Lucha
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 14,516
- 50,658
Kwasababu ni ajabu kwa mwanamke wa kiafricaKwanini tusikitishe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwasababu ni ajabu kwa mwanamke wa kiafricaKwanini tusikitishe?
Hiyo dhana uliyonayo ndiyo walionayo wanawake wengi, kuwa ukizaliwa mwanamke tayari unajua kupika, kwa dhana hiyo ni kweli kula mtu anajua kupika.Mtu kutokujua kupika ni maamuzi tu.
Yani uwe na dhamira kabisa ugali, wali maharage vikushinde kupika!
I wish!Mtoto wa kishua wewe hata kuchemsha maji ya kuoga hujui.
Kila kitu anafanya dada
Kumejaa hukuMi sijawahi kula birian nilifikiri unajua unialike
Sawa ila fikiria ombi languKumejaa huku
Na hapa niongezee, kuna watu hapa wanalalamika wanawake zao hawajui kupika, muulize amemuwezeshaje mwanamke huyu. Huwezi kutaka mtu amalize ufundi na huku budget unambana. Chakula kitamu ni gharama, utake, usitake.Nadhani hata "utamu" wa kuku au chakula chochote inategemeana na umeshakutana na wapishi wazuri wangapi..
Kuna watu wanajua kupika chakula ili mradi watu wasife
wengine wanapika chakula kinacholika
Wengine wanapika chakula kitamu kikawaida
Halafu kuna mafundi wa kucheza na spices kiasi hata akipika mchemsho lazma ukubali
Umemuachia shingapi?Kizazi Cha ef2 au Generation Z
Wife angu nikizaz ch ef2 ayo mambo nagombana naye Kila siku, Leo kanunua kuku bloiler nusu aliekaangwa kanipikia na ugali, hii nimekuta kwenye hotpot nilivorudi mishee wazee..😄 Af kimelala na kinataka mambo.
Na wewe kwa akili hizi unajihesabia kabisa kwamba utakuja kuolewa! Labda ujioe mwenyewe hakuna mwanaume timamu anahitaji mke wa aina yako wallah!Kabla hamjaoa muwe mnawafanyia interview au kama vipi awe amepitia kabisa shule ya mapishi.
Ushauri mwingine...sio lazima uoe. Ajiri mpishi awe anakupikia, mfanyakazi wa kufua na kufanya usafi. Watu kama nyie ndo mnaharibu taasisi ya ndoa kwa uvivu wenu.
Hadi sasa umeoa wake wangapi na wote hawajui kupika?
Mabint wenyewe siku hizi wao ni kuzalishwa tu majumbani kwao hawajui kupika, hawajui kufua, hawajui kuandaa watoto na malezi yote kwahiyo wanazaa madanga watarajiwa na mashoga watarajiwa nani ana haja nao waendelee tu na u ferminism wao wajioe wenyewe tuuMabinti wengi wamejikita kwenye Mitandao ya kijamii, kupiga picha kali na kuzipost. Furaha yake akisifiwa ni mzuri au anatako kubwa, baasi ndo hayo. Muda wa kujifunza kupika haupo.
Kuna haja ya binti kua na cheti cha mapishi ku qualify kuingia ndoani.
Umekuwa kaongo ghafla sana.Tupo wengi kumbe🤣
Lakini pia wapo wanawake wavivu na wenye kuedekeza urembo hasa kucha zao. Hawa ni balaa sana kwa makusudi huwa wanakwepa shighuli za nyumbani ikiwemo mapishi.JANGA JIPYA LA WANAWAKE WENGI KUTOKUJUA KUPIKA NN CHANZO!
Tunaacha elfu 3 milo mitatu kwani haitoshi?Na hapa niongezee, kuna watu hapa wanalalamika wanawake zao hawajui kupika, muulize amemuwezeshaje mwanamke huyu. Huwezi kutaka mtu amalize ufundi na huku budget unambana. Chakula kitamu ni gharama, utake, usitake.
Kwa mfano kuna mchuzi wa samaki wa aina tofauti. Ule basic kabisa usikose 12000 kwa familia ya watu wanne...lakini kwa grade zingine material zinaongezeka. Ndo mara makange, fish curry, samaki wa kupwaza (kama sijakosea). Kuna grade za samaki pia, na aina tofauti za samaki, akina calamari, lobsters, ngisi etc.
Sasa ufundi wa mtu utategemea na materials zilizopo, kama kuna mtu analalamika na anaacha dusco la maana la viungo kununuliwa ili ale vizuri ni HAKI yake kulalamika. Lakini kama huachi hela, unalalamika kutwa kuchwa mkeo hajui, huku unambana hata lotion yake anakosa, unategemea afanyeje, atapiga panga hela ya chakula.
Kuna nyumba nilikwenda, yule dada alinipikia kitu hicho, mpaka nikasema mi ni mwanamke lakini hapa nasurrender. Lakini kwa gharama za ile kazi...haikuwa chini ya 50k... Kwa meal moja TU. Kaka zetu mnaacha ngapi mezani?
😅😅😅😅Women empower, hao ni wana harakati, yuko radhi akukunulie chips lakin asipike
Sie wengine kupika ndio kipaumbele chetuKitendo cha mwanamke kutokujua kupika tu probably pia hajui kufua, hajui kudeki yeye ni mfuga kucha, mpaka makeup hata kitanda hajui kutandika, haoshi vyombo ni mvivu ukimuoa jiandae kumsusia nyumba kwa uchafu, kila kitu atategemewa dada wa kazi.
Ndo aina ya wanawake ukimwambia akuchemshie hata chai anakuuliza kwani we huna mikono?
Mpishi wetu 😘😘😘Kupika ni elimu pana lazima ujifunze
Kuweza kuchanganya vitu viwe na ladha ni elimu inahitajika
Pia ni hobby kupenda kile kitu
Mwanamke km hawez huenda kakosa hiyo elimu au Hana mapenz na kupika so ni kawaida sio ajabu mpike nyinyi Sasa😀
Kila napozidi kukusoma nakuona mtu mwenye mitazamo ya kizamani, unahukumu watu kwa kutazama zaidi mionekano yao ya nje, wakati kipimo sahihi cha kumhukumu mtu kwangu ni kukaa nae karibu, upige nae story, hapo ndipo utapata nafasi nzuri ya kumjua ni mtu wa aina gani.Tafsiri ya kujipenda inatofautiana. Sijui kwako unaitafsirije. Tukikubaliana kujipenda ni nini tunaweza kufika muafaka otherwise tutatofautiana tu. Mfano mm naweza sema kujipenda ni kuoga uwe msafi uchane nywele ila wewe ukasema kujipenda ni kuweka kucha za bandia na kung'oa nyusi upake hina kila baada ya siku mbili hapa hatutafika muafaka, tutabishana badala ya kujadili sababu tafsiri ya kujipenda ni tofauti.
Maisha hayapo fixed kama mwamba, yapo tofauti tofauti ndo maana hapa tumetofautiana tayari mtazamo.
Mwanamke ambaye kipaumbele chake ni kope, nyusi, kucha, kigodoro hafanyi hayo kwa ajili yako tu, ni either kazi yake inamlazimsha au anataka kuvutia wanaume. Huwezi niambia asubuhi mkeo atatumia nusu saa kurekebisha kigodoro kikae sawa kwa ajili yako kwa gharamaya kukosa muda wa kuandaa chai ambayo ungeinywa, Suala la kujiamini ni suala lako umelifikiri tu.
Hakuna sehemu yoyote nimesema mwanamke wa kijijini, sijasema kuibiwa, sijaongelea kuchapiwa. Ni assumption ulizojitengenezea, scenario za kufikirika ulizojitengenezea. Hapa tunaongelea vipaumbele vya mwanamke. Kama kipaumbele ni kucha, kope, kigodoro usitegemee atatenga muda wa iliki, nazi, mdalasini zaidi ya hivyo vitu ambavyo ni kipaumbele kwake. Na hivyo vitu si kwa ajili yako wewe mume wake tu.