Kumekuwa na wimbi la wanawake wengi kutokujua kupika wakuu nn chanzo mana inakera

Mtu kutokujua kupika ni maamuzi tu.

Yani uwe na dhamira kabisa ugali, wali maharage vikushinde kupika!
Hiyo dhana uliyonayo ndiyo walionayo wanawake wengi, kuwa ukizaliwa mwanamke tayari unajua kupika, kwa dhana hiyo ni kweli kula mtu anajua kupika.
Ila kwa wengine kupika kuna ufundi wake kujua namna ya kutengeneza vyakula mbali mbali, na vikawa vitamu.

Mfano: mapishi ya pilau wengi wanapika pilau pori, nyama zinapikwa nje, ya pilau. Tabia ya pilau ukituta limeandaliwa vyema, lazima ushibi haraka, ila haya mapilau ya kula mchuzi au maharage ni shida.
 
Kupika ni elimu pana lazima ujifunze
Kuweza kuchanganya vitu viwe na ladha ni elimu inahitajika
Pia ni hobby kupenda kile kitu

Mwanamke km hawez huenda kakosa hiyo elimu au Hana mapenz na kupika so ni kawaida sio ajabu mpike nyinyi SasaπŸ˜€
 
Na hapa niongezee, kuna watu hapa wanalalamika wanawake zao hawajui kupika, muulize amemuwezeshaje mwanamke huyu. Huwezi kutaka mtu amalize ufundi na huku budget unambana. Chakula kitamu ni gharama, utake, usitake.

Kwa mfano kuna mchuzi wa samaki wa aina tofauti. Ule basic kabisa usikose 12000 kwa familia ya watu wanne...lakini kwa grade zingine material zinaongezeka. Ndo mara makange, fish curry, samaki wa kupwaza (kama sijakosea). Kuna grade za samaki pia, na aina tofauti za samaki, akina calamari, lobsters, ngisi etc.

Sasa ufundi wa mtu utategemea na materials zilizopo, kama kuna mtu analalamika na anaacha dusco la maana la viungo kununuliwa ili ale vizuri ni HAKI yake kulalamika. Lakini kama huachi hela, unalalamika kutwa kuchwa mkeo hajui, huku unambana hata lotion yake anakosa, unategemea afanyeje, atapiga panga hela ya chakula.

Kuna nyumba nilikwenda, yule dada alinipikia kitu hicho, mpaka nikasema mi ni mwanamke lakini hapa nasurrender. Lakini kwa gharama za ile kazi...haikuwa chini ya 50k... Kwa meal moja TU. Kaka zetu mnaacha ngapi mezani?
 
Kizazi Cha ef2 au Generation Z
Wife angu nikizaz ch ef2 ayo mambo nagombana naye Kila siku, Leo kanunua kuku bloiler nusu aliekaangwa kanipikia na ugali, hii nimekuta kwenye hotpot nilivorudi mishee wazee..πŸ˜„ Af kimelala na kinataka mambo.
Umemuachia shingapi?
 
Uongo uongo tu...una sample size ya watu wangapi??
Siku hizi online classes kibao, youtube imejaa... people learn
Plus tasty food is not cheap....
Ukiwa unataka kuoa mpeleke shule ya mapishi akifuzu ndo ukatoe mahari, otherwise acha shobo
 
Na wewe kwa akili hizi unajihesabia kabisa kwamba utakuja kuolewa! Labda ujioe mwenyewe hakuna mwanaume timamu anahitaji mke wa aina yako wallah!
 
Mabint wenyewe siku hizi wao ni kuzalishwa tu majumbani kwao hawajui kupika, hawajui kufua, hawajui kuandaa watoto na malezi yote kwahiyo wanazaa madanga watarajiwa na mashoga watarajiwa nani ana haja nao waendelee tu na u ferminism wao wajioe wenyewe tuu
 
Suala zima ni malezi ambayo mtoto wa kike ameyokulia. Ikiwa kama familia aliyokulia ina wasaidizi wa kazi za nyumbani, na huku muda wake mwingi wazazi wakimsisitiza autumie kwa mambo ya kitaaluma ni lazima suala la mapishi binafsi litampa changamoro.
JANGA JIPYA LA WANAWAKE WENGI KUTOKUJUA KUPIKA NN CHANZO!
Lakini pia wapo wanawake wavivu na wenye kuedekeza urembo hasa kucha zao. Hawa ni balaa sana kwa makusudi huwa wanakwepa shighuli za nyumbani ikiwemo mapishi.
 
Tunaacha elfu 3 milo mitatu kwani haitoshi?
 
mpaka nimefika umri huu sintokuja kusumbuana na hv viumbe ni kwenda navyo sawa tu. hajui kupika achana naye kamata goma lingine ambalo unaona ili madhaifu yake yanavumilika maisha yaende....no more talking
 
Sie wengine kupika ndio kipaumbele chetu
 
Kupika ni elimu pana lazima ujifunze
Kuweza kuchanganya vitu viwe na ladha ni elimu inahitajika
Pia ni hobby kupenda kile kitu

Mwanamke km hawez huenda kakosa hiyo elimu au Hana mapenz na kupika so ni kawaida sio ajabu mpike nyinyi SasaπŸ˜€
Mpishi wetu 😘😘😘
 
Kila napozidi kukusoma nakuona mtu mwenye mitazamo ya kizamani, unahukumu watu kwa kutazama zaidi mionekano yao ya nje, wakati kipimo sahihi cha kumhukumu mtu kwangu ni kukaa nae karibu, upige nae story, hapo ndipo utapata nafasi nzuri ya kumjua ni mtu wa aina gani.

Wewe unaonekana kabisa ukitembea barabarani ukamuona mwanamke na kucha ndefu tayari kwako hafai, coz una small mind ya kuhukumu muonekano wa mtu kwa nje, kama ungekuwa na upeo mkubwa, ungekaa nae karibu umsome, tena anaweza hata kukufundisha mambo kwenye haya maisha.

- Dunia inabadilika ila wewe unajidai kugoma kubadilika nayo, ajabu hapo unatumia smartphone moja ya badiliko la dunia, sasa kwanini hutaki wenzio wabadilike kwa namna yao?

Leo akitokea mwanamke akasema mwanaume anaetumia smartphone hajui kulea familia, utaweza vipi kumkatalia ikiwa nawe tabia yako ni kuhukumu juu juu?!

Mwisho kutofautiana msimamo kati yetu ni lazima iwe hivyo, kwasababu watu wenyewe tumeumbwa tofauti, ndio maana kuna warefu na wafupi, wembamba na wanene, maji ya kunde na weusi au weupe, sasa wewe unapolazimisha tufanane mitazamo mimi nawe ili twende sawa hapa, nao ni upeo wako mwingine duni unaonionesha.

Bado unaishi ndani ya box, toka nje uijue dunia, halafu ukiona watu wanajadili mambo yao next time, usipende kudandia sema kwasababu ya upeo wako mdogo, sikulaumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…