Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 70,785
- 186,690
So unakuwa nao wawili? Beki tatu na ndugu yako?Huwa siachi kukaa na ndugu ila ndugu napendelea jinisia Ke na msichana wa kazi hii njia imenisaidia sana kudumu na wasichana wa kazi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
So unakuwa nao wawili? Beki tatu na ndugu yako?Huwa siachi kukaa na ndugu ila ndugu napendelea jinisia Ke na msichana wa kazi hii njia imenisaidia sana kudumu na wasichana wa kazi.
Kuna kabila moja kule Kaskazini wanaiweza hii. Wao wana focus na maisha yake yajayo. Anaishi kwa baba mdogo ambae ana grocery. Asubuhi anawahi kufungua duka tena kukaa dukani ndiyo faraja yake.Wazo zuri hili ila sio kila mtu anaweza kuishi na mtoto wa mwenzie kwa usawa bila ubaguzi. Kuna wamama wengine mna ubaguzi wa dhahiri kabisa inapelekea kumtia mtu uchungu na kujuta hata kuwafahamu.
Nia ni njema ila inapofikia watoto wako wanakuwa of more concern kuliko yeye inafikia stage unamfanya kama kijakazi huo unakuwa sio msaada tena bali ni kumfanya mtumwa! Kumgeuza mtoto wa kaka yako mtumwa its the worst form of relationship you can ever thought of creating.
Wengine tumekulia mazingira hayo watoto wa nyumba hio wao wanakula cakes na mayai asubuhi nyie mnakula magimbi. Wanalia sahani nyie mnapigwa kwenye sinia chini! Nyama za baba tu japo baba kanunulia familia nzima ile ila anapikiwa yeye na wanae nyie mwendo wa kabichi na maharage tu. Siku za shopping ya vyakula watoto wake wananunuliwa chocolates na pringles wanalia chumbani na kupangusa midomo mtakutana na maganda tu. Alfajiri uamke ufagie kiwanja na banda la mbuzi kisha unaenda shule hata chai hujanywa hupewi hata sh.100 utembee wao wanapandishwa school bus na buku ya kuspend on break time hapo washakula cakes, mayai na chai asubuhi! I don’t wanna remember that life aisee...Siwezi ruhusu mtoto wa mtu apitie ile hali akiwa kwangu! I rather not take him/her.
Imenigusa sana penyewe member, wengi sio watulivu halafu wana mdomo sana kila kitu cha maisha yenu kinaenda kwa ndugu. Hata mfanyie mazuri mangapi atalalamika kuteswa, kuonewa, na kutumikishwa tofauti na watoto wako na ndugu zako watamuamini. Hawata kwambia na utakuwa na uhusiano mbaya nao. Mimi nasaidia yoyote anayejitambua.Uzoefu wangu: watoto wa ndugu (baadhi) ni shida sana. Akitumwa kazi hakawii kupiga simu kwao kudai anateswa sana
Bora umsaidie kivingine tu ila linapokuja suala la kazi/usaidizi kuwe na options nyingine
Hii sio mbaya, hawa watu wana umoja kama wapopo na ndio maana wanafanikiwa! Huwa anamuweka mtoto wa ndugu dukani ajifunze business!Kuna kabila moja kule Kaskazini wanaiweza hii. Wao wana focus na maisha yake yajayo. Anaishi kwa baba mdogo ambae ana grocery. Asubuhi anawahi kufungua duka tena kukaa dukani ndiyo faraja yake.
Baada ya muda na yeye anaweka galloni zake za mafuta ya kula, anakusanya mtaji mpaka ukikaa fresh anakuaga.
Kutumwa kazi hakuna uhusiano na kuteswa ila kama mtajiondoa by 100% kwenye hizo kazi sababu yeye tu yupo lazma alalamike! Haiwezekani watoto wa rika lake wapo wanaangalia igizo halafu umnyanyue yeye akalishie kuku. Kazi wafanye collectively wakwake na wako halafu uone kama atalalamika.Imenigusa sana penyewe member, wengi sio watulivu halafu wana mdomo sana kila kitu cha maisha yenu kinaenda kwa ndugu. Hata mfanyie mazuri mangapi atalalamika kuteswa, kuonewa, na kutumikishwa tofauti na watoto wako na ndugu zako watamuamini. Hawata kwambia na utakuwa na uhusiano mbaya nao. Mimi nasaidia yoyote anayejitambua.
Binadamu ni social animals, tunajifunza kupitia socialisation. Unamtoa mtoto kijijini muekee utaratibu wa jinsi atavyo ku address , mfundishe rotine za nyumba taratibu.Achana na habari za kum control! Ukimsaidia mtu mwache free afanye anachopenda you guys mnafeli hapa...Unapomsaidia mtu usimuhenyeshe maana ile mantiki ya msaada inakuwa haipo kabisa na wala hizo thawabu unazozitaka hutazipata! Assist someone with a clean heart. Sio ndio umfanyishe makazi kama punda na kumkosesha amani!
Kuna watu wanakaa na watoto wa wenzao yani mtoto hawezi juta kuishi hapo sababu wote wanapata fair treatment! Sio mtoto wako shopping Mlimani wa mwenzio unampa hela aende Ilala Boma akanunue mtumba! Haya ndio mambo ya hovyo
Changamoto ni wake zetu huwa ni wagumu kukubali kukaa na ndugu wa mwanaume,unakuta kwao mwanamke hakuna tegemezi.Unakaa na mtoto kwa mkataba wa kumsomesha au kumuendeleza. Mnapanga muda wake wa kwenda shuleni au mafunzoni na muda wake wa kazi. Anaishi kama mtoto wa nyumbani, unamnunulia mahitaji yake madogo madogo. Sehemu kubwa ya mshahara unakwenda kulipia ada na Bima ya afya.
Akihitimu mafunzo unamuwezesha kujitegemea na unatafuta mwingine. Kama ndugu zako wote mambo safi unaweza kuchukua vijana wa kijijini kwenu. Hii ni njia ya kurudisha katika jamii na kukwamuana kimaisha.
Sababu hamna usawa lazma alalamike! Unapomtuma kazi jaribu kutengeneza balance aidha asaidiane na mkeo au asaidiane na wanao unless ni kumtuma dukani! Vinginevyoa atajiskia vibaya tu its usual.Uzoefu wangu: watoto wa ndugu (baadhi) ni shida sana. Akitumwa kazi hakawii kupiga simu kwao kudai anateswa sana
Bora umsaidie kivingine tu ila linapokuja suala la kazi/usaidizi kuwe na options nyingine
Kwangu ni ngumu. Watoto bado ni wadogo hawawezi kufanya majukumu collectively. In doing so vitu vingi ata deal nanvyo maana hataweza kufanya majukumu sawa na sisi walezi wake hivyo hana namna nyingine atapiga tuu kazi akishindwa safari njema.Kutumwa kazi hakuna uhusiano na kuteswa ila kama mtajiondoa by 100% kwenye hizo kazi sababu yeye tu yupo lazma alalamike! Haiwezekani watoto wa rika lake wapo wanaangalia igizo halafu umnyanyue yeye akalishie kuku. Kazi wafanye collectively wakwake na wako halafu uone kama atalalamika.
Msaidiane kazi sio mumpe mikazi yote kwa vile mnamsaidia kumsomesha!
Yeah yeah, kuishi na mtu ukiwa na upendo hawezi kuji feel vibaya hata siku moja as long as anajua una upendo genuine! Hata ukimpa maagizo atatekeleza kwa roho moja sababu anajua rafiki yangu huyu anantuma na anaipendaga sana. Hawezi ona anaonewa ila kuna watu ni wanyanyasaji tu hata kwa kauli yani, dont make someone feel like unamfanyia favour kumlipia ada so he/she has to suffer for that! It makes no sense na uswahili kama huo ndio hautakiwi umemchukua mtu unasema unamsomesha driving amekuja anakaa miezi anasafisha mabanda ya mbwa tu na kulimia bustani anaosha magari akiuliza vipi huna hela..Nobody wants that huo uswahili aki complain kwao utasema dogo mbaya! Huo ni uswahili!Binadamu ni social animals, tunajifunza kupitia socialisation. Unamtoa mtoto kijijini muekee utaratibu wa jinsi atavyo ku adress, mfundishe rotine za nyumba taratibu.
Kama mnakula wote mezani ajue table manners, mpange kabisa hela yake ya matumizi madogo anaipata kwa mwezi au kwa wiki.
Na wewe usiwe mshenzi mshenzi. Usimamie unachopanga. Siyo inafika mwisho wa mwezi unasema huna hela, au umeshindwa kulipa ada yake ya driving school.
Ninaifahamu familia moja, jamaa alikutana na mke wake chuo kikuu. Wote walikua na kazi super. Sasa dada wa jamaa ana watoto nane baba tofauti. Wote wako nyumbani kwa wazazi.Changamoto ni wake zetu huwa ni wagumu kukubali kukaa na ndugu wa mwanaume,unakuta kwao mwanamke hakuna tegemezi.
Yeye anataka mkae na binti wa kazi tuu
Ndugu anaejielewa yupoje na asiyejielewa yupoje? Kwani ndugu anakuwa hajui purpose yake ya kuja hapo ama mnakuwa hamjawaweka wazi anapotoka huko anabebwa kama kiroba?Wazo ni zuri, hasa ndugu huyo akiwa anajielewa ila asipojielewa tabu itakua kubwa mno.
Haya ndio mie nayapinga haswa..,kuna watu wavumilivu kama watoto wa kike watakausha ila sasa wakishaondoka hapo uhusiano umekwisha hutaona wakikanyaga tena hio nyumba! Mjomba wao wataonana nae misibani na kwenye harusi za watu.Ninaifahamu familia moja, jamaa alikutana na mke wake chuo kikuu. Wote walikua na kazi super. Sasa dada wa jamaa ana watoto nane baba tofauti. Wote wako nyumbani kwa wazazi.
Aliamua kuwachukua wakubwa. Wale watoto walipofika ndipo Mrs alipokua fundi cherahani. Anawashonea maroronya wakati watoto wake wanavaa nguo za Uturuki. Ukiingia tu ndani ya nyumba unaona tofauti.
Lakini wale mabinti walifanikiwa mmoja alisoma nursing mwingine uwalimu. Sasa hivi wote wanakitegemea na wanamsaidia mama yao.
Kuna mtu hata akifaamishwa lengo bado haelewi, awe ndugu au asie ndugu.Ndugu anaejielewa yupoje na asiyejielewa yupoje? Kwani ndugu anakuwa hajui purpose yake ya kuja hapo ama mnakuwa hamjawaweka wazi anapotoka huko anabebwa kama kiroba?
Ambaye haelewi mnamuacha tu dunia itamfunza! Hamna haja ya kulumbana nae, nilimlipia ada akashindwa mwenyewe shule. Wala haina sababu ya kupigizana nae sana kelele.Kuna mtu hata akifaamishwa lengo bado haelewi, awe ndugu au asie ndugu.
Asie ndugu umaweza mwambia nitakulipa na bado nitakusomesha mfno chereheni na asielewe na ndugu pia unaweza mwambia haya na asielewe.
Unamuacha lkn roho inauma. Kuna mtoto wa mama yangu mdg ambae ni marehemu alipata chuo sasa sababu mzee wake hajali nikamwambia awe anakuja kwangu kula sababu chuo na kwangu sio mbali. Ikawa jion akija anakula nami nampa 5000 kila siku ya mambo madg mdg llakini lawama ninazozipata huko mkoani hadi nashinwa kuelewa anataka nini. Maana nyumbani kila siku naambiwa ulilelewa wewe lkn hutaki kuangalia wenzioAmbaye haelewi mnamuacha tu dunia itamfunza! Hamna haja ya kulumbana nae, nilimlipia ada akashindwa mwenyewe shule. Wala haina sababu ya kupigizana nae sana kelele.
Hahahahah sasa umuangalieje kama anakula na kiinua mgongo anapata daily!😅😅😅 mwambie bandogo aache uchizi. Well, hopefully humsimangi simangi tu maana misaada ya masimango inakera!Unamuacha lkn roho inauma. Kuna mtoto wa mama yangu mdg ambae ni marehemu alipata chuo sasa sababu mzee wake hajali nikamwambia awe anakuja kwangu kula sababu chuo na kwangu sio mbali. Ikawa jion akija anakula nami nampa 5000 kila siku ya mambo madg mdg llakini lawama ninazozipata huko mkoani hadi nashinwa kuelewa anataka nini. Maana nyumbani kila siku naambiwa ulilelewa wewe lkn hutaki kuangalia wenzio
Binadamu wengi hatufahamu jinsi ya kubadilisha negative situation into positive one. Hawa mabinti faraja waliipata shuleni na huko ndiko waliko kazia.Haya ndio mie nayapinga haswa..,kuna watu wavumilivu kama watoto wa kike watakausha ila sasa wakishaondoka hapo uhusiano umekwisha hutaona wakikanyaga tena hio nyumba! Mjomba wao wataonana nae misibani na kwenye harusi za watu.
Huo ni ushenzi na wanawake wengi ndio wana tabia hii kwa ndugu wa mume!