Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

yani hapo hata mtoto mdogo anaweza kuwatoa kijasho, sio kwa unene huo. Hapo hakuna mlinzi hapo ni makasha tuu. Mlinzi gani wa rais ananenepeana kizembe hivo kuliko rais wake.
Na mashaka na mafunzo yao, wajaribu kupitia walinzi wa raisi wa mataifa mengine huwezi kukuta wana vitambi na shingo nene kama za hawa wa kwetu, wasijisahau kwa majukumu walionayo kuwa mnene sio sifa.
 
Mimi ile kauli ya kwamba Watanzia mniombee imenishtua sana, pia sioni haja ya msafara kuwa na walinzi wengi kiasi kile wakati Tanzania haina historia ya ulipuzi kwa viongozi
Tutamuombea Rais wetu na mama wa Taifa maana kwa sasa ndio nembo ya Taifa na wote tunamuelekea yeye kwenye masuala ya Nchi.
 
Kama ni fani yao mbona kipindi kaenda Marekani hao hao unaowaita wabobezi walisahau majukumu yao hadi kushika simu ya raia na kusaidia kupiga picha, je kile kitendo ni sawa ama si sawa?
Unataka kuhukumu kazi ya PSU kwenye kile ki clip? Unajua pembeni kulikua na ulinzi wa aina gani? Walinzi wa rais hujiridhisha na usalama wa eneo hata kabla ya rais kufika.
 
acha kupotosha,hata jpm mbona alikuwa Mara kadhaa akisema MNIOMBEE!!??,mbona hukusema ni kundi flani linamuandama jpm,pumbavu ...,samia huenda kwa Sasa amegundua ikulu sio pa mchezo Panahitaji moyo wa chuma na ujasiri wa kutosha. huwezi kukosa maadui ,Wala huwez kukosa marafiki,lakini pia ikulu usimwamini mtu hata Kama ni mkeo au mumeo.muda wowote mtu wako wa karibu unayemwamini anaweza kuwa adui yako !!!
Kwa hiyo ukiwa na utitiri wa walinzi ndio utakuwa salama ikiwa hata mkeo humwamini?
Nini mantiki ya kuwaamini hao walinzi wakati nao ni watu vile vile?
 
Wamesema nchini kuna magaidi yawezekana ikawa ndiyo sababu mkuu, ila siku nimekaa na mzazi mmoja hivi aliuliza siku ya Nyerere day ( Chato) viongozi wote wakuu walitambulisha wenza wao ila first gentleman hakutambulishwa kwa nini? Sasa sijui ni uzembe wa mzee yule kutambua au vipi?
 
Kama yule aliyekua anasimama pembeni ya Magu,pindi tupo nae SAUT,alikuaga mwembamba sana! Lakini akaja futuka hadi akawa analala wakati mwingine akiwa kakaa pembeni ya Magu
Haonekani yupo wapi siku hizi, ama analinda kaburi la boss wake?
 
Pia kuna wale wenye mabunduki ya kivita warefu pua zao zimechongoka kama wanyarwanda, kuishi kwangu Tanzania sijawahi kuona watu warefu kama wale, je ni wa vitego pia ama ni kutoka nchi za jirani? Maana hata huku mtaani hawaonekani kabisa wale watu warefu wenye mabunduki ya kivita
Kagema again is roading.
 
Unataka kuhukumu kazi ya PSU kwenye kile ki clip? Unajua pembeni kulikua na ulinzi wa aina gani? Walinzi wa rais hujiridhisha na usalama wa eneo hata kabla ya rais kufika.
Kosa kwanini apokee simu ya raia na kupiga picha?
 
Kama yule aliyekua anasimama pembeni ya Magu,pindi tupo nae SAUT,alikuaga mwembamba sana! Lakini akaja futuka hadi akawa analala wakati mwingine akiwa kakaa pembeni ya Magu
Comment ya kijinga na ya kitoto!
Talk about issues not personalities.
 
Si mlisema ni wanyarwanda Jman kipindi cha mwenda zake , Leo bado wapo kwenye ulinzi
 
umetuambia zamani akiwa anaanza kukalia kiti hakuwa na ulinzi mkubwa ila sasa amekuwa na ulinzi mkubwa....nafikiri umeshajijibu hapo mwenyewe..... kwa kukusaidia, system ndio inaamua aina ulinzi kwa Rais aliyemadarakani kulingana na intelenjia yao sio kutufurahisha raia....
 
Back
Top Bottom