Kumbe kubandika stika ya BIMA kwenye kioo cha gari ni lazima, hata kama umekata BIMA yako mtandaoni

Unafahamu kwamba TIRA ipo kisheria? Na maamuzi yake yanatambulika kisheria? , hilo la vifaa vya kuangalia haituhusu wenye magari, ni juu yao
 
Hizo hoja za busara tutajua huko huko mahakamani
sasa ukienda mahakamani mbona unapigwa kirahisii maana sheria inaelekezajeee? ka kunasheria mpya kuhusu namna ya kuweka bima iweke hapa tuone inasemaje?
 
Unaongelea sheria au kanuni
 
sasa ukienda mahakamani mbona unapigwa kirahisii maana sheria inaelekezajeee? ka kunasheria mpya kuhusu namna ya kuweka bima iweke hapa tuone inasemaje?
Mamlaka inayohusika na bima ni TIRA, ipo kisheria, sio kwa tamko; na wametoa tangazo kwa mujibu wa sheria juu ya kutotumia sticker, unataka sheria gani tena?
 
Unafahamu kwamba TIRA ipo kisheria? Na maamuzi yake yanatambulika kisheria? , hilo la vifaa vya kuangalia haituhusu wenye magari, ni

Unafahamu kwamba TIRA ipo kisheria? Na maamuzi yake yanatambulika kisheria? , hilo la vifaa vya kuangalia haituhusu wenye magari, ni juu yao
wapo kisheria sawa ila hapo ndo tunaita mgongano wa kisheria
 
Hiki kitu hakipo kwa sasa, huyu trafic kakuonea, stika sahizi hazibandikwi kwenye kioo kama zamaini, na hata watoa huduma hawatoi hzo stika
 
wapo kisheria sawa ila hapo ndo tunaita mgongano wa kisheria
Hakuna mgongano, sheria inasema wazi kwamba sheria na kanuni mpya hufunika za zamani, hata kama bado haijafutwa, sheria ipo hivyo na hakuna mgongano hapo; tutajua huko huko mahakamani, huniandikii faini ya kishezi hivyo
 
Mamlaka inayohusika na bima ni TIRA, ipo kisheria, sio kwa tamko; na wametoa tangazo kwa mujibu wa sheria juu ya kutotumia sticker, unataka sheria gani tena?
sheria ya usalama barabarani inakauli gani kuhusu sticker?
 
Mkuu sheria bado haijabadilishwa nadhani. Tena sheria sio inakutaka ubandike stika tu, inataka ubandike kioo cha mbele upande wa kushoto. Ukubandika pembeni hapo inategemea busara za askari. Ushauri wangu usilipe fine nenda kituoni kaonane na mkuu wa kituo au TIRA. Ukishindwa kufika piga hata simu watakupa maelekezo.
 
Mkuu askari alikagua BIMA kwa machine na kukuta gari kweli ilikua na bima
Tatizo ni kutokuibandika stika kwenye kioo, ni KOSA kisheria na lipo katika moja ya faini za magari kwenye zile machine walizonazo Traffic .!
Ungemuuliza stika ipi sasa?maana huko bima hawatoi hivyo vikaratasi vya kubandika au alitaka ubandike form ya malipo?
 
fact
 
je kunasheria mpya ya usalama barabarani?
Tofautisha sheria na kanuni zilizopo ndani ya sheria, hiyo kanuni ya sticker katika sheria ya usalama barabarani imeshafunikwa na agizo jipya toka kwa mamlaka ya kisheria inayosimamia hiyo kanuni, kwisha kazi. Mkijisikia kuiondoa ni vizuri zaidi ila ni obsolete kwa sasa, ni kama haipo tu. Na hiyo ndio sheria.
 
Hujui unachokitetea. Sheria ya bima haijabadilika ni lazima gari kukatiwa bima. Kanuni ndo huelekeza kubandika sticker kwenye kioo cha mbele cha gari upande wa kushoto. Waliotengeneza kanuni sio polisi wala bunge, kanuni zilitengenezwa na wasimamizi wa bima ambao kwa sasa ni TIRA na wameshatoa tangazo kuhusu kusitishwa kwa matumizi ya sticker za zamani na kuanza kutumika kwa e sticker kuanzia tarehe 01 april.
 
inawezekana sifahamu ila rejea kusoma sheria ya usalama barabarani
 
Wewe bado hujaelewa, hakuna Sheria inayokufa sababu ya kukua kwa technology
Ukitaka sheria ife basi ni lazima ifutwe, na hiyo Sheria bado ipo haijafutwa.
Umetoa mifano ya vitu ambavyo havihusiani, ungetolea mfano wa Sheria fulani kufa sababu ya technology
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…