Kuliko kuajiri mfanyakazi wa ndani tuwe na utaratibu wa kuchukua watoto wa ndugu kwa nia ya kuwaendeleza

Kuna kabila moja kule Kaskazini wanaiweza hii. Wao wana focus na maisha yake yajayo. Anaishi kwa baba mdogo ambae ana grocery. Asubuhi anawahi kufungua duka tena kukaa dukani ndiyo faraja yake.

Baada ya muda na yeye anaweka galloni zake za mafuta ya kula, anakusanya mtaji mpaka ukikaa fresh anakuaga.
 
Uzoefu wangu: watoto wa ndugu (baadhi) ni shida sana. Akitumwa kazi hakawii kupiga simu kwao kudai anateswa sana

Bora umsaidie kivingine tu ila linapokuja suala la kazi/usaidizi kuwe na options nyingine
Imenigusa sana penyewe member, wengi sio watulivu halafu wana mdomo sana kila kitu cha maisha yenu kinaenda kwa ndugu. Hata mfanyie mazuri mangapi atalalamika kuteswa, kuonewa, na kutumikishwa tofauti na watoto wako na ndugu zako watamuamini. Hawata kwambia na utakuwa na uhusiano mbaya nao. Mimi nasaidia yoyote anayejitambua.
 
Hii sio mbaya, hawa watu wana umoja kama wapopo na ndio maana wanafanikiwa! Huwa anamuweka mtoto wa ndugu dukani ajifunze business!

Akishaelewa anajua namna atabalansi apige pige magenji mpaka aanzishe cha kwake na wao huwa hawajali as long as haiui biashara! This kind of achievements inaimarisha undugu zaidi kuliko style ya kumnyanyasa mtu eti kisa unamlipia ada ya laki 3.
 
Asante ndugu mleta mada kwa mawazo +.

Ingawa katika jamii yetu kuishi na ndugu Ni mtihani kidogo tena ndugu hawa ambao wanadhani maisha kila siku ni mteremko, ila ni bora zaidi kwani kwa mbali tunakua tunapunguza mdogo mdogo mnyororo wa umaskini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutumwa kazi hakuna uhusiano na kuteswa ila kama mtajiondoa by 100% kwenye hizo kazi sababu yeye tu yupo lazma alalamike! Haiwezekani watoto wa rika lake wapo wanaangalia igizo halafu umnyanyue yeye akalishie kuku. Kazi wafanye collectively wakwake na wako halafu uone kama atalalamika.

Msaidiane kazi sio mumpe mikazi yote kwa vile mnamsaidia kumsomesha!
 
Binadamu ni social animals, tunajifunza kupitia socialisation. Unamtoa mtoto kijijini muekee utaratibu wa jinsi atavyo ku address , mfundishe rotine za nyumba taratibu.

Kama mnakula wote mezani ajue table manners, mpange kabisa hela yake ya matumizi madogo anaipata kwa mwezi au kwa wiki.

Na wewe usiwe mshenzi mshenzi. Usimamie unachopanga. Siyo inafika mwisho wa mwezi unasema huna hela, au umeshindwa kulipa ada yake ya driving school.
 
Changamoto ni wake zetu huwa ni wagumu kukubali kukaa na ndugu wa mwanaume,unakuta kwao mwanamke hakuna tegemezi.
Yeye anataka mkae na binti wa kazi tuu
 
Uzoefu wangu: watoto wa ndugu (baadhi) ni shida sana. Akitumwa kazi hakawii kupiga simu kwao kudai anateswa sana

Bora umsaidie kivingine tu ila linapokuja suala la kazi/usaidizi kuwe na options nyingine
Sababu hamna usawa lazma alalamike! Unapomtuma kazi jaribu kutengeneza balance aidha asaidiane na mkeo au asaidiane na wanao unless ni kumtuma dukani! Vinginevyoa atajiskia vibaya tu its usual.
 
Kwangu ni ngumu. Watoto bado ni wadogo hawawezi kufanya majukumu collectively. In doing so vitu vingi ata deal nanvyo maana hataweza kufanya majukumu sawa na sisi walezi wake hivyo hana namna nyingine atapiga tuu kazi akishindwa safari njema.
 
Yeah yeah, kuishi na mtu ukiwa na upendo hawezi kuji feel vibaya hata siku moja as long as anajua una upendo genuine! Hata ukimpa maagizo atatekeleza kwa roho moja sababu anajua rafiki yangu huyu anantuma na anaipendaga sana. Hawezi ona anaonewa ila kuna watu ni wanyanyasaji tu hata kwa kauli yani, dont make someone feel like unamfanyia favour kumlipia ada so he/she has to suffer for that! It makes no sense na uswahili kama huo ndio hautakiwi umemchukua mtu unasema unamsomesha driving amekuja anakaa miezi anasafisha mabanda ya mbwa tu na kulimia bustani anaosha magari akiuliza vipi huna hela..Nobody wants that huo uswahili aki complain kwao utasema dogo mbaya! Huo ni uswahili!
 
Changamoto ni wake zetu huwa ni wagumu kukubali kukaa na ndugu wa mwanaume,unakuta kwao mwanamke hakuna tegemezi.
Yeye anataka mkae na binti wa kazi tuu
Ninaifahamu familia moja, jamaa alikutana na mke wake chuo kikuu. Wote walikua na kazi super. Sasa dada wa jamaa ana watoto nane baba tofauti. Wote wako nyumbani kwa wazazi.

Aliamua kuwachukua wakubwa. Wale watoto walipofika ndipo Mrs alipokua fundi cherahani. Anawashonea maroronya wakati watoto wake wanavaa nguo za Uturuki. Ukiingia tu ndani ya nyumba unaona tofauti.

Lakini wale mabinti walifanikiwa mmoja alisoma nursing mwingine uwalimu. Sasa hivi wote wanakitegemea na wanamsaidia mama yao.
 
Wazo ni zuri, hasa ndugu huyo akiwa anajielewa ila asipojielewa tabu itakua kubwa mno.
Ndugu anaejielewa yupoje na asiyejielewa yupoje? Kwani ndugu anakuwa hajui purpose yake ya kuja hapo ama mnakuwa hamjawaweka wazi anapotoka huko anabebwa kama kiroba?
 
Haya ndio mie nayapinga haswa..,kuna watu wavumilivu kama watoto wa kike watakausha ila sasa wakishaondoka hapo uhusiano umekwisha hutaona wakikanyaga tena hio nyumba! Mjomba wao wataonana nae misibani na kwenye harusi za watu.

Huo ni ushenzi na wanawake wengi ndio wana tabia hii kwa ndugu wa mume!
 
Ndugu anaejielewa yupoje na asiyejielewa yupoje? Kwani ndugu anakuwa hajui purpose yake ya kuja hapo ama mnakuwa hamjawaweka wazi anapotoka huko anabebwa kama kiroba?
Kuna mtu hata akifaamishwa lengo bado haelewi, awe ndugu au asie ndugu.
Asie ndugu umaweza mwambia nitakulipa na bado nitakusomesha mfno chereheni na asielewe na ndugu pia unaweza mwambia haya na asielewe.
 
Kuna mtu hata akifaamishwa lengo bado haelewi, awe ndugu au asie ndugu.
Asie ndugu umaweza mwambia nitakulipa na bado nitakusomesha mfno chereheni na asielewe na ndugu pia unaweza mwambia haya na asielewe.
Ambaye haelewi mnamuacha tu dunia itamfunza! Hamna haja ya kulumbana nae, nilimlipia ada akashindwa mwenyewe shule. Wala haina sababu ya kupigizana nae sana kelele.
 
Ambaye haelewi mnamuacha tu dunia itamfunza! Hamna haja ya kulumbana nae, nilimlipia ada akashindwa mwenyewe shule. Wala haina sababu ya kupigizana nae sana kelele.
Unamuacha lkn roho inauma. Kuna mtoto wa mama yangu mdg ambae ni marehemu alipata chuo sasa sababu mzee wake hajali nikamwambia awe anakuja kwangu kula sababu chuo na kwangu sio mbali. Ikawa jion akija anakula nami nampa 5000 kila siku ya mambo madg mdg llakini lawama ninazozipata huko mkoani hadi nashinwa kuelewa anataka nini. Maana nyumbani kila siku naambiwa ulilelewa wewe lkn hutaki kuangalia wenzio
 
Hahahahah sasa umuangalieje kama anakula na kiinua mgongo anapata daily!πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… mwambie bandogo aache uchizi. Well, hopefully humsimangi simangi tu maana misaada ya masimango inakera!

Chuo mtu hasimamiwi anajisimamia mwenyewe.
 
Binadamu wengi hatufahamu jinsi ya kubadilisha negative situation into positive one. Hawa mabinti faraja waliipata shuleni na huko ndiko waliko kazia.

Kuna mwalimu wangu mmoja alinisimulia matatizo aliyoyapata ugenini. Baba yake alihamishwa kikazi na yeye ilibidi ahamie na kusoma kule. Kwakua lafudhi yake ilikua tofauti, akiongea watoto wenzake walimcheka darasani. Aliamua kufa na kitabu ndiyo ilikua faraja yake. Matokeo yake alikua wa kwanza darasani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…