Kuna anayejua Pesa za Kodi, Tozo, Misaada na Mikopo zinakwenda wapi?

jitahidini muwe na uwezo mkubwa wa kufikiri nchi hii inakusanya pesa nyingi sana kwa mwezi
Zinajulikana mwaka jana ni Trilioni 18 zilikusanywa na Budget ya mwaka jana iliotekelezwa ni trilioni 24, trilioni 7 kati ya 18 zilitumika kulipa deni la taifa, so effectively trilioni 11 ndio zilikuwa kwa ajili ya kufanya Mambo muhimu ya kitaifa kama Afya, Elimu, mishahara etc. Hizo nyengine tumetembeza bakuli tusaidiwe.

Unlike you natumia data kuelezea hoja yangu, wewe huna data unataka tu tuanze ku guess ili tutengeneze nadharia za ajabu ajabu.
 
We unamwulizaga nani? Huko kijiweni kwenu?
 
Kwanza angejiuliza ni watanzania wangapi wana akaunti benki. Ni wachahe sana, sana sana ni wafanyakazi wa umma na binafsi maana lazima mshahara upitie benki. Wengine hata humu JF ni bendera fuata upepo hawana akaunti benki. Mfanyakazi lazima kila mwezi atafanya muamala hata moja akiamua kutoa mshahara wake wote vinginevyo atafanya miamala kadhaa.
 
mshahara umetoka mkaangalie hayo mahela mmepata kiasi gani ?
 
Unapolipa Kodi betting umelipa wewe imelipa kampuni ya Kubeti?
Mkuu ukishinda million 100, serikali inakukata MSHINDI at least 12-18M.

Kingine Kodi nyingi ni shiftable, mfano gari linapotoka kiwandani Bei yake ni million 5 lakini mpaka lifike downstream market Bei ishafika 8m hapo ukinunua wewe na kuagiza kwa CFI unakuta limefika 15M hivi unadhani hiyo 10m iliyoongezeka hakuna ushuru uliohamishwa kutoka Kwa TOYOTA kuja kwa mlaji wa mwisho??

Bei za bidhaa zote zimechajiwa kwa wazalishaji ila wao wanapouza Wana include Ile Kodi waliyokatwa so mwisho wa siku WEWE unailipa sio WAZALISHAJI tena.
 
Hujanielewa concept yangu, kinachotakiwa ni VALUE sio QUANTITY ya walipaji!! Kodi ya FDIs kubwa 100 zina offset Kodi za wamachinga wote!!

Kingine unielewe, Kodi nyingi in VALUE zinatokana na indirect tax, haya matozo, Kodi za miamala, VAT kwenye bidhaa zinaingiza pesa nyingi kuliko PAYE au Corporate Tax!! Sababu Kila mtu ananunua bidhaa whether ana kazi au Hana, ila hao wanaolipa DIRECT TAX ni fraction tu ya tax base.

So ni makosa kudhani waTanzania million 30 hawalipi Kodi ilihali wananunua bidhaa ambazo kama nilivyoeleza hapo juu Zina SHIFTABLE TAX yaani mzigo wa Kodi wa mzalishaji anaishia kulipa mteja wa mwisho.
 
Wasukuma mnapata tabu sana na mama yetu samia.

Hebu tupe hizo tozo zilizoongezeka na zilizoondolewa ili tuchanjue.

Unakumbuka yule Gaidi watu wamekufa kwa stroke alopowaibia pesa mabenki?

Bureau de change ngapi alowachukulia hela zao..
MO alitoa ngapi.
Mama anaupiga mwingi, no wizi lakini kazi zinaendelea kama kawa
 
huyo Jamaa ni mr Perfect
 
no wizi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
mi sio Msukuma mkuu
 
Naona pesa ya mshahara iliyoongezwa yote inarudi kupitia Tozo bado mnashangilia tu
 
Hujanielewa concept yangu, kinachotakiwa ni VALUE sio QUANTITY ya walipaji!! Kodi ya FDIs kubwa 100 zina offset Kodi za wamachinga wote!!
Kinachotakiwa ni haki kukiwa na Haki automatically makusanyo yataongezeka naongea hivi kama mfanyabiashara mzoefu nafahamu Abc za biashara,

Wewe unauza madera, mbele yako kuna machinga anauza madera, machinga anaeka faida 500 automatic utarespond na wewe kumatch price ama hata kupunguza kidogo, sababu yeye halipi kodi utahitajika na wewe usilipe kodi, situation imekuforce kufanya hivyo.
Hio indirect inatokana na direct kulipa kodi, direct ametimiza wajibu wake, na toka mwanzo nimejenga hoja kodi ni ile uliolipa kwenye source ya kipato chako, ni kudanganyana ukwepe kodi ya kipato chako useme mpesa ama kununua bidhaa umelipa kodi. Logic hii ikiendelea hata Bakhresa nae hatalipa kodi, huenda na yeye atafanya miamala mikubwa kuliko sisi.
So ni makosa kudhani waTanzania million 30 hawalipi Kodi ilihali wananunua bidhaa ambazo kama nilivyoeleza hapo juu Zina SHIFTABLE TAX yaani mzigo wa Kodi wa mzalishaji anaishia kulipa mteja wa mwisho.
Mkuu unashindwa kuelewa kitu hapa, Chimbuko la hizo Shiftable tax unalosema ni wapi? Ni kulipa kodi, sababu kuna mtu analipa kodi wewe unanunua ndio maana kodi imelipwa.

Msemo wako hautofautiani na kumshauri mkulima avune tu na asipande.

Hawa wa sasa wakiwa wanakimbia kodi na usubirie kodi zitoke kwa biashara kubwa tu
1. Biashara ndogo zitanawiri sababu zitakua na price advantage over biashara kubwa
2. Biashara za kati zitaongezeka kinyemela na nyingi zitakua hazilipi kodi
3. Biashara kubwa zitakwepa kodi kupitia biashara ndogo
4. In long run mapato yatapungua sana.

Na ndio tatizo kubwa tunaloface sasa hivi kama Nchi watu wengi sana hawalipi kodi ili kuongeza mapato inabidi wale wachache waminywe.
 
Yes lakini mlipaji aliesababisha kodi iingie ni mwanzilishi wa hio biashara, usingeshinda wewe hio betting angeshinda mwengine kivyovyote kampuni ingelipa kodi, hizo kampuni zinaandika kabisa shinda donge nono milioni kadhaa kwa wiki, imeshaandikwa na inajulikana kodi italipwa that week.

Same kwa magari serikali inajua exactly magari mangapi ya Toyota yameingia na kodi imelipiwa akiuza anaenda tu kufanya mahesabu sometime hata cash haitoki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…