Tetesi: Kumbe Mo Dewji analipa TZS 4,000 watu kwenye kampuni yake

Kama tunakunywa jasho la Watanzania wenzetu basi afanye Mo extra buku alipe hao binadamu 10,000 kwa siku.
Hata akifanya elfu kumi au laki moja kuna shareholders wataendelea kutaka faida zaidi hivyo lazima kuna sehemu kuwe na mapunguzo (cost cutting) na ndio hivyo supply and demand na kwenye dunia ya automation nguvu kazi haina demand tena.., tena hapo anaweza kufunga machinery / robotics hazilalamiki, haziibi wala hazichoki na kuugua..

Cha maana katika hili soko huria ndio maana kila siku nasema liwepo soko huria na serikali UMMA/ Ukiwemo sababu the only language bepari anaelewa ni Profits na hata ukiona anakupa mshahara mkubwa ni sababu bottom line wewe una faida ya ku justify mshahara huo (iwe ni productivity au public relations)
Halafu Pepsi au Coca-Cola inauzwa shillingi ngapi na vibarua katika hizo kampuni wanalipwa shillingi ngapi??
Tukiongelea Coca na Pepsi worldwide hivi unajua ni mazingira mangapi wameharibu na kuna kipindi nchi fulani walifunga kabisa mto watu wakakosa maji safi na salama ili wayatumie kwenye products zao (na hapo bila public relations i.e. wasionekane wanyonyaji hivyo kupoteza sales worldwide ndio maana wanabanwa hata kuwalipa watu peanuts...

Tukubaliane baada ya kina Thatcher na Regan kuua vyama vya Wafanyakazi hivyo mfanyakazi kukosa bargaining power it has been a dog eat dog world..., Na ndio hilo Soko Huria (you can not Have your Cake and Eat it too...)

 
Hawana uwezo wa kusomesha hata mtoto mmoja kwa kipato cha 4,000 kwa siku. Serikali inalipia gharama zote kwa primary mpaka form six. Hiyo 4,000, nauli, chakula kwa siku na kodi ya nyumba hesabu inapinda Kona wala siielewi. Kweli huo ni utumwa wa hiari.
 
Basi awalipe hata 10,000. Hiyo 4,000 sawa kabisa hata kama ndio tuko kwenye soko huria, ni malipo ya udhalilishaji.
Kweli kabisa elfu4 kwa maisha ya sasa hivi utasave nini? Inasikitisha.

Bado mishahara ya miaka 10 nyuma hawapandishi mpaka leo wakati kampuni inakua na gharama za maisha zinapanda kila siku.
 
Ni kwa vile bongo hatuna wapiga kelele wakubwa wa haya masuala wanaoweza kusikika kimataifa, kweli ingekuwa skendo kubwa sana huko nje ingesikika Mo analipa $1.5 per day.
Haya mambo yamefanyika sana ulaya na China wakati wanajitafuta ila kwa sababu wenzetu wana sera nzuri na muendelezo bora si ajabu sasa haya mambo hayapo wamekwisha jipata.

Tanzania itachukua muda mrefu itategemeana na sera za nchi na serikali iliyopo madarakani.

Tujikipata haya mambo yatakaa sawa tu ni hatua tu ya ukuaji kiuchumi.
 
Ukisoma kitabu "rich dad poor dad" utaishia kumkubali Mo, otherwise upitie njia zake nawe uwe na projects zako kama njia ya kujikwamua kiuchumi na si kuajiliwa.
 
Ni kwa vile bongo hatuna wapiga kelele wakubwa wa haya masuala wanaoweza kusikika kimataifa, kweli ingekuwa skendo kubwa sana huko nje ingesikika Mo analipa $1.5 per day.
Achana ni 1.5 per day Nike wenyewe wameshabanwa na activits mara kibao kutumia mpaka child labor na kumbuka hio ni world brand ambayo inajifanya ni humane..., ila ndio hivyo has anything change ?!!!

 
Mkuu, hii ya kula na kulala hapo si hoja maana hata gerezani wanakula na kulala bure. Anyway, nilichotaka kumwambia mleta mada ni kuwa tatizo la ujira mdogo Tanzania si kwa Mo tu unless tunataka kuleta unafiki.
 
Hizi kazi za viwandani bongo kumbe karibia zote ni sweatshops tu, hazina tofauti na utumwa wa hiyari.
It's vicious circle of poverty.
 
Simtetei Mo Dewji kwa sababu za mgongano wa kimaslahi....ila ninatamani watanzania tuzidi kuwa bora kimtazamo na kimaendeleo......

Umejipeleka kulipwa elfu 4 ilihali unatumia nauli kwenda na kurudi kazini...kwanini usikaange mihogo nje ya nyumba yako ?!!

Umekubali kuendesha maisha ya familia yako kwa hiyo elfu 4 basi itakuwa unafanya WIZI huko kiwandani kwa MO DEWJI na ndio maana naye ameamua kukupa kiasi hicho....
 
Nike ilishakubali maovu yake yote na ikachukua hatua kubadilisha hayo. Jikite kuwataka wakina Mo na wenzake wengine wa Tanzania wakubali na kuchukua hatua kubadilisha huu utumwa wa kisasa.
 
Tumuamini nani sasa?Mleta uzi kaeleza wafanyakazi wanalipwa 4000 na mchangiaji mwingine ameeleza ni 7500.Kama ni 7500,je ni malipo kidogo hayo?

Tumuamini nani sasa?Mleta uzi kaeleza wafanyakazi wanalipwa 4000 na mchangiaji mwingine ameeleza ni 7500.Kama ni 7500,je ni malipo kidogo hayo?
Mkuu mimi kwa bakharesa mara ya kwanza mililipwa 11k. Mara ya pili 9k. Inategemea na idadi watu hiyo shift yenu na idadi ya viroba vilivyobebwa 12hrs non stop. Inafika time ukiwaangalia wanaobeba viroba nenda rudi nenda rudi unawaomna ni kama mazombi vilee. 12hrs non stop nenda rudi nenda rudi na 25kg. Pumzika yako ni kwenda toilet tuuu na kunywa maji.

Point yangu sio kuwa unalipwa tsh ngapi. Point yangu ni kwamba kazi za mule kubeba viroba masaa yote yaleee HAZIFAI. Walau angeweka masaa 6 per shift.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…