Kula matunda tu usiku ni formular ambayo haiko applicable kwa hapa kwetu Afrika

Inawezekana kabisa hujaamua tu as kila kitu kinahitaji mazoea so ungeendelea ungezoea
Mimi nilifika kg 93 ila diet ikanirudisha kg 70 ndani ya miezi 5. Usiku kula matunda, kipande cha samaki wa kuchemsha na glasi ya mtindi.

Ukisikia njaa kunywa mtindi nakuhakikishia utaona matokeo mazuri! Na ukitaka usinenepe zaidi badala ya ugali mchana kula mhogo au kiazi kutamu cha kuchemsha na veggies nyingi+samaki au nyama au dagaa, utapungua taratibu but ni very effective!

Siri haipo kwenye kushinda njaa bali kula mlo unaofaa!
 
mi ni mtu wa kula kula kila dakika, yani ikipita miwa nimo, wakipitisha azam ukwaju nipo, wakipitisha fenesi nipo, etc
Mkuu wewe upo kama mimi Ila tunachotofautiana mimi pamoja na kula kula kote mwili hauwi na uzito mkubwa nipo normal, nakula mpaka usiku yaani siwezi kucheck movie bila kula au kunywa chochote na usiku hata nikishtuka usingizini lazima nile chochote yaan sina formula kwenye suala la kula Ila mwili wangu sio mnene ni wa kawaida tu
 
Mkuu hii sio kweli 90% ya body fats inapungua kutokana na diet na 10% ni mazoezi. Hata upige mazoezi vipi kama ww ni bonge hutapunguza mafuta bali utajazia misuli (buff). Lakini kama lengo ni upate lean body ni lazima uzingatie diet na hii inahusisha kupunguza kabisa kula vyakula vya wanga...kupunguza kula junky foods...carbonated drinks...ongeza ulaji wa matunda...mbogamboga za majani...kunywa maji mengi matokeo utayapata. Kwahiyo vumilia tu matunda usiku inawezekana na utazoea
 
Anza kwanza kwa kupunguza kiasi unachokula taratibu taratibu mpaka mwisho ndio uache kabisa.
 
Nakula matunda usiku. Ila sio matunda haya yenye maji pekee.
Nakula ndizi
Parachichi
Maembe,
Usijidanganye ukala tikiti maji na machungwa halafu ulale mzee utashirikiana na sungusungu kulinda mtaa ukiwa kitandani.

Mimi sio mnene Ila sitaki kunenepa.

That's all.
 
Komaa mpaka siku ya 4 unakuwa poa tu, ila ndo utapungua mpk wakusahau niliifanya hii nilipungua kibongo bongo mwanamke kutokuwa na vinyama huvutii nimerudi kwenye mwili wangu
Kumbe inafanya kazi hii, na mimi sijui nijaribu
 
Kumbe inafanya kazi hii, na mimi sijui nijaribu
Ijaribu inasemekana chakula cha usiku ndo kinafanya mwili uongezeke kwa speed kwahiyo matunda mboga mboga ina menyu nzuri kwa usiku hunenepi
 
Ijaribu inasemekana chakula cha usiku ndo kinafanya mwili uongezeke kwa speed kwahiyo matunda mboga mboga ina menyu nzuri kwa usiku hunenepi
Mimi tayari ni mnene nataka kupungua
 
Pole sana kwa uzito huo mkuu, pambana ushuke usikaribishe maradhi
 
Aah njaa ya usiku inauma vibaya nyie! Matunda jau
 
Utakuwa umejichanganya mimi nazingatia vyakula toka kukua kwangu pamoja na mazoezi nafanya maana nacheza mpira haswaa tena mpaka ligi za vijana za ndondo nikiwepo Chuga nacheza kwa hiyo hilo tatizo sina matunda na mbogamboga ni sehemu yangu ya maisha.

Muda mwingine naenda Samunge asubuhi kujaza hizo na matunda pamoja na nyanya.. Ukipunguza kula red meat hizo mambo utazisikia tuu ingawaje napenda maziwa ya mgando haya yanaongeza mwili sana...
 
Usiku kula chakula, lakini by 75% yawe matunda na glass ya maziwa / ndio principle yetu Ulaya.
 
Kuna mambo mengi hawa watu wa lishe wanayaruka na ndio sababu masomo yao hayafanikiwi
Mf: Hatua gani za kupitia hadi kufikia kula matunda pekee usiku

1. Hali ya hewa ya eneo husika (kuna hali inaongeza metabolic process)
2. Aina ya Kazi mtu anayofanya
3. Aina ya chakula mtu anachotakiwa kula asubuhi na mchana (na uwezo wake wa kukipata)
4. Utaratibu wa kufuata hadi mtu aweze kula hayo matunda pekee
5. Ufanyaji wa mazoezi (yapi na kwa kiasi gani, sio kunyanyua chuma kama mtu anajiandaa na world cup)

Kibongo bongo unaambiwa tu, mimi nakula matunda au flani anakula matunda ila ukifuatilia kwa makini wanakula kama adhabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…