama maumivu,harufu, sauti na mengineyo.
 
Ubongo sio akili, haiwezekani kutazamana katika ramani ya shuhuli za ubongo na kutabiri au kujua emotions au ufahamu na uelewa wa mtu. Hiyo yote ni kazi ya Mind.
Bila ubongo unaweza kutumia hiyo akili yako kufikiri?

Kama ubongo sio akili, Tukutoe huo ubongo kichwani halafu utumie hiyo akili yako kufanya vitu.

Je Hilo linawezekana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…