Kulikoni? Msafara wa Rais Samia kuwa na magari yote haya, pia ulinzi wake umeongezeka maradufu

Hili swali linawahusu TISS, na kwa bahati mbaya hawawezi kukujibu
Rais wa dunia ya tatu anahusika moja kwa moja katika maamuzi ya analindwa lindwaje na kubebwa bebwaje kwenye magari.... Labda Marekani ndio kuna protocol za kisheria na kitaasisi ziko vitabuni na zinafuatwa

Samia Suluhu anachojaribu kufanya ni kukazia uzito wa Urais wake ambao yeye mwenyewe anaamini na anasema wazi ni urais unaodharauliwa.

Ndio maana kila uchwao haishi kujishtukia na kujitetea, mara mimi Mzanzibar, mara mimi naongea kwa kalamu, mara oooh nilikuwa bado nawasoma, mara mimi sifoki foki, mara mimi mwanamke, mara mkinizingua ntawazingua, mara mimi ndio Amiri Jeshi Mkuu... empty rhetoric za mtu anaejijua anapwaya na anadharaulika, na juzi katamka mwenyewe viatu vya Magu havimtoshi....
 
Maskini watanzania wenyewe wa kumdhuru wako wapi dah.... Hela TU zinapigwa bila sababu. Watanzania huwa tunachukia TU na kuishia kunung'unika Moyoni
 
Jana akiwa Moshi nilishangaa sana kuona ule msafara na zile chopa mbili juu!

Lissu alisema ni mapema mno kumpa sifa Rais Samia! Sasa keshaonja utamu wa Urais,kwa hiyo na yeye anafanya tu atakavyo
Hakuna Rais asiye na ulinzi duniani au unataka apigwe vibao kama Emmanuel Macron
 
Kaka hawa watu unawachambua vilivyo ila all in all hakuna ulinzi wa uhakika kama ule kutoka kwa Mungu, sasa hao wanaokaa kwenye mapaa wana mtisha nani unakuta wana bunduki ilihali inatakiwa wasiwe identified kwa namna yoyote wawe na wametulia zao na binocular wana zoom watu katika angle tofouti wakiwa na snipers wao sasa hawa wetu wako tofouti labda mfumo wao ni tofouti na wa nchi nyingine
 
Hii habari haikuwa siri. Kwani unajaribu kuthibitisha nn kuhusu ulinzi wa JK? Maana unanipa tu evidence huku ukiniita mbishi.
 
Nimekupa link soma! Mbona unakua too much spoon feeding??? Kila kitu utafuniwe wewe umeze tu??
Umetaka Nisome ili nithibitishe nn kuhusu unayoyazungumza?

Kwamba JK hakuwa na ulinzi mkubwa ndo maana tairi likapasuka?

Au hakuwa na ulinzi ndo maana gia za gari hazikuingia?
 
Wadau Nawasalimu
Nimeushuhudia Msafara huu leo hakika nimeshangazwa sana na Uwingi wa Magari na Helkopta Angani.
Ombi kwa Wapangaji hebu Punguzeni idadi ya Magari na Hizi Helkopta kuokoa KODI za MASIKINI
TANZANIA NI NCHI MASIKINI NA WANANCHI WAKE
Your browser is not able to display this video.
 
Yale yale ya jiwe! afadhali ya Mkoloni
 
Watu wako madarakani kwa wizi wa kura unategemea nini? Unashangaa rais yuko kwenye nchi yake ana ulinzi kama kaingia kwa kupindua nchi. Lakini hivi majuzi kaonekana huko Marekani ambako hajapigiwa kura, yuko bila ulinzi wowote wa kutisha. Kwahiyo rais anaonyesha akiwa nje ambako hajachaguliwa yuko salama, kuliko hapa anaposema kachaguliwa kwa kura! Hapo wazungu wataacha kutuita manyani kweli?
 
Nyie huko msije mkapopoa mama kwa mawe na bado tunaongeza tatu.
Maana cha Arusha kipo huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…