Kumbukumbu (Legacy) ya Dkt. John Pombe Magufuli
Ila sio siri mkuu unateseka mno hadi naingiwa na huruma. Hivi Magufuli alikuwa nani kwako ukiachilia kuwa alikuwa rais wa nchi?
 
SI RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ALIYEKO MADARAKANI KWA SASA WALA RAIS AJAYE, ATAKAYEMFUNIKA HAYATI RAIS MAGUFULI KIUTENDAJI, IWE KWA SIKU 100 AU MIAKA 100 IJAYO:
Rais Bora sio Mtendaji bali ni kuunganisha nguvu kazi zote ili watende (mtu mmoja huwezi kufanya kila kitu), ila hata wewe usipofanya mwenyewe, kuwafanya watu wafanye ndio uwezo / ubora wa kiongozi.

Kuwafanya watu wa-give their all, kwa yule Bwana kutenga baadhi ya watu / kuwadhihaki, ni upotevu wa nguvu kazi
 
Legacy aliyoacha Magufuli ni hii hapa:

1.Kuondoka duniani wakati hahitajiki.

2.Kuteka wapinzani wake kama akina Azory Gwanda.

3.Kutesa wapinzani wake kwa kuwaweka ndani kila siku.

4.Kuua wapinzani wake na wakosoaji wake kama akina Ben saanane na kuwapiga wapinzani wake risasi kama ilivyokuwa kwa Tindu Lissu.

5.Kuua uhuru wa vyombo vya habari.

6.Kuua uhuru wa kujieleza kwa wananchi kama vile kufungia mitandao ya kijamii kama twitter na kukamata wanaotumia mitandao mingine kumkosoa.

7.Kuiba kura kwa kutumia Polisi,jeshi,TISS pamoja na tume ya uchaguzi.

8.Kuua biashara za watu kupitia sera mbovu za uchumi.

9.Kudanganya katika takwimu za ukuaji wa uchumi wa nchi.

10.Kuweka mihimili yote mitatu mfukoni mwake,yaani mhimili wa urais,bunge na mahakama.

11.Kuua uchumi wa nchi kupitia sheria mbovu za uwekezaji.

12.Kuua watu kwa Corona kupitia leadership negligence.

13.Kuhakikisha kuwa akina Ben Saanane na Azory Gwanda walikipata cha mtema kuni.

14.Ukabila kwa kuhamishia rasilimali nyingi za nchi katika wilaya ya Chato na kujaza wasukuma serikalini.

15 Ukanda kwa kupeleka SGR mwanza wakati siyo economic viable zone.

16.Ubaguzi wa rangi kwa kuwakandia wanawake weusi.Imagine mtu anafanya ubaguzi wa rangi karne ya 21!Is this not insane?

17.Kugandamiza demokrasia kwa kukataza vyama vya upinzani kufanya siasa wakati CCM kufanya siasa ni ruksa.

18.Kunyanyasa malaika-watoto wa kike wasirudi shule wakipata mimba.

19.Ufisadi wa kutisha kwa kufanya miradi mikubwa bila budget kupita bungeni.

20.Wizi wa kutisha wa mali ya uma kupitia kampuni yake ya Mayanga constructions LTD.Mfano uwanja wa Chato umetengenezwa na kampuni hii bila tenda kuitwa.

21.Kubambikizia kesi za kuhujumu uchumi wapinzani wake nchi nzima na kuwatupa korokoroni bila dhamana.

22.Kugushi report ya CAG ya hasara za mabilion za ndege za ATCL na kuilazimisha ATCL watoe gawio fake kwa serekali.

23.Kupora utajiri halali na wa jasho wa matajiri wa Tanzania kwa kuwabambikizia kesi fake za kuhujumu uchumi na kuwalazimisha wakiri makosa ya uwongo kisha kuwafilisi mali zao.

24.Ufisadi na wizi wa kutisha kama ulivyoibuliwa na CAG mara baada ya dikteta kufa.

Umemaliza yote mkuu

Kuongezea tu ambalo siyo la umuhimu sana ni kupora pesa za wafanya biashara wa ‘bureau de change’ na wengi wakiwa na leseni halali za kuendesha biashara na kisingizio ni sehemu za kutakatisha pesa chafu utafikiri regulator (BOT) walikuwa likizo
 
Kila awamu huacha kumbukumbu zake muhimu wengine hutumia neno "Legacy". Kwangu mimi ninaamini wananchi na Taifa litamkumbuka Rais Dr JPM kwa mambo yafuatayo baada ya muda wake kuisha:

1. Nidhamu maofisini haijawahi kutokea maadili na nidhamu kurejeshwa hivi hata kama bado kuna changamoto ya rushwa maeneo kadhaa.

2. Kuhamishia serikali makao makuu Dodoma na ujenzi wa Ikulu na mji wa serikali. Na uendelezaji wa jiji hilo kwa kasi i.e miundo mbinu barabara na uwanja ndege Msalato etc.Amevunja mwiko ulioshindikana.

3. Kufufua shirika la ndege la ATCL "the national flag bearer".hili lilishindikana huko nyuma.changamoto nyingine zozote za kiuendeshaji za kampuni ni sehemu ya mapambano kama ilivyo biashara yoyote,rada 4 viwanja vya ndege vikuu nk.

4. Daraja la Busisi Kigongo "generational Miracle" ni alama ya kudumu milele.

5. Reli ya SGR ni alama na kumbukumbu kubwa mno.

6. Daraja la Tanzanite na flyovers.

7. Umeme wa Stiglers Gorge JKNHP.

8. Mifumo ya ukusanyaji mapato ya serikali na mageuzi kwenye madini.Haya ni mambo makubwa sana vizazi vitamkumbuka. Yapo mambo mengi ila haya ni kielelezo na alama ya kudumu. Mungu ambariki

Soma pia Hayati Magufuli ameacha legacy ya kuthubutu kufanya kitu bila ya kuomba ruhusa kwanza kwa mfadhili yeyote
🚮🚮
 
1. Nidhamu ya woga iliyojengwa katika msingi wa vitisho na wafanyakazi kulia hawajapandishiwa mishahara kwa miaka si kitu cha kujivunia. Kwa kiasi kikubwa huu ni woga na si nidhamu.

2. Wazo zima la kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma ni wazo la kisiasa lisilo na tija kubwa kiuchumi.

Ni mazingaombwe ya mtu aliyeshindwa kazi ya kuboresha uchumi wa Mtanzania masikini. Ni habari ya mtu aliyeshindwa kufanya kazi ya umuhimu aliyopewa kufanya, akaamua kujitungia kazi nyingine tofauti ambayo hajapewa.

Nyerere nampenda kwa mengi sana. Hususan zama hizi za uongozi mbovu, nikimkumbuka from all those Ikulu parties - my mom used to work in the Nyerere Ikulu, so, I ate some of Miss Wicken's famous apples. That is to say, Nyerere is a personal figure to me, not just a mythical politician- nikimkumbuka na kumsoma, namuona ni political giant.

Lakini, mimi ni mtu wa ideas. Siangalii mtu. Nilikuwa nabishana na mama yangu kuhusu makisa ya Nyerere - she could see no wrong in the man- mpaka naona inataka kuwa ugomvi mbaya. Namtuliza bi mkubwa kisiasa.

And the man knew how to take care of his immediate staff. Very humane gentleman. Something I cannot say for the current occupant.

So, that is the personal context of how Nyerere was held high in my household.

Lakini.

Kwenye kuhamisha makao makuu ya serikali kwenda Dodoma Nyerere alikosea sana.

Alikuwa anatatua tatizo ambalo halipo, katika nchi ambayo ina matatizo mengi sana ambayo yanahitaji utatuzi.

Hakuna Mtanzania aliyelia anataka makao makuu yabserikqli yaham8e Dodoma.Hii haikuwa kwro ya wananchi.

Nyerere alijitungia tu hii habari. Hii habari haina tija kiuchumi. Kwa kweli ni habari ya anasa inayotugharimu tu.

Kwa hivyo, mimi sioni kama ni kitu cha kujivunia.

It is one of the biggest white elephant projects, economically speaking.

Makao makuu ya serikali tayari yalikuwapo Dar. Kulikuwa na haja gani ya kuhamisha kwenda Dodoma?

Muandiahi mmoja- Nafikiri Jenerali Ulimwengu- alisema akikejeli habari hii, na kusema kwamba makao makuu ya serikali ya Tanzania sasa si Dar wala Dodoma. Ni barabara ya kuiunganisha miji miwili hii.

Viongozi mpaka leo wanatumia muda mwingi sana, mafuta mengi sana, allowances nyingi sana, kwa safari za Dar- Dodoma and back.

Ni anasa ya ajabu sana kwa nchi ambayo ina upungufu wa fedha za kigeni.

3 Habari nzima za "national flag bearer" zimepitwa na wakati. Biashara ya ndege ni ngumu sana, inabadilika kwa haraka sana. Na haiendani na dhana nzima ya serikali kujitoa kwenye biashara na kuweka mazingira ya biashara yawe mazuri. Tulishafika pazuri sana na Fastjet, Precision Airlines etc. Hakukuwa na haja ya serikali kujiingizq katika biashara ya ndege yenye risk kubwa na colossal losses.

Again, we are trying to solve non existent problems, while real and existing problems qre not solved!

Ndege zimeanzia Marekani. Kitty Hawk hapo North Carolina ndipo Wright Brothers waliporusha ndege mara ya kwanza duniani mwaka 1903.

David McCullough, muandiahi wangu mmoja mshindi wa nishqninya Pulitzer ninayempenda sana kaandika kitabu kizuri sana kuhusu historia ya ndege ya kwanza kuruka. Kitabu kinaitwa "The Wright Brothers". Nimekisoma. Kitabu kizuri sana kwa wanaotaka kujua historia ya ndege.

Wamarekani wanajua sana biashara.Ila serikqli yao imekataa habari za "national flag carrier". Kwao ukiongelea flag carriers unaongelea US Air Force. Ndege za kijeshi.

Huku kwenye biashara, serikali imejitoa. Inaweka mazingira ya biashara yawe mazuri tu.

Private companies zinashindana.

Unafikiri Wamarekani ni wajinga kufanya hivyo? Serikali ya Marekani haitaki faida kutika biashara ya ndege?

Wanajua biashara hii iko very tricky. Serikali imeiachia sekta binafsi.

Sisi mpaka leo tunatamba na habari za national flag carrier?

Tunaitaka "national flag carrier" kwa ujiko wa kisiasa au ufanisi wa kibiashara?

If it is the former, how much are we ready to throw down a bottomless pit for this foolish extravagance?

If it is the latter, is this avaricious?

Hivi watu wanajua hata ATCL ina operate at what loss or profit? Woth all this Ikulu interference and audit blocks? All these purchases that are totally outside of the open tender process?

Is this something to be proud of as a legacy?

4. Daraja, hata kama lina tija, halidumu milele.

Hapa tunarudi kwenye mjadala wa maendeleo ya vitu na watu. Granted. Tunahitaji madaraja na vitu. Lakini ukiona kiongozi anasifiwa sana kwa kuleta maendeleo ya vitu lakini hana accomplishment kwenye kuendeleza mawazo ya watu, hapi ujue kuna tatizo.

Nyerere hakuleta maendeleo ya vitu sana. Lakini aliwapa watu maendeleo ya watu. Kuna Bibi alizaliwa kabla ya Nyerere (1920), alikuwa mtu wa dini sana. Lakini alisikitika sana kutojua kusoma.

Nyerere alivyoleta habari za "Elimu ya Watu Wazima", huyu Bibi alipata nafasi ya kusoma. Aliweza kusoma Biblia yake mwenyewe bila ya kusaidiwa na mtu. Alisoma barua zake mwenyewe bila ya kusaidiwa na mtu. Hayo yalikuwa maendeleo makubwa.

Kipindi hicho, Tanzania ilikaribia 100% literacy rate.

Karibu kila mtu wa umri wa kujua kusoma alijua kusoma.

Kwa sasa nafikiri tumeshuka kutoka literamacy rate hizo za enzi za Nyerere.

Watu wengi zaidi, kwa asilimia, hawajui kusoma.

Sasa unaweza vipi kuwa na demokrasia na uhuru wa kuchagua katika nchi ambayo watu wasiojua kusoma wanazidi?

Hiki ni kitu cha kujivunia?

Ukiwa na daraja zuri jipya, halafu watu hawajui kusoma alama za darajani, hilo ni jambo la kujivunia?

6. Unarudia madaraja. Inaonekana huna kitu tofauti. Maneno yangu ya hapi juu jibu namba 5 yanahusika hapa pia.

7. Umeme wa Stiglers Gorge utamsaidia vipi mtu asiyeweza kumudu kuununua na serikali ambayo haiko investor friendly kuweza kuleta investors wengi walete ajira na kuutumia vilivyo? Unajua terms za finacing of the projects? Unajua Return on Investment Projections?

8 Mifumo ya ukusanyaji wq mapato iliwekwa tangu enzi za Makapa alipoanzisha TRA. Sioni kipya alichofanya JPM zaidi ya kuiingilia kisiasa na kusababisha TRA iweke unrealistic goals zinazofanya watendaji wake wabambikie watu kodi za juu kabla hata hawajaanza biashara. Na hili matokeo yake ni watu wengi kuona biashara ni ujinga, kwa sababu wanafanya biashara ili walipe kodi, na faida kwao ni ndogo sana.

Watu wanafunga biashara sasa hivi.

Nina rafiki zangu kadhaa wana biashara zao, wanafunga kwa sababu wamebambikiwa kodi za ajabu.

Watu wanauza nyumba zao Mbezi Beach na Mbweni kwa bei za kutupa, kwa sababu wanadaiwa kodi za ajabu na TRA. Na biashara mbaya, watu hawana hela.

Mimi familia yangu ina nyumba ya biashara prime area Dar (Oysterbay). Rent ilikuwa inapanda tu kila renewal. Kwa sasa rent zimeshuka sana. Hata nyumba zetu za Oysterbqy za kupangisha mabalozi wa nje. Wafanyabiashara wanafunga biashara zao.

Etihad is gone. Exxon Mobil is gone. Dangote is gone. So many more global business brands are gone.

Rafiki zangu wawekezaji wa ndani wanafunga biashara.

Hii ndiyo legacy ya Magufuli.

Rais aliyeua biashara Tanzania.
Mzee si kwa kunyoosha huku with white examples...me n mmoja wa watu wanaoshangaa namba watu wanataka kumpa utukufu bwana yule..sijui may be walikua side ambayo wapo benefited tofauti na hivyo no upuuzi wanajitahid kutuaminisha...me siyo mkubwa saaaana ki umri, nikiwa anasoma tu kuhusu watu kukimbia Nchi zao ila kwa macho yangu makavu nimeona kipindi cha mwendazake, uwanja wa ndege chato, Hifadhi ya burigi, kuna mazingira ya kingship kind of leading alikuwa anatengeneza huwez jenga uwanja wa ndege kijijini kwako wakati unajua utakuwa madarakani kwa miaka kadhaa tu unless otherwise ndo utawala wa kiimla ulikuwa ukiandaliwa.
 
SI RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ALIYEKO MADARAKANI KWA SASA WALA RAIS AJAYE, ATAKAYEMFUNIKA HAYATI RAIS MAGUFULI KIUTENDAJI, IWE KWA SIKU 100 AU MIAKA 100 IJAYO:

Naomba nianze kwa kusema kwamba, Kujaribu kulinganisha utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza siku 100 madarakani, dhidi ya siku 100 alizotimiza hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ni sawa na kufananisha kati ya ukubwa wa Mlima Kilimanjaro na Kichuguu, ambapo ni vitu viwili tofauti.
----------------------------------
Hivi sasa kuna mjadala unaoendelea nchini, ni kuhusu utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza siku 100 madarakani pamoja na mafanikio yake. Kwenye mjadala huu kupitia vijiweni, vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii, kuna sifa kedekede zinazotolewa na makundi mbali mbali ya watu wakiwemo, wanaharakati, waandishi wa habari, wasomi, wanasiasa, pamoja na wananchi wa kawaida.

Wapo wanaosema mama ameanza vizuri, wapo wanaodai mama amekuja kuiponya nchi, wapo wanaodiriki kusema mama amerudisha utawala wa sheria, wapo wanaosema hakuna chombo cha habari kilichofungiwa, na pia wapo wanaosema hakuna aliyekamatwa au kufikishwa mahakamani kwa kosa la kuikosoa serikali kama ilivyokuwa huko nyuma, na wengine wanadai, hivi sasa nchi inapumua baada ya watu kubanwa kwa kipindi cha miaka mitano bila kufurukuta.

Ukifuatilia mjadala huu unagundua ni kama vile kuna mambo mawili. Moja watu wajaribu kuonyesha kana kwamba, kuna ushindani wa ubora kati ya utendaji kazi wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyeko madarakani dhidi ya utendaji kazi wa hayati Rais Dkt. John Pombe Jiseph Magufuli, na jambo la pili ni kujaribu kuonyesha kwamba, Rais aliyeko madarakani ni mwema zaidi kuliko mtangulizi wake.

Baada ya kuufuatilia na kutafakari kuhusu mjadala huu, nimebaini kuhusu kuwepo kwa mapungufu matatu muhimu yanayowasumbua watanzania.

Jambo la kwanza, watanzania hatuna ufahamu wa kufuatilia maswala muhimu yanayolihusu taifa letu na badala yake tunajikita kusifia pamoja na kupongeza mambo madogo madogo yasiyokuwa na tija wala umuhimu katika maisha yetu. Kwenye eneo hili watu hawajishughulishi japo kuhoji kuhusu mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo ambao tuliambiwa, kutokana na masharti ya hovyo yaliyokuwemo kwenye mkataba huo, ni kichaa tu ambaye angeweza kuyakubali. Kwa watanzania, hilo si muhimu, kilicho muhimu kwao ni kupumua.

Aidha, vile vile watanzania hawajishughulishi kuhoji kuhusu waliokwapua mamilioni hazina na kujilipa posho, ni lini watafikishwa mahakamani, bali kilicho muhimu kwao ni kupewa uhuru wa kutukana mitandaoni pasipo kukamatwa. Watanzania hawajishughulishi kuhoji kuhusu wahujumu wa uchumi, na wezi wa mafuta waliotoboa bomba la mafuta ya serikali kule Kigamboni na watuhumiwa 14 kukamatwa watafikishwa lini mahakamani, isipokuwa kilicho muhimu kwao ni kuambiwa wadumishe amani huku nchi inateketea.

Kwenye eneo hili wanachosahau watanzania ni kwamba, kama kuna kiongozi aliyeingia madarakani, akashughulika na kero lukuki zilizokuwa zikiwakabili wananchi bila kupatiwa ufumbuzi, ikiwemo huduma mbovu za afya hususani kwa mama wajawazito kujifungulia chini, basi kiongozi huyo si mwingine isipokuwa ni hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Pia watanzania wanasahau kwamba, kama kuna kiongozi aliyeingia madarakani akakuta nchi imeoza, inanuka rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na uporaji wa rasilimali ikiwemo madini, ujangiri wa tembo na mikataba ya ovyo, basi kiongozi huyo si mwingine bali ni hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Vile vile watanzania tunasahau kwamba, kama kuna kiongozi aliyeingia madarakani na kukuta ujambazi wa kutumia silaha umeshamiri kufikia hatua ya mabasi kutosafiri usiku baada ya saa 4.00 ukiachilia mbali ajali zilizoua watu makumi kwa mamia kika uchao na kukomesha hali hiyo, basi kiongozi huyo si mwingine bali ni Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Sanjari na hiyo, watanzania wamesahau jinsi Chama cha Mapinduzi kilivyonuka rushwa na ufisadi kila kona kiasi cha wanachama wake pamoja na mashabiki kuzomewa popote walipoonekana wsmevaa sare za Chama. Ni hayati Rais Msgufuli aliyeking'arisha na kukirudishia uhai wa kupendwa.

Ndani ya siku 100 za Magufuli, wagonjwa wote Muhimbili walilala kwenye vitanda badala ya kulala chini sakafuni au mzungu wa nne. Ndani ya siku 100 za Magufuli, madawati yalitengenezwa karibu nchi nzima. Ndani ya siku 100 za Magufuli watumishi hewa zaidi ya 19,000 walibainika kisha kuondolewa kwenye mfumo.

Ninachotaka kusema ni kwamba, kujaribu kulinganisha utendaji kazi wa siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, na siku 100 za hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ni sawa na kulinganisha Mlima na kichuguu.

Kwangu mimi ukiniuliza ni jambo gani Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kwa siku 100 alizokaa madarakani ninaloweza kumpongeza, ni kushusha gharama za wateja kuunganishiwa umeme kutoka zaidi ya Tshs. 300,000/=, kuwa Tshs. 27,000/=, iwe kijijini au mjini.

Mengine yoote anayofanya ni kuwapa ahuweni wezi, wakwepa kodi, mafisadi, kuwaachia walioua Padiri, kumwagia watu tindikali pamoja na kuwaumiza wafuasi wa Chama chake waliokipigania Chama kwa gharama ya jasho la damu kupata ushindi katika mazingira magumu. Ndiyo maana majambazi wameibuka kwa kasi, mapato yameshuka, watu wanadiriki sasa kutoboa hadi bomba la mafuta, ajali zimerudi kuuwa abiria kama wote. Sijaona nimsifu Rais kwa lipi, kwa siku 100 alizokaa madarakani.

Yaani wakati Mbowe na Chadema yake wakiwapambania wafuasi wake wanaokitetea Chama katika mazingira ya kihalifu, ikiwemo kuitukana serikali, yeye mama anawafurahisha Chadema hao hao kwa kuwakomoa wafuasi waliokipigania Ccm katika mazingira magumu. Wakati utafika, pumba na mchele.
Mkuu huu muda uliotumia kuandika huu upuuzi si ungeutumia kumkatikia mumeo huenda ukapata Mimba? Maana mimba imekuwa changamoto kwako miaka nenda rudi?
 
Si ndio nyie mnaojidanganya kwamba akifa mtu na legacy yake anakufa nayo? Watu wa aina yako mlijitahidi kumfuta Nyerere wee na nia yake ya kujenga nchi huru inayojitegemea, lakini wapi. Ndio maana tunasema msifurahi kupita kiasi, kufa kwa JPM si kufa kwa spirit au legacy yake.
Mmmmh...
 
Tundu Lissu alijaribu kutukana legacy ya Nyerere akakutana na nguvu ya uma.

Hatokaa arudie tena.
Nguvu ipi aliyokutana nayo ambayo unaijua wewe tu? Toka barabarani na gari yako funga spika ingia mtaani tangaza legacy yake, hapa Jf tutaishia kukutukana tu. Toka nje huko kaseme alinunua ndege, alijenga flyover Dsm, amerudisha nidhamu, kahamishia serikali Dodoma then ikifika jioni uangalie kama gari yako itakuwa na vioo!!
 
1.Wakati wa JPM, hakukuwa na ubabaishaji katika taasisi za Serikali, sasa ni balaa tupu.

2. Wakati wa JPM bei za vitu hazikuwa zikipanda ovyo ovyo, sasa ni balaa tupu.

3. Wakati wa JPM, hakukuwa na kata kata ya umeme, sasa ni balaa tupu.

4. Wakati wa JPM hakukuwa na upigaji, lakini sasa ni balaa tupu.

5. Wakati wa JPM hakukuwa na vibaka wala PANYAROADS lakini sasa ni balaa tupu.
RIP, JPM, Mwana Afrika na mzalendo wa kweli.
 
Back
Top Bottom