Kula matunda tu usiku ni formular ambayo haiko applicable kwa hapa kwetu Afrika

Kula matunda tu usiku ni formular ambayo haiko applicable kwa hapa kwetu Afrika

Mambo mengine tuwaachie wenyewe..

Mimi nikajaribu kuangalia movie huku nakunywa juisi, movie haijafika popote, dumu la lita 1.6 lishaisha.. 😂
😂😂Mimi popcorn aisee kabla giza haijaingia zimeisha zote mfuko wa mahind wa nusu kilo ni siku mbili😂😂😂
 
Unene wa wengi husababishwa na chakula.

Yaani wanene wengi wanakula sana.

Kumdiet mtu mnene mpaka umlazimishe, hawezi kujinyima kwa hiari.

Nilikuwa na jamaa yangu anafuta ndoo nzima ya ubeche, kreti la soda, galoni la maziwa na mkungu wa ndizi peke yake na alikuwa bonge la jitu limepanda hewani hasa!

Sasa mtu kama huyo utamdanganyia viparachichi viwili alale!

Kama ulivyosema dieting ni kwa wazungu tu huko!
Hahahaha umeongeza chumvi mkuu ,mtu gani anayeweza kumaliza ndoo nzima ya ubeche? Mkungu mzima wa ndizi? Kreti nzima ya soda? Huyo siyo mtu ni JINI.
 
Umepungua!?na ni matunda gani huwa unakula
Nakula matunda aina yoyote ninayopata. Mfano jana nimekula embe dodo. Nikanywa na kahawa kwa karanga.
Huwa najitahidi uzito usizidi kg 65. Wiki iliyopita nilipima nilikuwa na 61. Kwa urefu nilinao wa cm 165 huo uzito uko sawa.
Lakini pia nafanya mazoezi. Napendelea zaidi jogging na kutembea.

Nikiwa nipo Karume au Kariakoo na nina shida ya kwenda maeneo ya Posta au nipo Posta nahitaji kwenda Kariakoo, na kama sina haraka na jua si kali sana huwa natembea kwa miguu. Kama ni jioni/alfajiri huwa sijiulizi kabisa kuhusu kutembea kwa miguu.
 
Nilihudhuria darasa flani la mambo ya afya coz niliona mwili wangu umekua mkubwa mno so nilitaka darasa la namna ya kupunguza, moja ya masomo ilikuwa ni kula matunda tu usiku.

Nimejaribu jana ila leo nimeshindwa, nimekula matunda saa 1 na nusu nikapanda bed kulala ila sasa hivi saa 3 naskia nenge ya ajabu, imebidi niingie jikoni kurusha nguna tu.

Nadhani hii formula ya matunda tu usiku kwa sisi waafrika haiko applicable kabisa, tuwaachie wazungu tu.
Acha uroho wewe...
 
Unabidi kula chakula kutokana na kazi unafanya mfano mtu, anafanya Kazi Ofisini then anakula Kama mbeba zege

Mimi nakunywa chai kikombe 1
Andazi 2

Mchana maji lita 2 na upawa mmoja wa wali

Usiku chapati nne na maziwa nusu lita

Lakini by that time nafanya Kazi ngumu nilikuwa nakula robo tatu ya unga siku nzima

Nina kilo 60 na sitaki ziongezeke that. Enough
 
Mimi kwangu sio matunda tu ata nikila chips mayai au kavu sipati usingizi kwa njaa.
 
Hahahaha umeongeza chumvi mkuu ,mtu gani anayeweza kumaliza ndoo nzima ya ubeche? Mkungu mzima wa ndizi? Kreti nzima ya soda? Huyo siyo mtu ni JINI.
Nishaeleza, siyo mmoja tu aliyekuwa na sifa hizo za ulaji wa kustaajaisha! , ni wengi tu enzi hizo michezo(body builders) ikithaminiwa na Taifa.

Kulikuwa na power Mabula na power Mwamgiga, power Mwanakulya niliowafahamu na wengineo wengi.

Huyu power Mabula tulisongeshwa naye vitani akitokea Tank battalion Arusha.

Nilienda kumjulia huko kwa maajabu aliyoonesha mstari wa mbele!

Mojawapo ya miujiza yake ni pamoja na kufyatua mzinga wa kifaru, bomu lake likaenda kuingia kwenye mtutu wa mzinga wa kifaru cha adui na kukisambaratisha!

Jambo hilo ni gumu sana, hadi tuliamini kuwa anatumia juju.

Chakula tunachokulaga vitani kinaitwa "scale 2", lakini yeye alikuwa anakula "special diet" hakipimwi kwenye mizani, ni kama watu wa "game" wanavyohudumia simba wao wa kufugwa!
Ni kula hasa, unajua kula!
 
Fanyeni mazoezi acheni kujitafutia vidonda vya tumbo!
[emoji1492][emoji1492]
 
Kwenye friji ukiweka juisi au soda kila saa kikoo kiawwasha washa😂
Sisi sote tunaoongea humu yawezekana tuna afya njema.

Huyu mtoa mada nadhani alishauriwa vinginevyo na madaktari.

Haiwezekani mtu hauumwi ama kusumbuliwa na dalili zozote mbaya za kiafya, ukaanza kujishuku na kuanza kubagua vyakula!

Magonjwa mengi tunayoyahofia sisi wachakarikaji, huwa kuyapata siyo rahisi, hayo ni magonjwa ya mapadre wanaotumikiwa pamoja na maofisa wa serikali waliobweteka hadi milango yao ya magari kufunguliwa na watu wengine!

Na ubongo wa binadamu ulivyo, hofu yako inaweza kujenga uhalisia na baadaye ukaingia kwenye migogoro ya ki afya ya kudumu maisha yako yote!
 
Kutembea ni zoezi zuri sana, kula sana tembea sana 😂😂
 
Nilihudhuria darasa flani la mambo ya afya coz niliona mwili wangu umekua mkubwa mno so nilitaka darasa la namna ya kupunguza, moja ya masomo ilikuwa ni kula matunda tu usiku.

Nimejaribu jana ila leo nimeshindwa, nimekula matunda saa 1 na nusu nikapanda bed kulala ila sasa hivi saa 3 naskia nenge ya ajabu, imebidi niingie jikoni kurusha nguna tu.

Nadhani hii formula ya matunda tu usiku kwa sisi waafrika haiko applicable kabisa, tuwaachie wazungu tu.

Haiwezekani kwako, ila tafakari sana kifo cha kizembe hutasikia njaa
 
Nilihudhuria darasa flani la mambo ya afya coz niliona mwili wangu umekua mkubwa mno so nilitaka darasa la namna ya kupunguza, moja ya masomo ilikuwa ni kula matunda tu usiku.

Nimejaribu jana ila leo nimeshindwa, nimekula matunda saa 1 na nusu nikapanda bed kulala ila sasa hivi saa 3 naskia nenge ya ajabu, imebidi niingie jikoni kurusha nguna tu.

Nadhani hii formula ya matunda tu usiku kwa sisi waafrika haiko applicable kabisa, tuwaachie wazungu tu.
Soma kitabu Cha sayansi ya mapishi Cha Dr Boaz mkumbo hutajuta ukiyatekeleza yaliyomo
 
inategemea,kwa mfano leo nimepiga biriani moja matata sana mpaka sahivi sina mpango tena wa kula.ukila vizuri mchana unaweza kulalia matunda.
Ila pia inategemea na shuhuri zako za kutwa, zinatumia nguvu kiasi gani.

Ninachopingana na wataalamu wa afya, ni pale wanapotoa suluhisho la milo fulani kwa watu wote, bila kujali kazi zao za kila siku.
Mtu kutwa mzima anapiga tofari, alafu jioni umwambie ale papai alale, wakati anaesema hivyo anafanyia kazi kwenye kitu kinachotembea, mchana wali kuku, pembeni chupa ya kahawa, maziwa na juis.
Akitoka pale tusile sana jioni, anasahau watu waliwengi hawali bali huondoa njaa.
 
Back
Top Bottom