Kasi ya kina Mbowe, Lisu ,Msigwa, Lema na Nape, Makamba na Chadema kwa ujumla kushambulia hayati Magufuli imeishia wapi?
...Nashauri Vunjeni Madaraja na Flyovers zote, Ng'oeni reli zote especilly SGR, uzeni Ndege zote na vivuko vyote nchini, Uza Meli zote Mpya zilizozinduliwa, kule Ziwa nyasa, simamisheni Ujenzi wa Bwawa la umeme, Gaweni Migodi yote, Binafsisheni Milima, Maziwa na Mbuga.
Bomoa Bandari zote zilizoboreshwa ikiwemo Mtwara, Tanga na Dar, Jengeni moja ya Wachina kwa mkataba wa miaka 100...rudisheni Ada shuleni tukuze uchumi, Wapeni Matajiri Exemptions za kodi, Ruhusuni Makinikia kwenda nje, Vunjeni Masoko mapya ya Madini mikoani, ...Charaza Bakora Machinga mjini, Mwaga wali wa Mama Ntilie.
Vunja vyama vya wakulima na utaratibu wa stakabadhi ghalani, Ruhusuni Uhuru wa Mashoga, Mateja kwa wingi mtaani, madawa ya kulevya n.k....pia Msisahau kuifunga ile Mahakama ya Mafisadi,....kwa uchache tu Hakika hapo sasa pengine Tanzania itakuwa kama ULAYA, Tanzania ya Asali na Maziwa!.
" Siku moja mtanikumbuka"- JPM.
"Vita ya kiuchumi ni ngumu"- JPM
"Nimeamua kuwa Sadaka ya Watanzania" - JPM.
"Nimesacrifice Maisha yangu kwa ajili ya Watanzania Wanyonge" - JPM.
Note Uzalendo ni kusimama na nchi yangu, uzalendo si kusimama na hili kundi la kinafiki lililojitokeza ili wafute mazuri ya JPM kinafiki.
Malori kukwama bandarini ni furaha kubwa sana kwa Lema, Msigwa, Lisu na chadema kwa ujumla kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kuuwa legacy ya Magufuli.
Huwezi kuchafua oil chafu itakuchafua, tayari chadema maji ya shingo .
Magufuli aliwagaragaza akiwa hai atawagaragaza akiwa mauti.