Kuingia kwa vyama pinzani Afrika kutaleta maendeleo kwa haraka (ndani miaka 2 au 3) kama wananchi tunavyotarajia

Kuingia kwa vyama pinzani Afrika kutaleta maendeleo kwa haraka (ndani miaka 2 au 3) kama wananchi tunavyotarajia

Rijali jandoni

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2018
Posts
2,174
Reaction score
2,265
Mimi nadhani ifike wakati na kukubali kwamba sisi wa africa bado hatujui tunapo kwenda na tulipotoka siku zote hakuna mtu au familia ambayo itaendelea kuwa na mambo makubwa pasipo kuwa na umoja hasa kwa upande wangu nadhani:-

Uwepo wa kitu kinacho itwa demokrasia na vyama vingi ilikuwa ni mtego kwa nchi za africa hasa baada ya upatikanaji wa wazo tunaloita uhuru wa bara la afrika, waliokuja kutawala kuua na hatimae kuondoka na mali nyingi za africa tukiwemo Tanzania walianzisha mambo mengi ambayo mpaka leo yana tutesa na hasa hili la uwepo wa vyama vingi kwa akili ya kwamba kutakuwa na maendeleo

Amini usiamini wewe kijana wa leo ingelikuwa nchi zote za afrika ndani ya miaka 50 baada ya upatikanaji wa uhuru tungekuwa na chama kilichoweza kupingana na sera za mataifa ya kizungu nadhani tungekuwa mbali sana tunaona hiyo kwa nchi hasa za asia wameweza kutunza umoja wao na hata uwajibikaji katika uongozi wao

Nadhani uundwaji wa vyama pinzani ni kuleta ugombanishi wa fito kwenye ujenzi wa nyumba ya familia moja kutumia kivuli cha demokrasia wakati ukiangalia katika nchi zao hata bara la marekani waliendelea na chama kimoja zaidi ya miaka 40 wakiwa wana jijenga kisera,kiuchumi na hata kisiasa ukija uingereza,hispania na nchi za kiarabu mpaka leo kwenye ngazi ya ufalme wapo hivyo hivyo

Sasa leo kwa nchi zetu za africa hasa vijana wa leo huwa tuna ingia kwenye mtego mmoja wa kutaka mabadiliko ya chama kingine sikatai na siwezi kuwabishia maana ndio watu wanacho elewa kwamba ukiwa unabadilisha vyama kwa awamu ndio kutakuwa na maendeleo kwa kasi nadhani ni dhana potofu

Najua wapo watakao dhani ya kwamba natetea upande mmoja ila dhumuni langu ni wewe uelewe namna hawa watu wanavyo jaribu kuvuruga mambo
leo angalia Nigeria kinacho enda kutokea ni mtego mdogo ambao wamekubali kuingia ukiangalia Nigeria ni nchi ya kwanza kuwa na mafuta na uchimbaji kuanza kuliko hata nchi ambazo zipo chini ya UAE (waarabu) sasa leo ina nasa kwenye mtego mdogo sana

Na hata ukija ukiangalia nchi kama libya ndio usiongee walikuwa wana kila kitu ila kwa akili na kuwa brain washed wakaamini wana stahili zaidi kuliko walichokuwa wanapata 2008 Libya afya ilikuwa bure elimu nzuri miundombinu ya kutosha kitu ambacho nchi kama marekani hawana hata afya bure ila wakashawishi wananchi ya kwamba Gaddafi hafai na anakula sana wakijua kwamba tukiua nyoka mkubwa tutakula mema zaidi
dopl3r.com - Memes - Before After IRAQ LIBYA

Kilicho tokea ni kwamba wametokezea nyoka wadogo na hata wengine wasiojulikana mpaka leo libya haina miundombinu ya mwanzo miji imegeuka kuwa magofu ni huruma na mafuta na rasilimali nyingine watu wana jilia tuu
Before, After Photos of NATO Intervention Highlight Devastation in Libya
Libya before and after | Libya, Muammar gaddafi, Democracy

Ifike wakati waafrika wajue hata nchi kama marekani unayo isikia leo ilitumia takribani miaka 80's na kuendelea ili kufikia angalau kwenye kiwango kizuri cha uchumi sasa wao wamesha tambua ya kwamba africa kuna rasilimali wanacho leta ni ugombanishi tuna bomoa amani kwa kivuli cha uhuru wa kujieleza na chama kingine kiingie madarakani leo waingie wengine madarakani mpaka wakae sawa tuwape miaka 30 tuseme hapo bado hawajarudisha gharama zao mfumo hawaja uweka sawa sasa tutajikuta inafika miaka 80 ya uhuru bado Tanzania hatuna cha maana kikubwa kama watu fulani waliaminiwa waongoze naamini wanajua tunapoenda tatizo letu ni kwamba nchi za africa hasa sisi wananchi tuna tamanishwa na miundombinu ambayo nchi za magharibi wameipata kwa kuiba na kuchukua rasilimali zetu kiutapeli na hata kwa kuua na uzulumishi

ni nchi gani ya Africa ilisha hoji uendeshwaji wa kampeni za marekani nani Africa alisha hoji uwepo wa familia za kifalme uarabuni miaka yote uingireza hispania na nchi nyingine zenye maendeleo tunayoziba akili zetu kutojua yametokana na nini tukumbe sisi wa africa hatuibi hatupori viongozi wana jitahidi na wanafanya kazi kwenye mazingira magumu na hatarishi sasa kama vyama vya ukombozi masharti yapo hivi je wengine itakuaje ulaji kwa africa upo maana nchi za magharibi ndio wanapo tajirikia sasa leo nchi ya africa iinuke iwe kama china au Malaysia una dhani ni furaha kwao? ndioutakuwa mwanzo wa pandikizi kwa mataifa yetu ya africa

leo Africa mtu akila kuku na viazi kesho tukitaka kujenga nyumba tutoke kwenye kupanga yupo radhi amwambie mzazi usijenge tuendelee kula viazi na kuku na jirani yako alie kupangisha akiona mzazi wako ana hamia kwake ana kushauri uue na wewe una kubali ukiamini utakula kuku zaidi kumbe ndio alikuwa ana kuletea vyote hivyo hebu tukae chini na tutathimini je wanataka tujenge nyumba yetu au bado wanatamani kodi zetu za kupanga?

Je hawa jamaa wana tutakia mema watu ambao walikuja na kuua wazazi wetu watu ambao wanakuja na kuchoma chanjo huku tukijua zina ponyesha magonjwa kumbe wanaanzisha magonjwa mengine africa ?

leo mtoto wako mdogo wa kike anashauriwa saa nyingine hata kupewa vidonge vya uzazi wa mpango na vinapelekea kufa na hata kansa ya kizazi mwishoni hazai na africa tunapungua leo wana kuja na kusema wewe hautakiwi kuishi hivi una hitaji uhuru zaidi upi basi wange utoa tangu ukoloni wao na mateso yao leo nani ameteseka zaidi ya muafrica katika dunia hii na bado wanataka kukuaminisha hauteseki na hawana nia mbaya na wewe mtoto wa africa?

wangetaka tuishi vema si wangefanya tokea enzi wanakuja kugombania Africa
Leo uchukue hata mzee wa mwaka 1940's mwambie babu au bibi naomba historia ya africa ana anzia kwenye ukoloni?
hii ni sawa kweli kwetu yaani waafrica hatuna na hatujui thamani yetu hatujui historia yetu hatujui utamaduni wetu tufikirie sana hasa vijana mtu alietesa babu na bibi zako ndio mfumo mmoja mpaka leo, na leo anakuja kuku tangazia utapata amani ukianza kuandamana na kupigana wenyewe kwa wenyewe africa tunaenda wapi? Naandika hivi kwasababu tunaona ya nigeria yanavyokuja juu ni swala la muda tu.

Sio kwamba wamesahau wao bado wanakumbuka na kujua africa kunamali na wanaamini ipo siku watakuja na kukaa kabisa leo ugonjwa unazuka na wana weka takwimu kubwa za vifo africa hata kabla haija tokea je hii ni sawa machoni kwenu?

Hebu amkeni tufikirie hakuna atakae kuja na kuikomboa africa na tusipo angalia tutajikuta kila nchi ya africa itaanza vita vya ndani wenyewe kwa wenyewe na kukimbilia ulaya wao wata anza kujenga tena africa na tukija tunakuwa wageni angalieni sana

Kama hawa watu walikuwa wavumilivu zaidi ya miaka elfu moja na wakafanikiwa kuangusha ufalme wa waafrika uliyokuwa unaongoza DUNIA unadhani hawatoweza kutupelekea magonjwa na vifo mpaka tukaisha ndani ya miaka mia tano au hata 200 tusipo makini ?

kama tunajenga nyumba africa tunagombania fito za nini sisi ni wa africa wazee waliweka mambo ya ukuu wa kijiji na hata wafalme au chifu je walibadilika na ulisikia hata ugombanishi katika historia

leo africa haina upendo leo africa hatuna umoja kama babu na bibi zetu leo africa tuna gawanywa na kutenganishwa

Usipo mmbagua mweusi mwenzako kwenye nchi itakuja kwenye ukanda ukimaliza mnakuja kwenye mkoa mkimaliza mnakuja kwenye ukabila ukimaliza kummbagua kwa ukabila utakuja uwezo wa hela na ukimaliza na kabila moja na mna kipato sawa utakuja kwenye dini huyu muislamu huyu mkristo mkiona hamja ridhika basi tuna uana kwenye uchama

Nadhani ifike wakati na tuwaze je tutafunguka lini kiakili africa na wananchi wake ikiwemo na Tanzania tupo brain washed sana inaumiza sana na kutesa akili tuamke wewe kijana wewe dada jua thamani yako kama muafrica jua ulicho nacho kuanzia mwilini mpaka kwenye udongo wako

tuwe na upendo sana kama waafrica tusiuane kisa chama au dini maana yote ilikuwa kama njia za kuendeleza ukoloni na utumikishwaji wa Sisi waafrica tuamke tusimame tuwe na upendo

niwatakie siku njema
 
Hao wazungu walivyoleta vyama vingi ndo walisema tuwauwe na kuwatesa , kuwafunga wapinzani wetu?, walisema tuibe kura waziwazi?. Shida tunajitakia sisi wenyewe, wala sio vyama vingi.
 
Acha kutetea mijitu miovu
sio kwamba tuna tetea uovu hapana ila tunatakiwa tutambue namna ya kwenda mbele leo kila mtu akileta chuki badala ya sera kwa bara la Africa inakuwa nini
 
Acha kutetea mijitu miovu
hata wazungu na nchi za bara la ulaya wanafanya mangapi kinyume na uhuru wa mtu uarabuni wameua waangapi,urusi China sasa leo Africa ina inuka na ni tishio wazungu wana tetemeka

amini ya kuwa hakuna demokrasia duniani ila kila mtu ana hofia kuamka kwa Africa wanajua hawato lamba kitu
africa iko very peacefully
 
Hao wazungu walivyoleta vyama vingi ndo walisema tuwauwe na kuwatesa , kuwafunga wapinzani wetu?, walisema tuibe kura waziwazi?. Shida tunajitakia sisi wenyewe, wala sio vyama vingi.
mzungu hajasema uue mtu akiua hilo ni kosa na hatukatai kama ni kweli amelifanya

Issue ni kwamba sisi waza wa Africa ni kwanini bado tunakuwa walinzi wa mifumo ya wazungu ?
Africa ikiwa inaanza kuamka angalia leo mauaji na vurugu zina anza tunaenda wapi?
 
Hao wazungu walivyoleta vyama vingi ndo walisema tuwauwe na kuwatesa , kuwafunga wapinzani wetu?, walisema tuibe kura waziwazi?. Shida tunajitakia sisi wenyewe, wala sio vyama vingi.
tatizo moja kwetu vijana tukishasoma mpaka chuo na kupata viwango mbalimbali vya elimu

tunageuka kuwa bullet proof wa maovu na mfumo wa kidhuluma wa watu wa magharibi ambao bila kujua na kwa kupandikizwa mawazo yao kwenye elimu yetu tuna geuka kuweka chimbuko na maendeleo yetu chini na kuwapa nafasi

hili tumeanguka
 
Hatuwezi kuwapa Nchi upinzani hata siku moja
lakini pia kwa upande wangu ni mfuasi wa mfumo mmoja nimebadilika na kuwa hivyo kutokana na kujaribu kuona na kusoma mbinu za hawa watu hawapendi Africa tuwe na umoja hawapendi Africa tuwe na maendeleo

kama wananchi hatuto wasapoti viongozi wetu wa Africa hawato weza pekee yao kuvuka vikwazo vyote hivyo vya nchi ya magharibi

yaani unatakiwa kama kupinga uzazi wa mpango wote tunakuwa na uelewa na tunashikamana maana vidonge na madawa yao yana madhara ila leo sisi tume aminishwa kwamba tutazaliana tukose hela za kulisha watoto

wakati wao agenda ni controlling Africa population isizidi maana rasilimali hawato zifaidi na nguvu kazi itakuwa kubwa

hebu tuwashike viongozi sahihi na wenye malengo mazuri

mzungu ana kutunza akiona unaenda na matakwa yaje ila akiona una kimbia mbali na unyonyaji lazima aanze propaganda kwa wananchi
 
sio kwamba tuna tetea uovu hapana ila tunatakiwa tutambue namna ya kwenda mbele leo kila mtu akilera chuki badala ya sera kwa bara la Africa inakuwa nini












kwahiyo kwenda mbele ni kuendelea kutawaliwa na madikteta wauaji?

Au kwenda mbele ni kuendelea kutawaliwa na chama kiloshatutawala miaka 60 lakini bado kimeshindwa kutuletea maendeleo na kinaendela kulizimisha kutawa?
 
Hatuwezi kuwapa Nchi upinzani hata siku moja
ubaya wa hizi propaganda zina anza mitandaoni na kubebwa pasipo kuchujwa na wananchi hasa vijana

nimeshakutana na vijana wengi wa vya ambavyo havipo kwenye uendeshaji wa nchi hapa Africa huwa tuna tabia na hurka ya kutaka tuu chana kiingie kwa kudhani tutakuwa na maisha bora na hela kwa haraka

leo hata hapa Tanzania wewe kijana mwenzangu umekosa nini mpaka sasa kufanya uwaze kupinga kila kitu

kuna mambo tunalishwa na hatujui tunalishwa nini ni aibu na hatari sana
 
Mkuu, ukipata muda soma mada yangu hii hapa.

ume elezea vizuri sana tatizo letu hatuelewi na hata wakiingia hawa tuna waita wapigania uhuru ndio kutakuwa na upigaji sana maana wao lazima warudishe gharama ndio mambo ya zimbabwe yataanza hapa wanaingia na wananchi wana choka

leo Tanzania hatuna hata miaka 60 ya maendeleo watu wamesha jaa tamaa ya hela na ni vijana tujenge nchi kwanza China walijitoa muhanga miaka ya 1960's mpaka 1990's wakawa imara wao waligundua mapema

sasa na sisi tungejua kujibana enzi hizo kama sasa tungekuwa wapi amini ikifika 2040 au kwenda 2050 Tanzania tukiwa hivi tuna kuwa super power Africa na tishio kwa wazungu soon

Na hawatopenda kuona hivyo maana tutavuruga mipango yao ya long term ya miaka mia kitu maana kila nchi ya Africa itainuka

Tumeshaanza kwenye lugha maana ukitaka uwe na nguvu ya ushawishi kazana watu wajue lugha yako unaona China anataka super power ya dunia leo kila nchi africa hata ulaya na America wameanzisha Chinese language hiyo ni target nzuri

Na leo africa inajaa na inaingia kumi na nane ya kutumia lugha ya kiswahili amini usiamini Tanzania inaenda kuamka na imeshakuwa tishio

Giant giraffe of Africa is waking up!
 
Yaani upo hapa kutetea kuondoa Demokrasia Africa turudishe authoritarianism?

Africans ni watu kama watu wengine wowote duniani,wanataka uhuru wa mawazo na kila kitu!

Upo hapa kutaka Waafrika wasiwe huru?

Hivi una akili wewe maiti?

Stop this nonsense kabisa!
hizi ni hoja kama hoja nyingine acha lugha chafu kwenye hoja kama unaona huwezi usichangie kabisa hiyo maiti unaitamka ya nini sehemu hizi

kama una hasira scroll nenda mada nyingine kila mtu yupo huru ila lugha chafu sipendelei tuheshimiane
 
Yaani upo hapa kutetea kuondoa Demokrasia Africa turudishe authoritarianism?

Africans ni watu kama watu wengine wowote duniani,wanataka uhuru wa mawazo na kila kitu!

Upo hapa kutaka Waafrika wasiwe huru?

Hivi una akili wewe maiti?

Stop this nonsense kabisa!
ila ngoja nijibu kwa part ya kuu hapo sijapenda lugha yako

hakuna mtu anae support ubabe Africa kama ulivyo andika tatizo kubwa ni kwamba viongozi wengi wa upinzani hata wa vyama tawala Africa wanataka madaraka kwa faida zao wenyewe na watu wanao wapambania na kuwa support kipindi cha kampeni

kuwa na demokrasia sio kubadilisha viongozi kama sisi waafrika tunavyo dhani leo niki kuuliza umekosa uhuru gani unaweza niambia?

kwamba bwana Rijali mimi naona sipo huru kwenye vitu moja mbili tatu ukiweza hapo sawa tutajua lakini pasipo hivyo itakuwa ni kufuata mkumbo wa maneno ya mtu tuu

leo mtu mmoja anataka kuaminisha kwamba Africa au Tanzania si salama ukisikiliza kila nchi Africa uongozi wa kila nchi unalalamikiwa na wananchi

Je viongozi wote walioko madarakani Africa watoke ndio nchi za Africa zitakuwa huru?

Na kutakuwa na maendeleo ya kutosha?

Kikubwa ni kwamba wazungu wamejua kutumia divide and rule policy ndio maana mpaka leo Africa hatuwezi kuwa state moja maana wanajua kabisa kuna watu wao wanawalindia mfumo kwa kutumia kivuli cha uhuru wa kujieleza ambao je kwao upo?

Je kama kila nchi Africa ina lalamikia hakuna uhuru unaotolewa na viongozi kwahiyo bara la Africa viongozi wake walioko madarakani waachie nafasi ili kuwe na uhuru wa kujieleza chini ya wazungu au hao wana harakati wanadhaminiwa?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom