Huo ndio ukweli kwamba historia itaendelea kumkumbuka hayati Magufuli wakati wote kwa yale mema aliyoyatenda kwa taifa hili lililopendelewa na Mungu.
Magufuli atakumbukwa kwa uchapakazi na ujasili wake.
Nje ya CCM Magufuli amejenga SGR, amenunua ndege, Ubungo fly over, daraja la kigongo - busisi, haya yaliingizwa kwenye ilani baadae baada ya ubunifu wake wa kisayansi.
Kama binadamu atakumbukwa pia kwa mapungufu yake ya kutowasimamia sawasawa TRA, DPP na Takukuru kiasi cha watu kubambikiwa kesi na wengine biashara zao kufungwa.
Lakini kwenye mzani Mema yamezidi mabaya ndio maana tunasema Kazi Iendelee huku makosa yakirekebishwa.
Nawatakia Sabato yenye baraka!