Thread inamwongelea Magufuli. Sasa hao unaowataja anzisha thread yako kuwahusu pia tutaongezea kwenye list yao.
 
Mzee magufuli ameiachia tanzania ukiwa

Hakika JPM ni Rais bora kabisa wa kizazi chetu. Apumzike kwa amani mbinguni.


wape maneno yao wanaompinga jpm wengi ni chadema domo tusi

JPM daaaaaah.!!! kufa kufaaana imewaachia nchi wala Bata wanaekti movie na ruby zinapotea
1. Wakati wa Magufuli alizuia kupandishwa kwa madaraja watumishi wa Umma, yaani akakanyaga sheria za Utumishi na watu wakakosa haki zao na hakuna wa kuwatetea, UKISEMA UNATUMBULIWA..!!!

Rafiki yangu alitakiwa kupanda madaraja mawili (2015 na 2019) ila baada ya kifo cha Magu akaja kupanda 2021 kwa daraja moja.
Ina maana bila Magu kufa ASINGEPANDA?
MUNGU ALILIONA HILI NINI?

2. Wakati wa Mafuguli kukazuiwa "Annual increament" ambayo ipo kisheria.
Yaani Magu aliamua kuvunja sheria iliyopitishwa na bunge.
YE ALIKUWA NANI?

3. Wakati wa Magufuli Vibali vingi vya ruhusa vilizuiliwa.
Kwakuwa yeye alikuwa Raisi na wanae wakaajiriwa REA na u-DAS huko, basi hakuona umuhimu wa kuajiri watoto wa wenzake?

KIFUPI ALININYIMA WATU WENGII HAKI ZAO na hasa zile za USTAWI WA UCHUMI.

Kokote alipo ajue kabisa ""ALIKANYAGA SANAA SHERIA TENA KWA MASLAHI YAKE NA MAWAZO YAKE MWENYEWE""

#YNWA
 
KWA Sasa karibu KILA taasisi wanakwea mwewe tu angani kwenda nje sijui kwenye visemina,kinachouma ni kodi zetu tunakamuliwa kinoma Ili watu wapige per diem.

KILA taasisi Sasa hivi ina semina na vikao,Daah hatari sana hii.
 
Michezo ya kufuturisha hovyo hovyo imeanza upya kwenye taasisi za serikali(wakuu wa mikoa na taasisi zake).

Tutegemee mwakani sherehe na tafrija za kuukaribisha mwaka kama kawaida,huku tukichapisha ma T-shirt na makofia ya kuukaribisha mwaka KILA taasisi huku miti ya X-mass ikijaa tele kwenye maofisi KWA budget kubwa kubwa
 
Tupo tunapambana na ROYO TUA,week Mbili nzima nchi ipo America,tukilamba posho za kutosha na msafara ulosheheni watu wa kutosha,Afu TOZO nakamuliwa mimi ninayemtumia hela ya dawa dada yangu mgonjwa
 
Halafu mnataka watu wasiongee KWA kuogopa kuitwa SUKUMA GANG,nyinyi ni empty tank kabisaa.

Tutaongea na kuzidi kuongea kijiti wamekabiziwa wahuni wanao pata uungwaji mkono na CHadema.
 
Kwani kikwete anaitwa Juma? Au Mwinyi anaitwa Mushi? Au mama samia anaitwa Rose? Eti muacheni Magufuli aitwe Magufuli, kumbe angeitwa nani sasa? Yesu? Au Muhammad?
Walishawahi kumfananisha na Mungu na kumuandalia mazingira ya kutawala milele.... Mungu mwenyewe kaona matusi yamezidi kamvuta fastaaaa. Yaani jiwe lingekuwa ndio limeanzisha mifumo mingi kama mkapa (TRA, NSSF, PCCB, TANROADS nk) sijui wangejisifuje
 
Hakuna utawala uliojaa wizi kama wa JPM
 
Hakuna utawala uliojaa wizi kama wa JPM
Andika hii>>>17/03 ni siku yenu ya maadhimisho ya sherehe za mafisadi TZ.


Hii mtaendelea kuadhimisha mpaka siku anakuja mwana mwengine wa kiAfrica kuleta ukombozi
 
Walishawahi kumfananisha na Mungu na kumuandalia mazingira ya kutawala milele.... Mungu mwenyewe kaona matusi yamezidi kamvuta fastaaaa. Yaani jiwe lingekuwa ndio limeanzisha mifumo mingi kama mkapa (TRA, NSSF, PCCB, TANROADS nk) sijui wangejisifuje
Hakuna aliyebisha,watu wanazidiana.
Ila hizo ni mifumo ambayo ni systematically document inayofatiwa na teuzi za kuzisimamia pamoja na budget zake TOKA serikalini mwanzo baada ya kuundwa na ni kitu kimefanyika Dunia nzima.

Ila jua kutofautisha kujenga nchi kimiundombinu,miradi ya kimkakati,kukemea ufisadi,utumishi wenye kujali utu na haki za raia na kuepusha kuulizana 'UNANIJUA MIMI NANI",Kudhibiti wa mali ya umma kama madini na wanyama(meno ya tembo na ongezeko la tembo n.k),Fursa sawa KWA wote.



TUNA MENGI YA JPM HUYU,TUKANENI NASI TUMEMUHIFADHI MOYONI.nukta
 
Magu kafa na harudi tena, utawala mpya, take it like a man, mambo ya udikteta na uhuni yeshapita, UCHUMI wa kishamba haupo tena, kuna formula za kurun uchumi, siyo kuvamia maghala ya watu kuwaambia wameficha sukari, ujinga mtupu
Wewe ni mshamba mara mbili usiyejua chochote kuhusu uchumi,umejazwa chuki na wivu tu kama mchawi.Huyo unayemuona hajui uchumi ndo alituvusha kiuchumi Tangu nchi hii inapata uhuru.
 
Sasa umeandika nini hapa
 
Kule mwanzo sikukuelewa, mwisho umekitambulisha vizuri na kujipambanua.
Kumbe chuki yako kwa JPM ni maslahi binafsi kuminywa. Kutozwa kodi ulizozikwepa kijanjajanja miaka ya nyuma na kukosa wateja baada ya wahujumu uchumi kusepa kutokana na kuzibwa mianya yao ya upigaji.
Hakika, wezi na walanguzi, wauza unga na wakwepa kodi hawakumpenda wala hawatampenda JPM daima
 

Wewe ni kilaza, bisha kwa kuleta matokeo yako ya kidato cha nne.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…