Kwanza atakosa sehemu ya utambulisho wake.
Kadri watoto wanavyokua huanza kuuliza, mimi ninafanana na nani?, Familia yangu ni ipi?, Baba yangu ni nani?
Hayo ni maswali ya kawaida ya kibinadamu, kukosa majibu kunaweza kuacha pengo la kihisia kwa baadhi ya watoto.
Jambo lingine muhimu mtoto atakosa historia ya ukoo wake na taarifa muhimu za kiafya, kuna magonjwa mengine au tabia za kurithi ambazo ni muhimu kuzijua kutoka pande zote za wazazi.
Kwahiyo issue ni kama baba ni mtu mwema, mtoto anaweza kupoteza fursa ya kupata jambo la ziada ambalo lingeongeza thamani katika maisha yake.
That's the real issue.