Kumbe kuna watu wana PhD halafu wanalipwa laki 5?

Kumbe kuna watu wana PhD halafu wanalipwa laki 5?

kuna watu walikuwa hawana PHD walikuwa wanajilipa milion 40 kwa mwezi wakati wa mzee Jakaya . kuna mashirika wengi tu walikuwa wanachukua milion 25 na 30 ilikuwa vitu vya kawaida sana kodi za watanzania jamaa alipoingia akasema kiwango cha mwisho milion 15 hutaki ondoka huyu ndio Jpm.
 
Kuna uzi fulani ulikuwa unazungumzia mishahara ya wahadhiri wa chuo kuanzia kwa Tutorial Assistant hadi ngazi ya proffesor kuna jamaa mmoja alidadavua vizuri mno ukampa pongezi...

Unaweza nitag katika uzi husika tafadhali kipenzi..
Siukumbuki jina.
 
Aiseeh! hii imenipa faraja, sio kwa nia mbaya, maana nilikuwa najiona nina bahati mbaya nilipokuwa najiona nina kipato kidogo na nimechelewa kufikia malengo yangu

Rais kasema Kuna mtu kasoma miaka 4 China PhD na alikuwa akilipwa laki 5, japokuwa kateuliwa kuwa DC, lakini inamaanisha bado watu Kama Hawa wapo

View attachment 1508536
Wewe unadhani alivyoambiwa vile angebisha kwamba alikuwa halipwi hicho kiasi.. jiwe msanii sana hamjui tu.
Mtashuhudia kwa makonda, mnyeti nk watakavyopewa mashavu.
 
Kwa usanii hao jamaa hutawaweza.

Hio yote ni kukwambia shukuru kwa ulicho nacho huku nyie mlioko serikalini mkipewa ujumbe wa mnalalamika nini na vi diploma/degree zenu wkt huku Chamani kuna watu wana PH.d na wanalipwa laki 5 tu.
unalipwa laki5 lakini posho za vikao ni 3m na kuendelea
 
Hivi mnaijua PHD?? Au mnachangamsha genge na meko wenu?
kirefu chake kwan ni nn maana unajua 70% ya watz ni wakulima hatujui ebu tuelezeee kistaaaaaaarabu yani kistaaaarabu tu
 
PhD uchwara hiyo, alikuwa Makao Makuu CCM kwa kazi gani kama hajasomea utopolo?

Bila shaka ndo hawa vibwengo wanashinda mitandaoni kutetea chama.
kwani unadhani kazi yake hasa itakuwa ni nn kwani??maana kazi za chama mpaka uchaguzi na uchaguzi ni after 5 years
 
Inategemeana na PHD ya nini; Huenda jamaa Alisoma Masters na Phd Kwa sifa, Akachagua Kozi mbovu mbovu; Sasa ikawa ngumu kupata mahali; ikabidi Ajishikize Chamani.
nadhani kusema PHD tu haitoshi
Hapo umenena vyema. Ujira unaendana na uefanya au unafanya nini . Sasa mtu akiwa na PhD lakini kazi yake ni kukata tiketi za ushuru wa mabasi yaingiayo stendi ungependa alipwe milioni tano? Wakati mwingine hebu tuacheni ushabiki.
 
Duh PhD mshahara laki 5
Lakini inataegema hiyo PhD ni ya taaluma gani. Kuna taaluma zingine wenye sifa za PhD ni wengie na ni vigumu kupata kazi hivi hivi! Kwa fano, unaenda kuomba kazi ya uhadhiri , unakuta kozi hiyo ina wahadhiri wa kutosha. Pai pengin eni mfia Chama na alijua ipo siku atatoka akiwa hapo jikoni
 
Hizo nchi unazozitaja hazikusomesha tu ila walipeleka watu wao kusoma kimkakati. kwa mfano, mnapelekwa kusoma taaluma ya Medicine, na baada ya kuhitimu mnarudi kufanyakazi katika hspitali zenu. Na wanapelekwa vyuo vinavyoeleweka siyo vyuo vya daraja la chini. Kwa mfano, huwezi kufananisha mtu aliyesoma Muhimbili/ KCMC au Bugando na yule aliyesoma hicho IMTU au KIU
Elimu haina shida, attitude za watu ndio shida..! Elimu hii hii imesaidia nchi zilizokuwa masikini Kama Korea, Singapore zimekuwa modernized, iweje kwetu tu iwe shida?
 
Yule jamaa kipindi cha JK alikuwa anafanya kazi Ikulu, sasa akili kumkichwa ujue tunavyozugwa majukwaani

Mtaani kunaa vijana kibao wana certificate, degree, masters na PhD na hawana kazi hiyo laki 5 wanataman kuipata
 
Si bora angeenda kusajili laini za halotel voda tigo kuliko kuamka kila siku unachomekea eti unawahi laki 5 kwa mwezi hujatoa kodi ya nyumba nauli za kila siku kula na vocha hebu acheni kutufanya ma bogaz
 
Kuna ambao wana PhD na wamekaa nyumbani tu wanadeki na kuosha vyombo. Taifa linapoteza sana na ingekuwa vizuri kama rais akawaita akawapatia kazi.
Unaweza ukatupa mfano walau WA watu watano wenye PhD halafu wapo tu nyumbani ???.
 
Back
Top Bottom