Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Kuna ubaya gani hapo 4000x28 =112,000?
 
Kama huwezi kufanya huu ujinga kauze uduvi uolewe. Kwa sauti ya mkuu wa mkoa Chalamila 31.12.24
 
Huyo tunaweza kumpa udhuru ni mama lishe, lakini pia wafanyakazi wake wanakula hapo na wateja wengine wanaacha chenji au wanahonga. Mo kulipa kiwango sawa cha ujira na mama Lishe mdogo sio sawa hata kidogo.
Siko hapa kumtetea mo ndio maana nimeomba mleta Uzi anitajie kiwanda kinacholipa 20k kwa siku. Nenda kwa barmaids ujue wanalipwa kiasi gani? Kifupi mtaani hali ni mbaya.
 
Acha atajwe mzee, Ndio ni Mhindi kwa huo Ujira aisee hapo ni kutafuta Maximum profit tu punda afe mzigo ufike, Na ivo Viwanda vya Hao wahindi ni very risk mzee hata regulatory Bodies za Safety sijui zinafanya kazi gani mtu hajali safety ya wafanyakazi bado ujira ni duni,
Bado tunamchekea tu
 
Kama hao hawana kazi ya kuwapa hata mia ,na wana kula hapo hapo na wamaeneo ya karibu na hapo kiwandani hiyo 4000 sio tatizo kwa kazi za kiwandani ila kama ni tofauti na hivyo ukue ni. Utumwa
 
10,000 kwa siku.
Angalau buku moja kwa lisaa, sasa hivi ni kama analima 400 kwa lisaa! Mpiga debe anayipga debe kwa dakika 10 tu anapewa 500 na konda.

Na hapo gari zinapita nyingi najaribi kuwaza ni 500 ngapi wanaingiza wapiga debe. Afadhali kuliko kushindankwa Mo siku nzima!
 
Acha upumbavu wako huwezi kumuacha mtu awanyanyase ndugu zako eti kisa ametoa ajira nyingi huko ni kunyonya watu na kuwatumia kama watumwa.
Kwenye hili serikali inatakiwa kubeba lawama huwezi kuwaachia matajiri wajiamulie wanavyotaka kisa wanalipa kodi ni lazima utanzania uheshimie na watanzania waheshimike kwenye kila sehemu hasa maeneo ya kazi.

Basi angalau wangesema kima cha chini kwa kazi za dayworker kiwe 10000 angalau.
Kama waajili wataona ni nyingi wawepe mikataba hao wafanyakazi japo ya miezi mitatu kwa hiyo mishahara ya kima cha chini nadhani ni laki na 90 kwa sasa..
 
Unafikiri kwa nini Serikali inakamata wauza dawa za kulevya? Kwa nini isiwaambie tu watu wasinunue??
Serikali hiyo hiyo pia imeweka sheria na miongozo mbali mbali ya kuwalinda hao wafanyakazi,unadhani msimamizi wa hizo sheria ni Mo Dewji?
Kima cha chini cha serikali kinafahamika na masaa ya kazi yanafahamika huyo mleta uzi ameleta thread ya kibaguzi na sio hoja ndio maana nimepinga hata yale ya msingi yaliyo katika thread uzi wake.
 
Kwa namna hii siwezi kuacha upumbavu boss,shida sio Mo Dewji shida ni serikali yako hilo tunaweza jadili mimi na wewe boss...Labda tuanzie hapo hao unaowaita ndugu zako wewe umewapa mbadala upi wa kufanya maisha ambao ni bora zaidi? au unaimba tu humu ili uonekane na wewe Watanzania wote ni ndugu zako kinafiki?
 
Umechelewa kujua mkuu mbona kitambo sana,bakhresa ndo pekee analipa vizuri,ila kupata nafasi ngumu,ukibahatika unaweza ingia mara Moja,pale kipawa.
 
Muda mwingine jaribuni kutoka nje kuangaza ya dunia. Hao mama lishe wote unaowaona mjini humu wasaidizi wao wanalipwa 3000 kwa siku imagine toka asubuhi chai, chakula cha mchana hadi usafi jioni na bado mtu yupo tu ndo ujue Hali mtaani ni mbaya
Kweli kabisa
 

Waswahili wengi wao sio watu wa kazi, ni heri kuajiri wahindi au wachina hata mshahara utakayolipa itakua ni halali.

Najua kufanya kazi na wahindi ni changamoto japo sidhani kama ni wote wapo hivyo.
 
Kwa hiki kizazi cha wavivu wanaopenda maisha laini kinacholazimisha kuishi Dar es Salam umedhani rahisi kumshawishi enda shika jembe kwenye majaruba??
 
UMEWAZA SANA
 
Kwa hiki kizazi cha wavivu wanaopenda maisha laini kinacholazimisha kuishi Dar es Salam umedhani rahisi kumshawishi enda shika jembe kwenye majaruba??
Isiwe kisingizio eti maisha laini wangekuwa wavivu kiasi hicho hata hiyo kazi wasingepeta mkuu.Tukemee kwa nguvu zote watu walipwe vizuri kulingana na kinachozalishwa asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…